Kiswahili: Matumizi ya Herufi “L” na “R” | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiswahili: Matumizi ya Herufi “L” na “R”

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by EMT, Sep 3, 2011.

 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Wakuu nimekuwa nikisoma hapa jamvini na kwingineko watu wanapoandika wanabadilisha matumizi ya herufi “L” and “R” kwenye maneno. Kwa mfano, unakuta mtu anaandika “daradara” badala ya “daladala”, “kibari” badala ya “kibali”, “foreni” badala ya “foleni” n.k. Kwa mfano pitia hii thread: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-sheria-the-law-forum/169004-daradara-bajaji-na-bodaboda-zimepewa-msamaha-wa-kufuata-sheria-za-barabarani.html.

  Wakuu wa lugha, hivi hii inasababishwa na nini? Kuna sababu za msingi zinazofanya watu waandike hivyo? Hivi watu kama hawa wanapongea huwa pia wanatumia herufi “R” badala ya “L” au ni kwenye maandishi tuu?
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Sep 3, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Moja ya sababu ni makabila tunayotokea. Kwa mfano, kwa Wasukuma "R" hakuna. Kuna Wasukuma wengi tu ambao wanatamka maneno yenye "R" kwa kuweka "L" ambapo hiyo "R" ipo. Sasa hiyo inaweza kupelekea hilo kosa hata kwenye uandishi.

  Sababu nyingine nadhani ni kutokujua vizuri misamiati ya Kiswahili na tahajia zake. Unakuta mtu hana uhakika wa kama atumie "R" au "L" na hivyo anakuwa anabahatisha tu kwa kuchagua kutumia herufi mojawapo na kwa vile wengi wetu tunakuwa tumejua alichomaanisha basi wala hatutamkosoa.

  Pia wapo ambao huacha kuandika herufi "H" mbele ya maneno yaanziayo na hiyo herufi na wengine ambao huiweka pasipotakiwa. Kwa mfano unakuta mtu anaandika "alafu" badala ya "halafu" au unakuta anaandika "hovyo" badala ya "ovyo".

  Kwa ujumla Watanzania hatujui vizuri lugha.
   
 3. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  NN kwa hiyo hapo inaonyesha kuna sababu za msingi na zisizo za msingi.
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Sep 3, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Yeah...unaweza kabisa kusema kuwa zipo sababu za msingi na zisizo za msingi. Kwa mfano, mtu ambaye anaandika "alafu" au "afu" badala ya "halafu" huku akijua "alafu" au "afu" si sahihi utaiweka hiyo kwenye kundi gani?
   
 5. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #5
  Sep 3, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  Wengi ya watu wanaoandika/ongea hivyo huwa Kiswahili wameanza kujifunza walipoanza shule na si lugha yao ya mwanzo.

  Wanatibua sana, hususan wale wanao changanya kwenye R na L, lakini tutaendelea kuwapa darsa, humu JF wangi waliokuwa wakifanya makosa hayo wamejirekebisha.
   
 6. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #6
  Sep 3, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,403
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Hii hali ipo sana na nadhani inachangiwa na lugha mama za hao wanaochanganya.
  Naona kuna hali ya watu kuacha baadhi ya herufi kwenye maandishi yao.mathalani badala ya kuandika asubuhi mtu anaadika asubui.
  Huendi inakuwa uendi.
   
 7. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #7
  Sep 3, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Naweza Sema karibu kila post haswa ikiwa ni yenye maneno mengi huwa haikosi kasoro,na utakuta mtu anapost baadae akiipitia anakuta makosa kadhaa tizma utaona last edit was date dash dash.

  Mimi ni mhanga mmojawapo wa R na L ila huwa siogopi kutumia popote nikiwa nahitaji kufikisha Ujumbe Na Ukinikosoa huwa napata Faraja zaidi hata miaka ya Nyuma tunachat kwenye hizi chat zetu marehemu za Bongo5 chat DHW Jambo Darchat nilikuwa natupa mawe ya R na L bila wasi wasi na walikuwa wananiweka sawa.

  Kiswahili nimezaliwa nacho na ninacho bado japo sikipendi nadhani Tuliingizwa mkenge na JKN kukiendekeza mashuleni hakijatusaidia sana kwenye maendeleo ya kimataifa kuna wanaopinga ila ukweli hujitenga Uganda na kenya wamewahi

  Wachaga hawana ''Z'' Huweka ''S'' Mfano Sa Saa hisi = Za Saa Hizi

  Wakurya Mwendo ni ''R'' Kwenda mbele Rirete hiro ri mwizi turiarest Rione rimenyoa V

  Wavisiwani wengi wapo sawia
   
 8. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #8
  Sep 3, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Kama mtu akiandika hivyo wakati anajua wazi sivyo, hapo hakuna sababu ya msingi. Lakini mbona hii imejikita zaidi kwenye Kiswahili? Unafikiri mtu anayechanganya "R" na "L" kwenye Kiswahili kwa sababu za msingi au zisizo za msingi anaweza kuchanganya kwenye Kingereza? Mfano "rike" badala ya "like", Engrish" badala ya "English".
   
 9. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #9
  Sep 3, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapo kwenye red hata mimi nakosea sana spellings. Lakini kwa hili la kutumia "R" badala ya "L" sidhani kama lina uhusiano mkubwa sana na spelling. Wapo watu unakuta wamefanya editing lakini hawa edit walipotumia "R" badala ya "L" labda kwa sababu za msingi.
   
 10. bht

  bht JF-Expert Member

  #10
  Sep 3, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  EMT wapo wanaochanganya sana R na L kwenye kiingereza hasa pale kwa baba Moi, akitamka unaiskia kabisa wazi...load = road, rake=lake!

  Mi nimegundua pia matumizi ya jumbe fupi kwenye simu yana athari kwa lugha, yanajenga mazoea mabaya ya kufupisha fupisha maneno na wakati mwingine hata kuharibu maana. (aya=haya)

  Kuna kabila moja tz pia matumizi ya H na A ni tatizo (hunakuja=unakuja, hana kazi nyingi =ana kazi nyingi)

  )
   
 11. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #11
  Sep 3, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,999
  Likes Received: 2,655
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  Kwa hiyo wewe unaona umenyoosha sentesi zako vizuli?
   
 12. Kimbojo

  Kimbojo JF-Expert Member

  #12
  Sep 3, 2011
  Joined: Apr 12, 2009
  Messages: 387
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hapa hakuna dawa kwasababu ni athari za lugha mama.
   
 13. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #13
  Sep 4, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Mzee umenikumbusha mbali. Wapo watu wengi ambao huweka "R" kwenye "L". Nimeshasikia baadhi ya Watanzania wakifanya hivyo na baadhi ya Waarabu.

  Halafu ikija kwenye matamshi ya maneno ya Kiingereza ndiyo kunakuwaga na balaa. Utakuta mtu anatamka "honest" kwa kuiwekea msisitizo "H" wakati hiyo herufi kwenye hilo neno huwa ni ya kimya.
   
 14. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #14
  Sep 4, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Yawezekana japo huwezi kuwa na asilimia nyingi. mie hunichangaya haswa neno lenye R na L ndani yake Kama waluguru Sielewi ni Waluguru , Warugulu au Waruguru Walugulu Sijui lipi ni Sawa ila nikiwa nataka kufikisha ujumbe naweka lolote hapo msg Sent Hapo Vipi!

  Mkaguru! ila kuna maneno ambayo haya umuhimu.
  Nishaambiwa kule sio Vingunguti ni Mkunguti.

  Sababu Kiswahili sio issue sana haisumbui Sometime Serikali !! Selikari msg Sent
   
 15. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #15
  Sep 4, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Wakuu naona mnauzunguka mbuyu tu! The fact is mafundisho shule ya msingi yamedorora. Tanzania ya leo almost 95% wanakifahamu kiswahili tofauti na say miaka ile ya 60, 70 mpaka 80 ambapo kiswahili kilikuwa mijini tu, tena baadhi ya miji maana sehemu kama Tukuyu, Muleba au Rombo hata mjini watu walikuwa wanachapa lugha za asili. Turudi kwenye hoja:

  Ni kweli ili ujifunze kiswahili sanifu same lugha yoyote kiusanifu unahitaji mafundisho of some sort. Nakumbuka wakati ule tunaanza darasa la kwanza, la pili mpaka la tatu. Kuna watu walipata shida mno kutokona na matashi yalioathiriwa na lugha za asili

  mfano ra, re, ri ,ro ,ru au za, ze, zi, zo, zu ziliwekwa l and s respectively. To be frank enzi zile fimbo ilikuwa inatembea (Probably not applie to this day) mpaka watu wanajifunza. Nakumbuka kuna jamaa ilimchukua takribani mwezi kutamka "zamani za kale" yeye alitamka "samani sa kale". Lakini make no mistake by then mtu aliyekuwa na tatizo hili kwanza alikuwa careful akabla ya ya kulitamka neno na pili there was no way akakosea kulianndika. Na kama ukifanya uchunguzi utagundua hii ni generation problem. My own granny hakuweza kutamka meza au zulia but he would never write mesa au sulia kama alivyokuwa akitamka.

  Mimi nachokiona ni kwamba walimu shule za msingi, they don't care anymore!!!!!!!! Na hili pia indirectly ni tunda la ufisadi. On top of that nna hakika zikitafutwa takwimu za ukweli kuhusu "numeracy" and "literacy" rate in Tanzania hali ni ya kutisha kwa sasa.
   
 16. s

  seniorita JF-Expert Member

  #16
  Sep 4, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  sound systems za kila lugha is unique na zinatofautiana. The way we speak our mother tongue influence the way we speak or write other languages for most of us....Si tu consonants hata vowels at times....
   
 17. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #17
  Sep 4, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Nadhani wengine ni kutokana na matatizo ya utamkaji tu, kama vile wale wenye kithethe...! Wamezaliwa hivyo na hawawezi rekebishwa.

  Ndio maana mimi wakati mwingie humpa maiwaifu wangu kuhakiki kile ninacho wasirisha/kiwasilisha hapa! Japokuwa mimi ni mwana kindakindaki pale Gerezani Kariakoo, mitaa ya Livingstone, Somali na Kidongo Chekundu.

  Ah! Kiswahili kitamu bana ukikijuwa (ukikijua).
   
 18. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #18
  Sep 4, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hiyo sawa kabisa mkuu, lakini tatizo linakuja pale matamshi yanapoanza kufanana na maandishi!
   
 19. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #19
  Sep 4, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Ukizowea/ukizoea kusema kwa kuchanganya R na L, basi kuna hatari ya kuandika vile unavyo tamka.
   
 20. Researcher

  Researcher Senior Member

  #20
  Sep 4, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 187
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ala (R) na ero (L)..
   
Loading...