Kishindo cha Rais Magufuli bomba la mafuta Tanzania - Uganda

Sep 8, 2020
67
133
Katika hatua za maandalizi ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 Ibara ya 63 - Mafuta na Gesi Asilia (e) “Kuendeleza Utekelezaji wa miradi ya kielelezo na kimkakati ambayo ipo katika hatua za mwisho za makubaliano ikiwemo mradi wa Bomba la kusafirisha Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) na mradi wa Kusindika Gesi asilia (LNG) Mkoani Lindi ambayo itaongeza ajira kwa watanzania na mapato kwa nchi”.

Pamoja na Ibara ya 63- Mafuta na gesi Asilia(g) “Kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya ushirikiano na nchi jirani ikiwemo miradi ya kusafirisha mafuta na gesi asilia ili kuongeza ajira, mapato na usalama wa upatikanaji wa mafuta na gesi nchini ili kuimarisha ushirikiano nan chi jirani”

Tanzania leo imeshuhudia tukio la uwekaji saini wa Hati ya Tanzania na Uganda inayoitwa 'Host Agreement' wa ujenzi wa Bomba la Mafuta la Kusafirisha Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki 'The East African Crudial Oil Pipeline’ (EACOP) litakalojengwa kutoka Ohima Uganda hadi Tanga lenye jumla ya Km 1,445. Mradi mkubwa utagharimu takribani Dola za Marekani Bilioni 3.5 sawa na Shilingi Trilioni 7.8 hadi 8 za Tanzania.

Itakumbukwa kuwa tarehe 26 Mei, 2017 nchi za Uganda na Tanzania zilisaini mradi wa ushirikiano 'Intergovernmental Agreement' wa mradi huu. Aidha tarehe 5 Agust, 2017 Rais magufuli na Rais Museveni waliweka jiwe la msingi huko Chongoleani Mkoani Tanga - Tanzania na 9 Novemba, 2017 waliweka jiwe la msingi huko Luzinga upande wa Uganda.

Bomba litakalojengwa litakuwa na urefu wa km 1,445 na hivyo kulifanya liwe refu zaidi kwa mabomba yanayotumia Teknolojia ya Kupasha Joto Duniani (The longest Heated Pipline in the World) na sehemu kubwa ya Bomba hili takribani KM 1,115 zitakuwa upande wa Tanzania na KM 330 zitakuwa upande wa Uganda.

Akihutubia baada ya tukio la utiaji saini, Mhe Rais Magufuli amesema Kwa upande wa Tanzania mradi huu utapita kwenye mikoa Minane, Wilaya 24, Kata 132 na vijiji Zaidi ya 186. Mikoa hiyo ni pamoja na Kagera, Geita, shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara, na Tanga.

Kwa tathmini iliyopo inakadiriwa kwenye eneo la upande wa Tanzania watalipwa fidia watu zaidi ya elfu 90 watakaoguswa mashamba yao na fidia zitakazolipwa zinakadiriwa kuwa ni bilioni 21. Vilevile patajengwa vituo 14 na watu watakaoguswa na kile kituo kwenye maeneo hayo watalipwa zaidi ya bilioni 9.9.

Katika Mradi huu, Tanzania itachukua asilimia 60 ya faida itakayopatikana na asilimia 40 itabaki kwa waganda.

Mradi huu utaufungua kiuchumi Ushorobo wa kaskazini (Northen Corridol) wa kanda ya Afrika Mashariki wenye kujumisha nchi za Burundi, Kenya, Ruanda, Sudan Kusini n ahata DRC kwa kutengeneza taswira chanya ya uwekezaji kwa kanda yetu ya Afrika mashariki.

Kwa muda mrefu Bara la Afrika limekuwa muhanga wa taarifa hasi duniani ikiwemo vita, njaa na magonjwa, hali ambayo imekuwa ikiwafanya baadhi ya wawekezaji kusita kuja kuwekeza kwenye Bara la Afrika. Hivyo Mradi huu umetoa taswira iliyo tofauti na utasaidia kuondoa taswira hiyo mbaya na utawavutia wawekezaji wengi kuja kuwekeza kwenye Bara la Afrika hususani kwenye Ukanda wa wa Afrika Mashariki.

Mradi huu pia utakuza ushirikiano miongoni mwa nchi za Kanda zetu katika shughuli za utafutaji mafuta kama ambavyo Mkataba ulioanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki unavyoelekeza katika Ibara ya 101 unahimiza nchi wananchama wa Afrika Mashariki kushirikia na kuendeleza rasilimali ya Mafuta na Gesi.

Mradi huu unatarajiwa kutengeneza takribani ajira Permanet zaidi ya 10,000 hadi 15,000 na kuchochea shughuli mbalimba za kiuchumi kama vile mama Lishe na huduma za hoteli.

Hata hivyo Tanzania na Uganda inaendelea kufanya utafiti wa mafuta kwenye mabonde ya Mto Eyasi na Wembele endapo mafuta yakipatikana itakuwa rahisi kuunganisha kwenye bomba hili.

Kadhalika waganda wakihitaji gesi itapitishwa sambamba na bomba hili la mafuta ikaanze kutumika kwenye viwanda vya kule Uganda na kuleta faida kwa waganda na watanzania.

Watanzania tumeamua tarehe 28, Oktoba, 2020 tutachagua CCM, tutachagua Maendeleo na tutamchagua Rais Dkt John Pombe John Magufuli.
IMG_20200913_145959.jpeg
 
Huu ndio ukuzaji wa uchumi tunaoulilia watanzania, sio yule anaelilia haki ya kuongea na akiipata anaishia kitukana #MATUSI@tundu!
 
Kule Tanga nadhani ilikuwa ni kuwapatanisha Ruge na Makonda. Leo ndio tumesaini mkataba rasmi
 
Lisu atakwambia hilo bomba halima msaada wowote kwa mwanachi wake wa kule Ikungi Singida
 
Huu ndio ukuzaji wa uchumi tunaoulilia watanzania, sio yule anaelilia haki ya kuongea na akiipata anaishia kitukana #MATUSI@tundu!

Unajitoa ufaham kabisaaa kwasababu ya buku7? Umeona wapi mradi unasainiwa mara mbilimbili Tanga 2016 na Leo tena? Mmesha yakoroga tulieni mtayanywa mtamuomba mpaka Trump aje kuwasaidia campaign. TL kawashika pabaya wasanii watakula sana hela za chama Mwaka huu
 
Ameamua kumwomba Museveni ampige chapuo kwenye kampeni, kweli Lissu hatari.
 
hakuna mradi hapo.wote wanaongopea wapiga kura wao

Huu ni Usanii tu wa Magufuli na hakuna lolote palr do!!
Inakuwaje Jiwe la msingi liliwekwa tangu 2017 ATI Leo anatumia Kama gia ya kuombea KULA.....TU......!!!
THIS TIME HATUDANGANYIKI NG'O.. !!!!’
 
Back
Top Bottom