Kiswahili kigumu

SuperImpressor

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
1,504
646
Kuna jamaa mmoja alikuwaga anakera sana watu kwa kutaka kila anachokisema watu wakubaliane naye basi siku moja hao watu kati yao alikuwepo mgeni na baadaye yule mtu naye akaonekana akija, wale watu wakaanza kuulizana kwamba ni nani anaweza kutusaidia kumbishia huyu jamaa leo mbona huwa anatukera sana? Basi akajitokeza yule mgeni, mimi hapa, wale watu wakasema safi mkuu sasa we akiwa anasema kila neno utakuwa unabisha. Basi yule jamaa wa kukera alipoanza mazungumzo ikawa hivi
Jamaa: Haijawahi tokea mechi kama ya jana hapa duniani.
Mgeni: Hodiii
Jamaa: Au mliionaje ile mechi washikaji.
Mgeni: Hodiii
Jamaa: Leo hatuko pamoja wakuu
Mgeni: Hodiii
Jamaa: Ndugu vipi! wewe naye wamekuchunia? manake nasikia unabisha lakini hujibiwi.
Mgeni: Hodi bhanaa, usiwe unababaisha watu hapa.
Watu: Hahahahahahaha hii nayo kali
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom