Mkuu hayo yanayoendelea ni ya kuwataki kheri
Kuna kitu kimoja kimetia doa sana suala zima na ndiyo maana nikasema hiyo ni ''missed opportunity''. Uchaguzi mzima umegubikwa na mambo yasiyo na majibu kwa wanaofuatilia
SUMAYE;
Niweke wazi kwamba ameshindwa uchaguzi katika sanduku la kura.
Hata hivyo kushindwa kwake kuna acha maswali mengi sana kwa kuangalia historia ya CDM
Imesemwa mara nyingi ukitaka kukutana na mkono wa chuma, zungumzia uenyekiti
Hayo yaionekana kama maneno na uzushi, lakini kwa hali ilivyo kuna sababu za kujiuliza.
Sumaye alijiunga na CDM kama akina Lowassa. Tofauti na wenzake yeye alianza siasa za chama ngazi za mitaani. CCM walimtania kuwa alicheza ''ligi za mchangani''
Hii ni baada ya kuwa mwenyekiti wa kanda ya Pwani.
Katika kipindi chote hatuskusikia malalamiko kuhusu uongozi wake katika kanda hiyo.
Sumaye akachukua fomu za kuwania uenyekiti wa kanda.
Alikuwa mgombea peke, na bila shaka wanachama wengine waliona ni maji marefu.
Hakuna aliyejitokeza kupambana naye
Katika kura Sumaye akashindwa na kivuli.
Yaani akashindwa kuchaguliwa licha ya kuwa m/kiti wa kanda na mgombea pekee.
Halikutokea kwa bahati mbaya, kulikuwa na sababu na mikono ya watu nyuma yake
Hilo ni baada ya kuchukua fomu za Uenyekiti wa Taifa.
Kwa dhalili aliyokumbana nayo, akajitoa katika chama. Ukimsikiliza Prof Safari kwa umakini kuna kitu kinachozungumziwa.
Ule ushindani uliotarajiwa na ambao ungekijenga chama chao, kukifanya kiwe tofauti umekufa.
Swali la kujiuliza, kampeni ya kumwangusha Sumaye imefanywa na nani na kwa lengo gani?
Narudia tena hilo halikutokea kwa bahati, ilikuwa ni ''calculated move''
Pili, Mwenyekiti Mbowe akiwa na miaka takribani 15 hakuwa na sababu za kuanza kampeni kwa kutumia kundi la ''mwaba tuvushe''. Alitakiwa achukue fomu kawaida ili kuleta uwanja sawa
Haya ni maoni yangu, lakini nasimama nayo kwa kusema ''kuna kitu hakipo sawa''
Pascal Mayalla