Ndugu wana jamvi mtakumbuka kuwa katika taarifa aliyotoa Mtikila majuzi juu ya tukio la mlipuko wa bomu Arusha alisema kuwa taarifa aliyowahi kutoa kuwahusisha CDM na mauaji ya Chacha Wangwe inafanyiwa 'finishing' kabla ya kusambazwa nchi nzima kama kitabu...
Ni wazi kwamba Mtikila anatumika tu kama editor wa 'kitabu' hicho huku author(s) wakiwa ni mahasimu wakuu wa CDM ambao wote tunafahamu.
Naomba niwatahadharishe CCM na style hiyo wanayotaka kufanya kwa kueneza uongo kwa njia ya kitabu. Endapo kama wataendelea na mpango huo dhalimu, naamini kuna wanaharakati na wapenda mabadiliko watakao-counter attack kwa kueneza ukweli wa unyama, manyanyaso, na udhalimu wa CCM kupitia polisi uliowahi kutokea nchini tangu ilipoingia awamu ya nne.
Narudia tena, picha zipo na mashahidi wapo, na ukweli unajulikana. Kuanzia mauaji ya tarime, Ngara, Mwangosi, Igunga, Songea, Mtwara, Zanzibar (padre), Arusha (kanisani), Arusha (mkutano wa CDM), bila kusahau picha za kukamatwa, kuteswa kwa viongozi wa CDM, Ulimboka, Kibanda na wengine.
Ni wazi CCM wakitoka na hiyo singo yao ya uongo kuhusu Wangwe, na CDM wakaja na habari za ukweli kuhusu utekaji, utesaji na mauaji ya CCM, vyote vikawekwa katika 'vitabu', na kusambazwa nchi nzima, tunajua ni ipi itauza zaidi...
Nawaonya tena CCM kwa mara ya mwisho katika hili...