Vitabu vinauwezo wa
kubadili kabisa maisha ya mtu yeyote yule. Baada ya vita vya pili ya
dunia wajapan walikuja na nadhalia iitwayo KAIZEN (Continuous improve),
yaani angalau kila siku uongeze kitu kipya kichwani chenye kukuza uelewa
wako na kuboresha maisha yako kwa njia yeyote ile.
hapa tujadili nguvu ya vitabu katika maisha ya mtu. yawezekana ulisoma
wewe au umewahi kukisikia kwa watu tushirikishane.
Kuna wengi tumebadilishwa au kuboreshwa maishani mwetu kiafya, kijamii,
kibiashara, kitaaruma,kimitazamo, kiimani, kimwili, mausihano nk kupitia
vitabu.
Kitabu gani ambacho kiligusa maisha yako au kukubadilisha na unatamani
wanajf wenzako tujifunze pia. unaweza kueleza kimekusaidiaje kwa ufupi
kama hutojali.