Kisutu: Yericko Nyerere ahukumiwa jela miaka mitatu au faini ya Mil 5 kwa uchochezi, alipa faini na kuachiwa huru

MAGALEMWA

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
6,281
2,000
View attachment 1732458
Leo ni siku ngumu katika historia ya demokrasia yetu. Rafiki yetu, ndugu yetu na mpambanaji mwenzetu Yericko Nyerere amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela au faini ya milioni tano katika kesi ya Uchochezi No 188/2017 ambayo inahusu maneno yake kufuatia maazimio ya Baraza Kuu la Chadema 2017 kudai Katiba Mpya, Tume huru ya uchaguzi na Uhuru wa maoni.

Hii ni kesi ya 4 ya uchochezi kwa Yericko kwa kipindi cha miaka mitano. Kesi ya kwanza (2016) aliishinda Jamhuri, kesi ya pili (2018) akashinda tena, kesi ya tatu (2019) akaibagaza Jamhuri. Lakini kesi hii ya 4 amepatikana na hatia.

Njia ya demokrasia haijawahi kuwa rahisi. Kwa miaka mitano Yericko amekuwa mtu wa kushinda mahakamani kila siku kwa kesi za uchochezi. Leo ametiwa hatiani kwa kudai Katiba mpya, Tume hutu ya uchaguzi na Uhuru wa maoni.

Pamoja na kazi nzuri iliyofanywa na mawakili wa chama akiwemo Wakili msomi Hekima Mwasipu, iliyomuwezesha kushinda kesi zote 3 za awali, kwenye kesi hii ya leo naomba tumlipie Yericko faini anayotakiwa kulipa, wakati taratibu za kukata rufaa zikiendelea.

Kukubali Yericko afungwe ni kukubali kutupilia mbali madai ya Katiba mpya, Tume huru ya uchaguzi na uhuru wa maoni. Hatuwezi kukubali hilo litokee.

Yericko anahitaji TZS 5M kabla ya saa 9 mchana wa leo, otherwise atapalekwa Segerea. Naomba tuoneshe dola maana ya nguvu ya umma. Sasa hivi ni saa 8 mchana. Tufanye challenge ya "one hour" tu kutafuta 5M.

Michango yote itumwe kwa M/Kiti Bavicha taifa John Pambalu kwa:
M- Pesa 0769 823839
Tigo-Pesa 0676 250710

UMOJA WETU, NGUVU YETU
Wana CHADEMA wameshamsitiri mil 5 imeshachangwa, imelipwa na yuko huru. One love.
 

magu2016

JF-Expert Member
Oct 8, 2017
5,833
2,000
Hongereni sana kwa kuwa na chama dume kwa kulazimisha .

Cdm ni chama cha hiari hivyo kila kinachofanyika ndani ya chama ni kwa hiari.

Hata hiyo michango imetoka kwa moyo mmoja kwa kila mtu kutoa angalau sh 100.
Endelea kudanganywa!
 

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
27,374
2,000
Taarifa kutoka Mahakama ya Hakimu Mkaazi Kisutu inasema kwamba Kada wa Chadema, Mkulima wa bamia, mfanyabiashara na Mtunzi mahiri wa vitabu vya ujasusi, Yerricko Nyerere ambaye ni mkazi wa Kigamboni, leo amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu Jela ama kulipa faini ya Shilingi milioni 5 za Kitanzania kwa kosa la uchochezi.

Mungu mbariki Yerricko, Mungu ibariki Chadema.

====

Yericko Nyerere AHUKUMIWA KWENDA JELA.

Leo 23/03/2021mahakama ya hakimu mkazi kisutu, imemuhukumu, Yericko Nyerere kifungo cha miaka mitatu jela au faini ya shilingi milioni tano (Tsh.5,000,000/=) katika kesi ya Uchochezi No 188/2017 ambayo ilihusu maneno yake kufuatia maazimio ya Baraza Kuu Chadema 2017 kuhusu UKUTA, Katiba Mpya na Tume huru ya uchaguzi.

Muda huu Yericko Nyerere anapelekwa Gerezani Kama mfungwa.

======

UPDATES: 1630HRS

======

Yericko Nyerere ameachiwa huru baada ya kufanikiwa kupata Milioni 5 ya faini. Wanachadema wamefanikiwa kuchanga kiasi hicho cha hela ndani ya saa moja.


Yeriko alikabiliwa na kesi ya kuchapisha maneno yenye nia ya uchochezi kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook iliyoko katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.

Hayo yalibainishwa na Wakili wa Serikali, Clara Charwe, wakati akimsomea Yericko maelezo ya awali mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, Respicius Mwijage.

Katika maelezo hayo, Yericko alikubali maelezo yake binafsi ambayo ni jina lake, yeye ni mfanyabiashara na kwamba alishtakiwa.

Yericko anadaiwa kuwa Mei 28, 2017 kwa nia ya kuwachochea Watanzania, alichapisha maneno kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook yasemayo:

“Maazimio ya Baraza Kuu yalikuwa (1) Katiba Mpya (2) Tume Huru (3) Bunge (4) Haki ya Kikatiba ya kuishi (Ben Saanane) (5) Haki ya Kikatiba ya kukutana na kuzungumza (Mikutano ya Hadhara ya Kisiasa) Hayo ndio yatahubiriwa katika Operesheni Ukuta.

“Baraza Kuu limeridhia kwa kauli moja kwamba vita rasmi ya kulikomboa taifa imezinduliwa na kama wewe Mtanzania unaogopa kulitetea taifa hili, ni bora ukakaa kando, nenda huko CCM ambako michemsho na supu vipo kwa wingi… kufa kwetu ni ukombozi wa Tanzania…

“Yaani sasa tunarejesha siasa za jino kwa jino, uso kwa uso, mguu kwa mguu, weka mguu niweke ugoko… Ni mwisho kuishi kinyonge, ni mwisho kulalamika, ni mwisho watu wetu kutekwa au kuuawa, ni mwisho watu wetu kuzuiwa kufanya mikutano ya hadhara… Tunasema sasa ni single touch double manifestational.” Mwisho wa kunukuu.


Pia soma: DAR: Yericko Nyerere akamatwa akiwa nyumbani kwake. Wachukua simu na laptop
Tatizo huwezi kupata hkumu tukaona reasoning ya Hakimu. Erythrocyte jitahidini mtuwekee hukumu hapa tusome reasoning
 

G.25

JF-Expert Member
Jun 12, 2013
1,407
2,000
Waislamu awapendi dhuluma mama atawatoa wote Waliobambikwa na Utawala dhalimu.
Ni wakati sasa wakuzifuta sheria zote za kichochezi pamoja na kuwakamata wote walioitwa (wasiojulikana) na kuwafikisha mahakamani.

Haiwezekani kuwa wazalendo huku tukishudia wengine wakionewa, kutekwa, kuumizwa, na hata kuuawa bila hatua kuchukuliwa.

Ni uzalendo wa aina gani huu!?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom