Kishika uchumba kimerudishwa

We nae miyeyusho ukishaona Kuna vikwazo vingi kumchukua binti rejea kwenye katiba ya jamhuri ya mabachela ibara 19 kifungu kidogo 2(a)piga mimba, ikifika miezi sita Anza taratibu za uchumba haraka sana, ikiwezekana zuga uonekane mimba si yako bali lengo lako ni kumuoa na mimba si kikwazo
 
Hivi kishika uchumba cha laki 5 ndio ile pesa wanasemaga inatiwa ndani ya barua ili ombi lako lisikilizwe na upande wa kikeni?
 

Mrejesho wa Thread hapo juu

Baada ya vuta ni kuvute kati ya familia ya kijana na binti kuhusu mahari.

Wanafamilia wa kijana wengi walionyesha kuchukizwa na tabia ya familia ya binti, baadhi ya wanafamilia wakiapa kuwa kama kijana akiendelea na mipango ya kumuoa huyo binti, wao hawatashiriki kabisa katika jambo hilo.

Kutokana na hali hiyo ya kutofikia muafaka kijana akakubali bora yaishe, Mshenga akatuma barua kwa familia ya binti kuwa kwa mahari hiyo ya milioni 5 bila kupungua , wao wameshindwa.

Baada ya wiki familia ya binti ikarudisha barau ya posa juu imeandikwa na wino mwekundu, IMEKATALIWA pamoja na shilingi laki tano za kishika uchumba.

Baada ya hayo ndugu wa kijana wengi wameonyesha kufurahishwa na muafaka huo.

Kijana amekubali matokeo kuwa haikuwa ridhiki yake.

Binti yeye ameonyesha kukubali kishingo upande kwani hii ni posa ya pili imekataliwa nyumbani kwao dhidi yake.

Binti ajitafakari hapo anamatatizo uyo n an familia yake asije badaee akaenda kushinda kwa Mwamposa tu
 
Hivi,mahali yote hiyo,ni bikra? Hivi,hao wazazi wanajua tunawaondolea tu mizigo ma kwao na kujionyesha! Wana habari watoto wao wameolewa na kuachika kisirisiri zaidi ya mara mia? Na hapo wakichukuliwa wanaendela kuolewa na watu wengine!? Sasa basi,bora kila aliegegeda nae achangie,maana najua watarudiana tu kisirisiri
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom