KISUTU: Tundu Lissu afikishwa Mahakamani, apata dhamana

Inasikitika kuona kuwa muhimili muhimu km judiciary wanataka kuutumia kwa manufaa yao....only in Tanzania
 
Hivi Huyo hakimu anayemng'ang'ania Lema anajisikiaje baada ya Lissu kupata dhamana?Wakiambiwa vilaza wanafuuura!
 
16665077_1283660068393678_4559885504951371469_o.jpg

16665091_1283660295060322_2356092932658264850_o.jpg

16707419_1283660261726992_7906957101702823260_o.jpg
Katika lugha asili ya magu jamaa anayerekebisha kofia kichwani husemwa "wibung'waga" _yaani linaona aibuuu!
 
Lisu hawatamueza jamani ni namba nyingine nimesikia baadhi ya mashitaka yake anasema Tanganyika inaikalia zanzibara kijeshi kimsingi hatuna nchi ya Tanganyika kwa sasa mawakili wa mtukufu watapata tabu sana kuitetea hiyo kesi
Labda wakipewa world Map wanaweza kutuonesha hio nchi ya Tanganyika.
 
Ikiwa upande mmoja uahitaji kuombewa ili uweze kuwashughulikia walio kinyume chao na ikiwa upande unaoshughulikiwa unaomba Mungu huyohuyo ili usiendelee kuteseka basi maombi yote yatachekechwa kwani Mumngu ni wa haki na upande unaostahili ndio utaopewa haki!
 
"Statements that are likely to.........." Nikiwa hakimu au judge nauliza-the statements were made more than 30 days ago, have they.......... or indications are there that the statements are about to make....." Yaani kama ni uchochezi watuambie nani hadi sasa amechochewa hadi kuonyesha dalili za kutaka kufanya au kuwa amefanya hicho serikali inasema. Hapo kesi itakuwa imelala
 
Waheshimiwa asalam alaykum...leo tar 9/ 2 nimebahatika kuhudhuria mahakamani kwa ajili ya kesi ya vijana wetu 22 kutoka zanz imepangwa kutajwa tena tar 13 March, nikiwa mahakamani nikamuona Mhe Lisu akiletwa ikabidi niingie kusikiliza kesi yake...

Mhe Lisu ameshitakia kwa makosa 4 yote yanahusiana na hotuba yake aliyoitoa katika mkutano wa Kampeni katika Jimbo la Dimani..

.1) kosa la kwanza nikusema kwamba Zanz ni koloni la Tanganyika..

.2) Wazanzibar wanachaguliwa Rais kutoka Tanganyika mf Jumbe alitolewa Dodoma na Mwinyi akapewa Urais siku hiyo hiyo Dom,

3)Zanz inatawaliwa kijeshi na Tanganyika tangu tar 12 mwaka 1964...

4) Shein ni kibaraka tu hana lolote wakitaka kumuondoa wanaweza kumuondoa kama alivyoondolewa Jumbe.

Mhe Lisu alipoulizwa akasema ni kweli nimesema mbona Tume ya Warioba wamesema kwamba Tanganyika imevaa koti la Muungano bse Tanganyika ndio inajifanya TZ, pia akasema ni kweli majeshi tangu yalipoenda Zanz 1964 ni lini yametangaza kurudi Tanganyika?

Hatimaye waliweka pingamizi kwa dhamana but Mawakili walifanya kazi nzuri hatimaye amepata dhamana hadi 6/3 kesi itatajwa tena walijipanga kumkamata but ameondolewa mahakamani kikomando.....

_________________________
Kulthum Mchuchuli (MHBS)

Kutoka kundi la Ulimwengu wa Kiislam
 
Nchii hii tutafika tu wanakotaka wao. Haya matabaka ya wananchi na wenyenchi lazima yapingwe na kila mpenda amani wa nchi yetu pendwa.
 
Utawala unakuwa tu wa kibabe pale mbunge wa upinzani akikamatwa na kupelekwa mahakamani..?
Unafurahi wabunge wa upinzani wakikamatwa na kuwekwa ndani??
Unadhani hawana hadhi ya ubunge??
Huo ni uvunjifu wa katiba na kudharirisha upinzani!!
Tunahitaji katiba mpya Rais awe ukomo wa maamuzi. Kama USA alivyofanyiwa Trump!!
 
Si mchezo, yaani ni mmoja tu,pamoja na viziavizia yate lakini bado kapigisha kwata mtu nne!!!!
Ah,nakubaliana kabisa na yule anayesema,'kuwa wakili wa serikali lazima uwe kilaza'.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom