Kisutu Girls Secondary School ::: Clearance Forms ::: A problem or procedure?

Baba_Enock

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
7,076
2,443
Wadau:

Sijui kama na shule nyingine kuna tatizo kama hili:-

Binti yangu amemaliza kidato cha nne "Kisutu Girls" mwezi huu na Graduation ilikuwa tarehe 26 Oct 2010. Kama ilivyo kawaida wamepewa "clearance forms" kwa ajili ya kuhakiki kama kuna kitu mtoto anadaiwa na shule au ana tatizo lolote of a sort. Sina shida na hizo forms

Tatizo langu ni kuwa kila siku binti yangu amekuwa akienda shule kutafuta waalimu husika ku-sign hiyo form na kibaya zaidi kuna siku anarudi bila kumpata hata mwalimu mmoja ku-sign hiyo form.

Hii inamchosa my dear daughter na mimi inanigharimu maana anapanda mabasi mawili hadi kufika posta!

Kama walimu wa Kisutu mpo hapa jamvini naomba muwe waungwana! Mtoto anahitaji kupumzika na kjipanga kwa ajili ya masomo yake ya baadaye!
 
Pia kuwa nae makini au fanya uchunguzi wako kufika shuleni...!!! anaweza kuwa mkweli lkn pia unaweza staajabu...!!!
 
Hivi huu utaratibu haujafanyiwa amarekebisha hadi leo.

Kwanini Initially wanafunzi kitokana na masomo au madarasa yao wasikusanye fomu kwa pampja. zao na fomu zisungushwe kwa walimu/ dept husika. Kisha walimuu kazi yao iwe ni kusisign kwaomu mkupuo fomu za wanafunzi wasiokuwa na matatizo.

Mwalimuau mkuu wa idara ya eg history anapelekewa fomu 40 wa darasa la "H2" may be siku ya j3. Anazipa baraka kwa wale asiokuwa na tatizo nao wenye tatizo anaacha gap. Siku ya j3 inakuwa ni zamu ya librarian ,etc.

Kwa kipindi hicho fomu zinazunguka kwa wahusika sio lazima wanafunzi waedde shule.

Hivi hata hawa walimu wenzetu wa kizazi kipya wanakosa ubunifu wa kurahisiha mambo???!!!. Walimu wakuu nao wanshindwa aku enforce sera hii na ratiba maalum kwa walimu wa shule zao ????!!!! Mpaka liadikwe dokezo kutoka wizarani.

Ushauri wangu kwa muwasilisha mada tuwe sehemu ya mabadiliko. Piga simu shuleni kisutu ongea na mwalimu mkuu mpe ushauri huo. Sio lazima utajee jina la mwanao kutoa usumbufu. Am sure itasaidia hata wa mwaka ujao. ikiwezekana nipe na mm number yao niweke msisitizo with two people compaling something positive can be done.
 
Back
Top Bottom