Kweli mkuu usemayo tatizo la elimu lina mkusanyiko wa matatizo mengi, ukianza kusolve moja moja ni hatua japo hautatatua tatizo lote. Lishe duni inadumaza uwezo wa kujifunza, fikiria mtu mwenye uwezo duni wa kujifunza sababu ya lishe duni halafu anakuwa na muda mfupi zaidi wa kujifunza kuliko Mjapan mwenye ana afya njema ya akili na kila kitu.Tuna changamoto nyingi sana katka mfumo wetu wa turathi ya maarfa kias kwamba kutatua changamoto moja au mbili ilhali zilizobak nazo n tegemezi kataka kuamua hatma ya urithi wa kimaarfa ...sidhani kama ni sahh....
Hao wa shule za majaribio za marekani walifanyia utafit mfumo wao wa urithishanaji wa maarfa(Elimu) wakaona Tatizo kuu n suala la muda...ili walitatue vzur ni lazma wadhibit na mfumo wa lishe(ni jambo muhimu sana...kuna uzi wa kitafit humu JF ambao unaegemeza Lishe (Upatikanaji wa chakula na IQ ya mtu au jamii fulan kwa mnyumbuliko wa kijiografia) ndio maana waliweza kufanyia experiment hypothesis yao na ikazaa matunda. Hopefully Iliwezekana tu kwasabab factors nyingne zilikuwa n zenye kujitosheleza.
Asante kwa mada nzuri!!
Sent using Jamii Forums mobile app
Moja ya mambo hiki kitabu kilikataa ni kuwa umuhimu wa muda mrefu wa watoto kupumzika ili akili ijichaji na kushika mambo.Kuongeza mda sio suluhisho, suluhisho ni kuanzisha semina zitakazo wapa wanafunzi mbinu za kusoma na kupenda kujituma, kwani huo mda wa free mwanafunzi anaweza akachimba vitu vingi sana, na kitu utakachokitafuta mwenyewe ni ngumu kusahau kuliko kufundishwa mda mrefu kuna kuchoka pia na mwanafunzi akakosa hata mda wa kupitia kile anachofundishwa na kufeli kukawa palepale, hivyo mda wa kutosha wa kupumzisha ubongo ili uweze kuwa fit kugain kitu kipya ni muhimu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Yap, primary unawwza msimamia vizuri. System kama hii nzuri ikianzia pale sekondari kidato cha kwanza mtu anapoanza kujifunza vitu vikubwa.Mtoto kama huyo sio lazima kumkazania sana ila kuanzia level za highschools anakuwa tayari amejielewa, na semina hizi pamoja na kula nzuri zitamsaidia, ila kwa hao wa primary schools unaweza ukamsimamia kama mzazi au mlezi au mwalimu kwa kumkumbusha kujisomea na kufanya homework na akafanya vizuri
Sent using Jamii Forums mobile app
Mada nzuri sana hii.
Lakini nadhani kabla ya kuongeza siku na masaa katika elimu yetu, cha kwanza ni kufumua mfumo wa elimu ili ubebe maana hasa ya elimu.
Elimu maana yake ni kufuta ujinga na kujenga nuru fulani kwenye akili lakini pia kuuwezesha uwezo wa ndani alioumbwa nao mtu ukae kwenye shape uweze kumnufaisha yeye alio nao lakini pia wale wanaomzunguka.
Mtu kazaliwa kwa mfano na kipaji cha muziki, anakwenda kusoma anapelekwa kusoma O level shule ya ufundi Tanga Tech, anasoma kozi za umeme, mabomba, kujenga matofali, magari mpaka kupiga randa.
Baadaye kijana huyo anafaulu kwa division one ya points 14 anakwenda kusoma PCM shule labda Milambo pale kwa miaka 2 tena.
Baada ya hapo anafaulu kwenda chuo kikuu anachukua kozi za Computer Science.
Sasa jiulize.
1.Kipaji chake cha muziki elimu yake ya miaka zaidi ya 19 mbona hakijawahi kuguswa na mfumo wa elimu??
2.Kama mwisho ulikuwa ni computer Science kwa nini kumsumbua kwa miaka yote hiyo anapiga randa na ufundi mabomba??, kwa nini asingemaliza tu darasa la saba pale pale anaanza kupiga kozi ndogo ndogo za computer huku anaendelea na masomo mengine ya msingi kama Civics, Basic Maths, History, Geography na Biology??
3.Kwa nini alienda high school kukariri ma-formula ya Organics Chemistry kumchosha tu ubongo??, kwa nini miaka hiyo miwili asingepiga diploma ya Computer Science ili akifika chuo kikuu awe ameiva vya kutosha??, badala ya kuanza kusoma what is a computer chuoni aanze kujifunza kozi za programming na hacking na nyinginezo ngumu ngumu??
Utakuta kuwa tatizo sio tu masaa na wingi wa masiku ya kukaa darasani, tatizo elimu yetu imejaa makoro koro mengi ambayo hayamsaidii kijana zaidi ya kuchosha tu ubongo wake.
ExactlyHapo ndiyo inabidi tuwaongezee zaidi muda wa kukaa shuleni.
Ni kweli mkuu.Na kiukweli hapa ndio wenzetu wanapotupiga gap. Ukikaa darasa moja mfano na wazungu, utagundua kua hawa jamaa sio kwamba wana akili sana la hasha! Ila wao ni perfectionists kwenye kila wanachokifanya kwa maana ya kwamba mtu anaanza ku specialize kwenye ka eneo kamoja tu tangu akiwa mdogo. Ndio maana unakuta kijana wa miaka 16 aliebobea kwenye computer huwezi kumlinganisha na PhD holder wa hapa Tz. Ila ukimuuliza mambo nje ya taaluma yake ni sifuri. Hapa kwetu unadonoa donoa kila kitu mwisho wa siku hakuna unachokijua.
Mtaji kwao akina nani?Ni wazo zuri mkuu, lakini nani anataka vijana wetu wafute ujing?
Ujinga wetu ni mtaji kwao
Sent using Jamii Forums mobile app
Hii inaweza ikawa kweli.Wenzetu watoto wapo free sio kama kwetu mtoto akirudishuleni anaingia jikoni kupika,kwenda shambani,ngombe nk. Sidhani kama itawezekana.
Mkuu kukaa shuleni ili iweje? Bado hujasolve tatizo. Elimu bongo ina matatizo mengi sana..Hapo ndiyo inabidi tuwaongezee zaidi muda wa kukaa shuleni.
Ni kweli. Inatakiwa kusolve mojamoja. mfano mda wa kusoma kwa watanzania ni mdogo sana. Tunatakiwa kuongeza itabaki vitabu, maslahi ya waalimu, maabara, upatikanaji wa chakula shuleni nk.Mkuu kukaa shuleni ili iweje? Bado hujasolve tatizo. Elimu bongo ina matatizo mengi sana..
Sent using Jamii Forums mobile app