Pulchra Animo
JF-Expert Member
- Jun 16, 2016
- 3,398
- 2,990
Na mdudu mwingine hatari zaidi kwa lugha yetu hii ni pale watumiaji wake kwa makusudi kabisa wanapoamua kuchanganya Kiswahili na Kiingereza. Na bila shaka, hali inageuka na kuwa ya kuogofya maradufu pale uchanganyaji huo wa Kiingereza unapofanyika katikati ya kukitetea Kiswahili! Inakuwa ni kama Mchungaji aliyesimama madhabahuni akikemea dhambi ya uzinzi wakati huo huo akionekana waziwazi na waumini jinsi anavyomtazama kwa jicho la matamanio mmoja wa waumini wa kike aliyeketi kiti cha mbele!Mara nyingi nisomapo makala ndefu za Kiswahili sikosi kukutana na angalau neno moja la Kiswahili linaloonekana kuwa jipya kwangu. At the same time, the same article may contain a few familiar words that do not appear to conform to the standard Swahili that I learned during my early school years. Mengi ya maneno yanayoathirika ni yale yenye herufi "h", "dh", "l" na "r" ndani yake.
Na mdudu mwingine hatari zaidi kwa lugha yetu hii ni pale watumiaji wake kwa makusudi kabisa wanapoamua kuchanganya Kiswahili na Kiingereza. Na bila shaka, hali inageuka na kuwa ya kuogofya maradufu pale uchanganyaji huo wa Kiingereza unapofanyika katikati ya kukitetea Kiswahili! Inakuwa ni kama Mchungaji aliyesimama madhabahuni akikemea dhambi ya uzinzi wakati huo huo akionekana waziwazi na waumini jinsi anavyomtazama kwa jicho la matamanio mmoja wa waumini wa kike aliyeketi kiti cha mbele!
Tofautisha kati ya kuazima maneno na kuchanganya lugha!Sidhani kama hilo ni tatizo linaloweza kulinganishwa na uchafuzi wa maneno ya lugha fulani. It's common for writers (in any language) to borrow a word or words from another language. The rule is that the borrowed word(s) should be presented in its (their) correct form. Obviously, that doesn't violate any grammatical rules!
I would be OK na mtu anayechanganya kuliko anayeharbu kiswahili. Inaudhi sana ninaposoma huku jamvini maneno kama "mshahala" badala ya "mshahara", "kula" badala "kura". Ninajua kuna makabila ambayo wanashida ya kutamka maneno mengine lakini kuyaandika siku hizi imekuwa ni shida pia. Aibu !Tofautisha kati ya kuazima maneno na kuchanganya lugha!
Kuchanganya nako ni kuharibu Kiswahili... mbona hili lipo wazi?! Tena ni kuharibu kwa makusudi tofauti na wale wa "r" na "l". Au mnaona hiyo si kuharibu kwavile tunachanganya na kizungu?!I would be OK na mtu anayechanganya kuliko anayeharbu kiswahili. Inaudhi sana ninaposoma huku jamvini maneno kama "mshahala" badala ya "mshahara", "kula" badala "kura". Ninajua kuna makabila ambayo wanashida ya kutamka maneno mengine lakini kuyaandika siku hizi imekuwa ni shida pia. Aibu !
Pia ufipishaji maneno isivyo stahili inakera sana.
Sasa, unakuta imeandikwa xaxa :-/
aGgggggrrrrrrrrr!
Wewe ume borrow sentensi siyo word au words. Poor teacher
Hahahaaa. Mkuu nimecheka sana. Hizi zote ni juhudi za kujitetea?Sasa mbona unarudia kosa hilo hilo? Tena afadhali mimi sikufanya uchafuzi wa maneno; ya Kiswahili yamesimama na kujitosheleza na ya English vivyo hivyo! Angalia wewe "Ume" yako isivyojitosheleza.
huwezaKuazima maneno kutoka lugha nyingine kuja kiswahili ni njia mojawapo ya uundaji wa msamiati wa kiswahili ambapo lugha uweza kukua...ila kuchanganya lugha wakati wa mazungumzo au maandishi ni kitu kungine tofauti kabisa
Kumbuka kuwa, kuandika na kuongea lugha ya Kiswahili kwa ufasaha utatakiwa ubobee kwanye hii lugha, wengi wetu tunaandika Kiswahili cha kuongea au cha mazoea.
Lugha za makabila nazo zinachangia sana watu kukosea katika uandishi wa herufu, kuchanganya lugha ya Kingereza katikati ya Kiswahili nao ni uchafuzi mkubwa wa lugha.
Upuuziaji au kutokuwa makini kumeshamiri siku hizi. Sijui upotofu uko wapi, mashuleni au mitaani.Mara nyingi nisomapo makala ndefu za Kiswahili sikosi kukutana na angalau neno moja la Kiswahili linaloonekana kuwa jipya kwangu. At the same time, the same article may contain a few familiar words that do not appear to conform to the standard Swahili that I learned during my early school years. Mengi ya maneno yanayoathirika ni yale yenye herufi "h", "dh", "l" na "r" ndani yake.
Watu wanaandika, mfano,
aya wakimaanisha haya,
ivi wakimaanisha hivi,
ivyo wakimaanisha hivyo,
erufi wakimaanisha herufi,
uzuni wakimaanisha huzuni,
nazani wakimaanisha nadhani,
zuluma wakimaanisha dhuluma,
karenda wakimaanisha kalenda, n.k.
Sasa ninapoona vitu kama hivi, ninapata kigugumizi kuamini kwamba yale maneno yanayoonekana kama mapya kwangu kweli ni maneno mapya na sahihi ya Kiswahili.
What's going on? Sarufi ya Kiswahili siku hizi haifundishwi tena kwenye shule zetu au mimi nimeganda kwenye karne ya ishirini?