Kiswahili cha Tanga na swaga zake

Freddy81

Member
Feb 3, 2009
99
3
Haya ni baadhi tu ya maneno ya kiswahili ambayo ukiwa tanga utayasikia tofauti kidogo
1. Nakuja - Naja
2. Unaenda- waenda
3. unanichokoza- Wanchokoza
4. unataka - Wataka
5. Mama mdogo - Odo
6. Mama mkubwa - Mkuu
Hayo ni baadhi tu, bado hiyo lafudhi yao yani utapenda kuwasikiliza.. Lkn je ni kiswahili fasaha?
 
Humu ndani mara kadhaa huwa tunaitana "mkuu"....kumbe kwa wanaume wa kitanga inawezekana huwa wanakwazika!
 
7. Ninakula = Nala
8. Kuona haya = kutahayari

In nutshell hicho ni kidigo....tuletee lafudhi ya kisambaa Freddy81, ni kasheshe
 
Last edited by a moderator:
mkaza mjomba......mkuu (mama mkubwa) daaah mbavu zangu jamani :bounce::laugh:
 
Back
Top Bottom