Kiswahili na 'Upumbavu' wa wanasiasa wetu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiswahili na 'Upumbavu' wa wanasiasa wetu!

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by ndyoko, Nov 28, 2011.

 1. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #1
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Kwenye mjadala wa Sheria ya kuunda katiba mpya, wengi tulishuhudia dhana ya kiswahili kuwa lugha muhimu ktk mawasiliano miongoni mwa watanzania ikitamalaki.

  Hata hivyo, imekuwa ni ngumu kwa wanasiasa kukubali kiswahili kutumika kama lugha ya kufundishia mashuleni-primary, sekondari na vyuo vya elimu ya juu.

  Mpaka sasa bado siwaelewi wanasiasa, iweje lugha ya kiswahili wakaona ni muhimu sana, kwamba itumike ktk mchakato mzima wa utungaji Katiba ya nchi lakini wanakiona kuwa hakifai kutumika ktk kufundishia mashuleni? Kwa mnaojua sababu hasa ya maana inayowafanya wanasiasa kukikataa kiswahili kutumika kama lugha ya kufundishia nijuzeni, tafadhali!

  Nawasubiria!
   
 2. CONSULT

  CONSULT JF-Expert Member

  #2
  Nov 29, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 223
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Mhe Ndyoko, Ni mawazo yangu, km kweli maendeleo ya nchi yeyote kwa dunia ya sasa ni mashindano ya kila nyanja na nchi zingine duniani ikiwemo biashara, ajira, technolojia, tamaduni, n.k. lugha ikiwa ni nyezo kuu mojawapo nadhani hata wewe unajua hilo na mifano unayo km wakny na watz mawazo ya kufundishia kiswahili unawarudisha watanzania hatua nyng nyuma sana usidanganywe na nchi zilizo endelea kiuchuni kutumia lugha asili yao kwani tayari wanajitoshelrza kwa mambo mengi sn sio km ss hatuna kila kitu, bado nfano china nchi nzima watu wana miminika kujifunja lugha za kibiashara na wanasaidiwa na serikali zao iweje sisi tulio hoi ? ?km ni swala la uasili na uwelewa mbona bado patakuwa na hoja za kutumia lugha za asili km kisukuma, kikurya,kisambaa zipo nchi zinafanya hivyo na uelewa utapanda je nini lengo la hy elimu ?? .,.,..,.., Tukija kwa swala la katiba kwanza ktk harakati za kuunda ni za muda mufupi tu, pili zinahusu watanzania pekee katiba haitaji kuuza nje ya nchi au kutumiwa na wamataifa, tatu ni rahisi saaannnaa mtanzania kuelewa vema kwa kiswahilli na kwa wingi zaidi kuliko lugha nyingine zezote.... kinachoangaliwa hapa ni malengo na tija kufikiwa,.,.,., nawasilisha,.,.,.
   
 3. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #3
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Nadhani bado hujaelewa lengo langu. Mimi sina maana ya kuacha kujifunza lugha nyingine. Mie hoja yangu ni kutumia kiswahili kama lugha ya kufundishia, hizo lugha nyingine ziendelee kufundishwa na kama ikibidi ziwe 'compulsory'. Unadhani mtoto/mwanafunzi wa kitanzania ataelewa vizuri zaidi akifundishwa kwa lugha gani, kiswahili au kiingereza? Hii ndo issue yenyewe. Elewa pia kwamba huo uelewa atakaoupata utakuwa na manufaa zaidi kwa Tanzania yetu halafu ndo huko nje unakoongelea. Tunaposema nchi ina tatizo la ajira hatuangalii nje ya tz yetu. Of course we are to think globally and act locally!
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Nov 29, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mkuu Ndyoko, tatizo kubwa la kushindwa kukubali kutumia Kiswahili kama lugha ya kufundishia ni kuwa hakuna maandalizi ya kutosha. Kuwa na kiswahili peke yake kama lugha, bila ya nyenzo za kufundishia kama vile vitabu na mitaala iliyoandaliwa mahsusi kwa ajili ya kukidhi haja hiyo, ni kikwazo
   
 5. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #5
  Nov 29, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,887
  Likes Received: 6,071
  Trophy Points: 280
  huu mjadala una umri mkubwa lakini umekuzwa na siasa zetu za Tanzania zilizojaa woga na unafiki!
  Je, umewahi kwenda kwenye ofisi za BAKITA (Baraza la Kiswahili la Taifa) au pale UDSM-TAKAKI!? ...kwa hakika utandaji wa kazi wa taasisi hizi pamoja na nyinginezo zinazojihusisha na ukuzaji wa Kiswahili hata zikiwezeshwa kiasi gani sidhani kama zinaweza 'ku-justify' matumizi ya hii lugha kufundishia mashuleni na vyuoni.
  Pia tusisahau kuwa waliotuletea 'formal education' waliileta na lugha zao. Na hii ina maana kuwa inakupasa kuwa unafanya tafsiri ya 'materials' yote duniani ili yasome Kiswahili kazi ambayo nasema BAKITA, TAKAKI nk sidhani kama wanaiweza!
  Nashauri (kwa uchungu lakini hakuna jinsi) tutumie Kiingereza na Kiswahili tunaweza kukitumia kwa mambo yetu ya kiasili kama jando na unyago.
  Kuna taasisi moja kubwa na ya kimataifa iliyokuwa ikijitahidi kuweka literature zake kwa matumizi ya Tanzania katika Kiswahili lakini wamegundua wale wanaong'ang'ania wafanyiwe tafsiri hata huo muda wa kusoma (culture ya kusoma) hawana na materials zinaishia kwenye shelves pamoja na 'kufungia maandazi' na majuzi tu wameamua watumie Kiingereza ili watu wa-develop spirit ya kujifunza na kujiunga na dunia nyingine badala ya kuendelea kutengwa na dunia kwa kizuizi cha lugha
   
 6. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #6
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Nakaribia kufnga mjadala!
   
 7. m

  mafutamingi JF-Expert Member

  #7
  Nov 30, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 859
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 60
  Mimi nashindwa kuelewa kwa nini kuna fikra kwamba watoto wa kiTZ hawawezi kufundishwa na kuelewa kiingereza na lugha hiyo ikatumika kama lugha ya kufundishia? Kwa nini watoto wa nchi zingine wanafundishwa na wanakielewa kimombo? Mimi sina tatizo kabisa endapo sisi kama taifa la tz tutafanya uamuzi wa kutumia kiswahili kama lugha ya kufundishia. Lakini isiwe kwa sababu tumeshindwa kuwafundisha watoto wetu kiingereza hadi wakakielewa. Sawa, nchi nyingine hutumia lugha zao kama medium of instructions lakini utakuta vijana wa nchi hizo wanazungumza hata lugha 3 za kigeni. Rai yangu ni kwamba tujenge uwezo wa kuwafundisha watoto wetu lugha za kigeni na wazielewe na baada ya hapo ndo tufikirie kutumia kiswahili kama lugha ya kufundishia.
   
Loading...