KISUTU: Kesi namba 457 (Jamhuri Vs JamiiForums) imeahirishwa hadi Machi 13! Ni ile ya Kampuni za Cusna na Ocean Link...

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
KISUTU: Kesi namba 457 (Jamhuri vs Maxence Melo na mwenzake Micke William) kuhusiana na tuhuma zilizowekwa katika mtandao wa JamiiForums juu ya Kampuni za Cusna Investment na Ocean Link kukwepa kodi na kunyanyasa wafanyakazi wazalendo imeendelea leo tena Mahakamani hapa.

Kesi hii imeahirishwa hadi tarehe 13 mwezi Machi mwaka huu baada ya kukosekana kwa shahidi kwa upande wa Jamhuri.

Hakimu anayeendesha kesi hiyo, Godfrey Mwambapa amesema hili ni ahirisho la mwisho kabisa katika kesi hii.

Kwa mantiki hiyo, kesi zote TATU (Kesi namba 456, 457, 458) zitasikilizwa siku hiyo ya tarehe 13 mwezi Machi, 2018.

Mahakimu wote waliitahadharisha Jamhuri kuwa hakutakuwa na ahirisho jingine katika kesi hizo tatu.

Kujua ilipotokea kesi hii, soma: KISUTU, DAR: Kesi namba 457 (Jamhuri v JamiiForums) yaahirishwa kwa kukosekana shahidi wa Jamhuri

Pia soma; Muendelezo wa Kinachojiri Kisutu: Kesi za Jamhuri dhidi ya JamiiForums
 
Mkuu Roving Journalist, asanate sana kwa taarifa. Tunafuatilia kwa ukaribu mno kesi hii. Tupo pamoja na washtakiwa wote kwakuwa ndiyo waanzilishi wa mtandao wetu huu unaotufanya tujidai bila kuvunja sheria. Wakuu Maxence Melo na Mike Mushi tupo pamoja nanyi.

Tupo pamoja sana Mkuu, tutazifuatilia mpaka mwisho wake. Ila hizi kesi za JamiiForums huwa zinapigwa sana kalenda kwa kukosa shahidi upande wa Jamhuri.
 
Back
Top Bottom