Kitabu kipya cha simulizi mwezi huu

Kitabu kipya cha simulizi mwezi huu

Chilojnr

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Posts
308
Reaction score
1,354
Mwili wa msichana mrembo na maarufu Tanzania, Veronica unapatikana maeneo ya Jangwani huku ndani ukiwa na madawa ya kulevya tumboni. Polisi wanachanganyikiwa kwani hawajui ni nani hasa alihusika kumuua msichana huyo na kuweka madawa ya kulevya tumboni mwake.

Haraka sana Kamanda Masumbuko anampigia simu mpelelezi Ashrafu Maganza ambaye anafika hapo Jangwani na kuuona mwili huo ambapo kiroba chake kiliandikwa MZIGO IV. Kumaanisha ulikuwa mzigo namba nne.

Muuaji hajulikani ila Maganza anaamua kuingia kazini kumtafuta muuaji huyo. Huku akiwa kwenye harakati zake, mpenzi wa Veronica ambaye alikuwa daktari wa Hospitali ya Jeshi, Moshi Pazi anafika ofisini kwake na kumwambia naye angefuatilia kesi hiyo, yeyote atakayepatikana lazima amuue tu.

Maganza alichukulia kawaida, ila baada ya siku kadhaa, akaanza kusikia mauaji yaliyowahusu Wahindi, anapata hofu, alipofuatilia zaidi mauaji hayo, anagundua Wahindi ndiyo waliohusika Veronica, akagundua bila shaka aliyekuwa akifanya mauaji alikuwa Moshi Pazi.

Anamuita mara kadhaa mwanaume huyo na kuzungumza naye lakini hamwambii kama yeye ndiye anayewamaliza Wahindi waliomuulia mpenzi wake, anafuatilia kimya kimya na kugundua Moshi Pazi aliwamaliza Wahindi baada ya kuweka urafiki na kijana wa Kihindi aliyeitwa Govinda.

Anampiga mikwara mtu huyo lakini mauaji hayakomi, mwisho kabisa anapata taarifa kwamba mtu pekee aliyefanya mchongo wa kuuawa Veronica ni kijana wa Kihindi kutoka familia ya kitajiri, Ranjit ambaye naye marafiki zake wameuawa na Moshi Pazi kwa kukatwa vichwa na kutumiwa kwenye boksi kama zawadi.

Maganza anapata kazi mbili, ya kwanza kuufuatilia ukweli wa Ranjit kuwa kiongozi wa kumuua Veronica lakini la pili kuhakikisha anampata Moshi Pazi na ushahidi uliokamilika kwamba yeye ndiye aliyekuwa akifanya mauaji hayo.

Kazi inakuwa kubwa sana kwake, mpaka anapopata mwanga wa kuujua ukweli, tayari mauaji makubwa ambayo hakuyategemea yanatawala Posta jijini Dar es Salaam kwenye appartments za Wahindi.

Unajua nini kilitokea? Kwa nini Wahindi hao walimuua Veronica? Tukutane kitabuni hivi karibuni.

Mwandishi ni yuleyule mwenye floo laini na isiyochosha, NYEMO CHILONGANI. Wasiliana naye kwa namba 0718069269.
IMG_20210308_130917_320.jpg


Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom