Kitachompata Iran, kitaweka Historia

Kitachompata Iran, kitaweka Historia

Usiamini sana hilo. Mataifa yapo makini sana kutojiingoza katika vita visivyokuhusu moja kwa moja kuogopa madhara utakayoyapata kiuchumi.

Israel imewahi kuishambulia Iran mara kadhaa au kwa kupiga vinu vya urutubishaji wa nuclear energy au kwa kuua wataalam wa Iran wanaofanya kwenye vinu hivyo. Si Mrusi, si Mchina, aliyenyanyuka kwenda kupambana na Israel.

Uchumi wa Mchina unaenda kombo, hawezi kujiingiza katika vita vya kumsaidia tu rafiki. Na wala mchina hamkaribii Mmarekani katika teknolojia ya kivita, na hana infrastructure ya kuendesha vita katika mataifa ya kigeni.

Mrusi naye ana shida juu ya uchumi wake. Kiteknolojia japo hamfikii Mmarekani lakini ana uwezo wa kumsumbua. Lakini Mrusi, kama alivyo Mchina, hana infrastructure ya kuendesha vita nje ya Taifa lake. Kuzorota kwa uchumi wake kwa sasa ni sababu nyingine itakayomfanya ajifikirie mara mbili kabla ya kuingia miguu yote kupambana na Marekani. Uchumi wa Russia ni kama 8% ya uchumi wa US. GDP ya Russia ni chini ya GDP ya jimbo Texas.

Pamoja na mambo mengine, vita hutegemea sana uwezo wako wa kifedha.
Hivi ni vichekesho mkuu ebu twink twise
 
Wanasita kwa sababu ya bihashara ya mafuta itaingia kwy kuporomoka vibaya sana, maana saudia anazarisha 10% ya mafuta ya dunia, sasa kuingia kwy vita bila kuangalia upande wa bihashara unakuwa mtu wa kukurupuka sana,
Hivi USA alipoishambulia Iraq hakujua kama kuna biashara ya mafuta?
Kubali tu bwana mkubwa ushawishi wa USA umepungua duniani kama CCM ilivyopoteza ushawishi hapa nchini
 
Sijawahi kufika huko uswahilini DDC club ya kkoo
Wewe ni mshamba sana kama upo DSM. Na ujawahi fika DDC Kariakooo. Maana hata jengo la Simba ujui lilipo hata Kariakooo huijui. Haya ndio matatizo ya kubishana kwy keyboard mtu anajitamba kumbe hata vitu haviju hata uwanja wa ndege ujui upo wapi?kazi kweli kweli
 
Hivi USA alipoishambulia Iraq hakujua kama kuna biashara ya mafuta?
Kubali tu bwana mkubwa ushawishi wa USA umepungua duniani kama CCM ilivyopoteza ushawishi hapa nchini
Watu tunashauri maswala ya msingi wewe una leta maswala ya CCM. Wewe umerogwa na iyo CCM yako.

Ugali maharagwe umeharibu akili za watanzania, wanawaza CCM tuuuu
 
Debris from drones and missiles that Saudi Arabia says prove Iranian involvement in oil installation attacks.

Saudia inasema muelekeo wa mashambulio unaonyesha makombora hayawezi kuwa yametoka Yemen
Wizara ya ulinzi Saudi Arabia imeonyesha inachosema ni masalio ya ndege zisizo kuwa na rubani na makombora yanayothibitisha kuhusika kwa Iran katika mashambulio dhidi ya vituo vyake viwili vya mafuta mwishoni mwa juma.
Imesema ndege 18 zisizokuwa na rubani na makombora saba yalifyetuliwa kutoka muelekeo unaoonyesha kwamba hayawezi kuwa yanatoka Yemen.
Waasi nchini Yemen wanaoiunga Iran mkono wamesema walihusika na mashambulio hayo.
Iran imekana kuhusuika kwa namna yoyote na kuonya kwamba italipiza dhidi ya shambulio lolote dhidi yake.

Marekani imeendelea kuituhumu Iran kuhusika na mashambulio hayo. Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo amesema baada ya kuwasili Saudia hapo jana Jumatano kwamba ilikuwa ni 'hatua ya kivita'.
Rais Donald Trump amesema Marekani "ina njia nyingi" za kujibu.
"Kuna njia kuu, na kuna hatua nyingine zilizo chini ya hilo," amesema. "Na tutaona. Tupo katika nafasi yenye nguvu."
Nini kilichoibuka katika utafiti wa Saudia?
Ushahidi uliwasilishwa katika kikao cha wizara ya ulinzi, ambapo masalio ya ndege zisizokuwa na rubani (UAV) na makombora kutoka kwenye mashambulio hayo yaliwekwa wazi.
Msemaji wa wizara ya ulinzi kanali Turki al-Malki amesema ushahidi unaonyesha mashambulio hayo yaliidhinishwa kutoka kaskazini na “bila shaka yalifadhiliwa na Iran”.
Hatahivyo, kanali Malki amesema Saudia ingali "inashughulika kubaini eneo maalum ambako mashambulio yalitoka".
Col Malki presented maps, photographs and video from Saturday's attacks
Haki miliki ya pichaAFPImage captionKanali Malki aliwasilisha ramani, picha na video kutoka kwenye hsmabulio hilo Jumamosi
Miongoni mwa vifusi vilivyokusanywa ni pamoja na kilichosemekana kuwa ni bawa la ndege isiyokuwa na rubani aina ya Delta ya Iran.
Kanali Malki amesema: "Data iliokusanywa kutoka kwenye kompyuta inaonyesha ni ya Iran."
Amesema ndege hizo 18 zilipeperushwa katika kituo cha mafuta cha Abqaiq na makombora saba yakafyetuliwa katika maeneo yote yaliolengwa.
Makombora manne yalifyetuliwa dhidi ya kituo cha mafuta cha Khurais na mengine matatu yalianguka karibu na Abqaiq.
A map showing Saudi oil strikes

Kanali Malki amesema taarifa kuhusu maeneo ambako makombora hayo yalikotoka haiwezi kutolewa kwa sasa lakini punde watakapobainisha hilo watalitangaza.

Amesema: "Licha ya jitihada nzuri kutoka kwa Iran kufanya ionekane hivyo, ushirikiano wake na maeneo ya karibu kuunda hoja hii ya uongo in wazi."
Ameyataja mashambulio hayo kuwa "shambulio kwa jumuiya ya kimataifa… Wale waliohusika wanapaswa kuwajibishwa kwa hatua zao".
Hatua gani zinafuata?
Licha ya kwamba Marekani imeweka wazi kuwa inaamini Iran imehusika na mashambulio hayo, Rais Trump ameonekana kwa ujumla kusita kuhusika katika hatua za kijeshi.
Hapo jana Jumatano alisema ni "rahisi sana" kuingia katika mzozo wa kijeshi lakini amependekeza funzo jingine kutoka mashariki ya kati limedhihirisha hilo lilikuwa gumu.
Kabla ya kikao hicho cha wizara ya ulinzi Saudia kufanyika, Trump alitangaza kwamba ameagiza wizara ya fedha "kuongeza vikwazo vya Marekani" dhidi ya Iran kufuatia mashambulio hayo.
Trump amesema kutakuwa na taarifa zaidi katika saa 48. Vikwazo vya sasa ni vipana vilivyonuiwa kupunguza usafirishaji wa mafuta ya Iran na kudhoofisha uchumi wa taifa hilo.
Pompeo baadaye alikutana na mwanamfalme Mohammed bin Salman, kujadili muelekeo wa hatua kuhusu suala hilo.
Wataalamu wa Umoja wa mataifa wameelekea Saudia kufanya uchunguzi kuhusu mashambulio hayo, Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres amesema, akionya kuhusu "athari mbaya" za makabiliano makubwa.
 
Hata source uliyofuatilia wewe imekupotosha!
Kwa nini unasema visima vya Saudia vimeshambuliwa na Iran wakati Houthis wamekiri ni wao. Jaribu kufatilia source tofauti tofauti za habari. Main stream media wanapotosha sana kwa maslahi wanayojua wao
 
kama kuna wafanyabiashara makini huu ndo mda wa kuagiza mafuta hata pipa milioni mbili,uwezekano wa hii vita kutokea sasa ni 97%,
mafuta yatakuwa juu sana,

leo saudi wameomba msaada wa mafuta pipa milioni 20 toka iraq ili waweze kucover order zao,

wenye filling station huu ndo wakati wa kujiandaa na stock ya kutosha ya mafuta
 
Back
Top Bottom