KISUTU: Kesi namba 458(Jamhuri v JamiiForums), Jamhuri yakosa shahidi! Kesi yaahirishwa hadi Mei 10, 2018

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,984
Kesi namba 458 ya Jamhuri vs Maxence Melo na mwenzake Micke William inayohusu kuendesha mtandao (JamiiForums.com) bila kutumia Kikoa cha .TZ imeendelea leo Mei 03, 2018 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu.

Mara ya mwisho kusikilizwa kesi hii, mnamo Aprili 05, 2018 Hakimu Huruma Shahidi aliyechukua nafasi ya Hakimu Victoria Nongwa alisema leo kesi hii itaendelea palepale ilipoiacha Hakimu Nongwa

Hata hivyo kesi hii imeahirishwa mpaka Mei 10 kutoka na upande wa Jamhuri kumuomba Hakimu kufanya hivyo baada ya kukosa shahidi.

Hakimu Shahidi amesisitiza kuwa siku hiyo ya Mei 10 upande wa Jamhuri uhakikishe una shahidi

Hivyo basi, kesi hii imeahirishwa mpaka Mei 10, 2018

Kujua kesi hii ilipotokea, fuatilia hapa; KISUTU, DAR: Kesi namba 458(Jamhuri v JamiiForums) imeendelea tena leo, Jamhuri yakosa tena shahidi! Kutajwa tena Mei 03
 
Huwez jua labda huyo jamhuri ame loose interest na shauri
Ni mara ya ngapi wameomba ku airisha
 
Back
Top Bottom