Nami nataka niuone huo ujasiri wa bunge hata baada ya kupewa hayo maamuzi ya mahakama kuu kuendelea na majadiliano ya acc. ya escrow. Nakubaliana na wachangiaji waliosema hii ilikuwa njia ya kuwafariji au kuwapoza wabunge. Pia uelewe zoezi hili likiendeshwa kwa kichwa ngumu tu madhara yanaweza kuwa makubwa kuliko mafanikio. Kwa kuwa bunge likiamua kuwawajibisha wahusika wanaweza kukimbilia mahakamani kwa madai wamewajibishwa isivyo halali na mahakama kuwapa haki. Hata hivyo ikiamuliwa washtakiwe ili pengine wafungwe au warudishe hela zilizoibiwa bado itabidi wafunguliwe kesi mahakamani na itaonekana wameonewa kwani lilishakuwepo zuio kabla ya kuwajibishwa kwao na tayari umeshajengwa uhusiano m-baya baina ya hii mihimili miwili. Mshindi hapo ni waziri mkuu ambae alishatoa tahadhari kwa bunge. Tusubiri tuone na kesho Makinda atakacha hicho kiti chake.