zubek
Member
- Sep 9, 2017
- 7
- 5
Habari za muda ndugu, jamaa na marafiki? Mada tajwa ni swali tosha kuwakamata kidato cha nne, cha sita na hata wanazuoni ambao wamewekeza katika elimu, hususan lugha ya kiswahili. NECTA, TUKI pamoja na vitivo mbalimbali katika vyuo vikuu hapa nchini, mtaala na vitabu kadha wa kadha, tumezoea kukutana na maswali kama vile:
1. Kiswahili ni kiarabu, jadili.
2. Kiswahili ni kibantu, jadili. N.k.
Sasa leo tujadili hili, je, kiswahili ni kiingereza? Au la?
>>>> Kwa upande wangu, kuna maneno mengi saaana ya kiingereza ambayo tunayatumia katika lugha ya kiswahili, hasa katika nyakati hizi za utandawazi na maendeleo ya kisayansi na kiteknolojia, misamiati mingi tunayakopi na kuyapesti kama yalivyo, ukiangalia hata hapo nimechanganya tayari. Maswali ya kuzingatia misamiati, hata kiarabu tunatazama uwingi wa maneno ya lugha hiyo katika lugha ya kiswahili na kukuta maneno meeeengi, tunayatumia bila shida na tumezoea.
Swali: lugha moja yaweza kuwa nyingine kwa kigezo cha mfanano wa kimsamiati? Au uwingi wa matumizi wa misamiati ya lugha moja katika lugha nyingine yaweza kusababisha lugha hiyo kuwa nyingine ???.
Ubantu na kiswahili, je, ni uchambuzi wa kipragmatikia, kisemantikia, kisintaksia, kifonolojia au kimofolojia unaotumika kusema kiswahili ni kibantu? angalieni hata misamiati niliyotumia hapo juu na matumizi yake katika pande zote mbili, je, kiswahili ni kiingereza ???
…… Tunatumia saaana maneno ya kiingereza kwenye kiswahili, tofauti na hali ilivyo kwa upande wa kiingereza, wao hawatohoi au kukopa kiasi hicho, ni maneno machache tu, na hii ni kwa sababu lugha ni sehemu muhimu ya utamaduni, hivyo utamaduni wa afrika mashariki ni tofauti na utamaduni wa mwingereza na ulaya kwa ujumla. Hivyo wazungu wanapokuja huku, wanajaribu kutohoa maneno na kuyatumia muda mwingune jinsi yalivyo iki maana isipotoshwe, kama tu hakuna namna ya kuunda msamiati mpya kwa lugha yao. Sasa sisi ambao hata hatutembelei saana kwao, kujua utamaduni wao ambao sehemu nyingine tunashea tu, imekuwa tatizo mpaka siku hizi mashuleni na vyuoni, walimu na wanafunzi ni full kiswanglish, mchanganyiko mpaka daaaa! Hata mjengoni huwa nasikia wakichanganya...je? Kiswahili ni kiingereza?