Maxence Melo
JF Founder
- Feb 10, 2006
- 4,230
- 13,415
Nashukuru... Naambiwa computa si kiswahili fasaha. Ila huyu kanijibu kwa PM. Ati ni tarakirishi. ....
Hapo UmenenaI do think sometimes tunalazimisha maneno ya kiswahili na as a result hata haileti maana wala ladha ya Lugha. Computer ni neno geni, yaani halikuzaliwa na waswahili. Therefore kama yalivyo maneno mengine ya kigeni tuliyorithi whay not call it KOMPYUTA kama yulivyozoea yaani tunaandika kama tunavyotamka neno ingawa ni la kigeni.
WoRM, umeridhika?
Puchu - koswa, ni kama almanusura, mf. Aliponea puchu gari lilipomkaribia! kusisitiza mara nyingi husema puchu puchu yaani koswa koswa!!
Tafadhali nisaidieni NAOMBA, kunisaidia mimi ni kuusaidia umma mkubwa ambao ama kwa kutojisajili au umejisajili unachangana maneno haya.
Haya nitaanza kukusaidia kidogo:
Vundika au vumbika?
Vundika inatokana na neno "Vunda" lenye maana ya kitu kilichoharibika na kuchacha kwa sababu ya kukaa kwa muda mrefu bila kutumika na kimefanywa hivyo kwa makusudi. Ni tofauti na kitu "kuoza" Ni kwa sababu hiyo watu wanavundika mchele, mtama, ndivi n.k ili kutengeneza pombe au matunda mengine ili kutengeneza mvinyo.
Vumbika, bila ya shaka linahusiana na kitu kuwekwa vumbi!!!
Kwa leo hayo yatosha.