Kitabu cha hadithi ya Kiswahili ya Willi Gamba kinahitajika haraka

CHAI CHUNGU

JF-Expert Member
Feb 20, 2012
7,113
930
Ndugu wana jf naomba kama kuna mtu anakitabu cha ile hadithi maarufu ya Willi Gamba na mwana dada Tausi aniuzie,nina kihitaji sana na nilikisoma takribani miaka 19 iliyopita.
 
Musiba aliandika vitabu vingi vinavyohusu Will gamba mplelezi mashuhuri barani africa ambaye alikuwa anateketeza mfumo wa kijasusi wa kuwaua wapigania uhuru enzi hizi -- kati ya hivi unataka kibabu kipi?

Kikomo
Njama
Kikosi cha kisasi
Hujuma.
 
Ndugu wana jf naomba kama kuna mtu anakitabu cha ile hadithi maarufu ya Willi Gamba na mwana dada Tausi aniuzie,nina kihitaji sana na nilikisoma takribani miaka 19 iliyopita.
Dada Cheusi;
Naona kama kwa level na umri uliofikia haustahili tena kusona vitabu au novel za kiswahili, waachie kindergatten na shule za Msingi.
Nakushauri badala yake usome novel za James Hardley Chase zipo nyingi mtaani zimezagaa, utapata satsfaction mara 10 zaidi ya kurudia kusoma hiyo novel ya kiswahili.

Kumbuka pia kuwa Musiba alikuwa anaiga utunzi wa Chase, ndiyo maana akaweza kutunga novel zilizoweza kukuvutia. Just imagine kusoma novel za yule aliyeigizwa na Musiba sijui itakuwaje. Try it out and you will tell me.
 
Kule jukwaa la elimu, jukwaa la lugha, jukwaa la burudani ama jukwaa la matangazo wapo wadau wa Willy Gamba. Jaribu kuhamishia bandiko lako huko!
 
hata kusoma novel za kiswahili kuna umuhimu wake
1. Kukuza soko la sanaa/utunzi wa ndani
2. Kukuza lugha
3. Kutunza kumbukumbu za kazi za ndani
4. Sentimental value, hadi leo na uzee wangu bado nasikiliza Marijan Rajab, na vitabu vingi nilivyosoma darasa la pili
 
Chase anapigana na wauaji wapigania uhuru?
Hata hivyo unaonekana sio msomaji wa novels na wala huwajui watunzi wakali kama kina Sydney Sheldon
Dada Cheusi;
Naona kama kwa level na umri uliofikia haustahili tena kusona vitabu au novel za kiswahili, waachie kindergatten na shule za Msingi.
Nakushauri badala yake usome novel za James Hardley Chase zipo nyingi mtaani zimezagaa, utapata satsfaction mara 10 zaidi ya kurudia kusoma hiyo novel ya kiswahili.

Kumbuka pia kuwa Musiba alikuwa anaiga utunzi wa Chase, ndiyo maana akaweza kutunga novel zilizoweza kukuvutia. Just imagine kusoma novel za yule aliyeigizwa na Musiba sijui itakuwaje. Try it out and you will tell me.
 
Na mimi navihitaji vitabu vile vyote vya musiba mwenye navyo anistue nitavinunu kwa gharama yeyote ile,kuna mahali humu nilishaitisha hivi vitabu but sikupata mpokeo mzuri
 
Ndugu wana jf naomba kama kuna mtu anakitabu cha ile hadithi maarufu ya Willi Gamba na mwana dada Tausi aniuzie,nina kihitaji sana na nilikisoma takribani miaka 19 iliyopita.

Hicho ni "Njama". Kama ingekuwa nchi nyingine, marehemu Musiba angekuwa ni milionea ($$ wise).
 
Musiba aliandika vitabu vingi vinavyohusu Will gamba mplelezi mashuhuri barani africa ambaye alikuwa anateketeza mfumo wa kijasusi wa kuwaua wapigania uhuru enzi hizi -- kati ya hivi unataka kibabu kipi?

Kikomo
Njama
Kikosi cha kisasi
Hujuma.

Umesahau na kile cha 'kufa na kupona'
 
Chase anapigana na wauaji wapigania uhuru?
Hata hivyo unaonekana sio msomaji wa novels na wala huwajui watunzi wakali kama kina Sydney Sheldon

Ni kweli mzee, love stories kama "THE OTHER SIDE OF A MIDNIGHT", kusema kweli siwezi, wewe niletee mastermind stories kama "A COFFIN FROM HONGKONG", hapo ndiyo umenifikisha, au true stories documentaries za kwenye DStv kama vile FBI Files, Forensic Detectives, etc hapo ndiyo kabisa unakuwa umenifikisha penyewe, tunaweza kukesha!
 
Huyo anataka kitabu cha "HOFU" au "KUFA NA KUPONA" maana kati ya vitabu hivyo kuna warembo Nyaso na Tausi maana mwenyewe nimesoma miaka 17 iliyopita.
 
Why ,!hakuna wakina willy,benny mtobwa

Niliwasoma nikiwa Form II, k.v. najisikia kuua tena, Salaam kutoka Kuzimu, Simu ya Kifo,.... Willy Gamba, wizi wa almasi mwadui, kuna yule kichaa alikuwa anatembea mtaani amevaa malapulapu anaokota makopo mitaroni halafu kila wakati anakaa anasema maneno kwa kurudia rudia "SAA ZA AFRIKA, SAA ZA AFRIKA,..." kumbe alikuwa anamaanisha South Africa, amabako nako pia kuna almasi! We acha tu enzi hizo ilikuwa prep zinakatika kwa mwendo wa novel siku za kwanza baada ya kutoka likizo!
Said M. Bawji je? Usiku wa balaa!
 
musiba aliandika vitabu vingi vinavyohusu will gamba mplelezi mashuhuri barani africa ambaye alikuwa anateketeza mfumo wa kijasusi wa kuwaua wapigania uhuru enzi hizi -- kati ya hivi unataka kibabu kipi?

Kikomo
njama
kikosi cha kisasi
hujuma.

tafadhali mr. Fuso nami ni mwanachama wa jf japokua nitakua nimeingilia kati uniwierathi,mimi nilikua na hamu ya kuipata hiyo story ya njama kuppitia internet tafadhali niwezeshe kuipata hiyo story pkeas i bag you.
 
mwenye uwezekano wa kutuwezesha kuvipata atupatie mawasiliano yake mimi navitaka vyote nifanye marudio nilishavisoma ila nahitaji kuvisoma tena maana vinasisimua
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom