Kisha Kuhani Mkuu akamtetea Bashite akisema...

Ikawa baada Ya kufa kwake bashite wana wa dar es salaam wakamuuliza mungu wa inchi yao wakisema ni nani atayekwea Kwanza kwa ajili yetu juu ya walanguzi wa dawa za kulevya ili kupigana nao? - 1 Bashite 2:6
 
"Enyi wana wa nchi ya makinikia,sitamuondoa mkuu wa mji wa bandari salama hata kama haijui 'a',yeye ni mmoja wao wachapakazi na wengine waige mfano wake.Baada ya kusema hayo Bashite akatabasamu na kujipiga piga kifuani akisema;na uhimidiwe kuhani mkuu,kwa maana itaandikwa ukae miaka 7 au zaidi ikikupendeza."
[waraka wa Polepole kwa wanalumumba 2:2-9]
Bulai nghukogoha nisani injelu
 
Hata kuhani Mkuu alipomfanya mwanawe awe na maamuzi ya juu ya Nchi ya Makinikia, Na jina la mwanawe mzaliwa wa kwanza aliitwa Daudi na jina Pili aliitwa Bashite, walikuwa na maamuzi katika wadanganyika(Watumishi Hewa 23:12)
 
Na akawapa vipande vya shekeli akisema eenendeni mkawanunue wote kule sinoni mpaka daraja mbili , huku akiwaambia hakuna hata mmoja wao atakayewasumbua sababu nipo kwa ajili yenu!
Teh teh teh umetisha mkuu.
 
Siasa walizokuwa wanataka mwigamba na kitila zifanyike ACT za kijinga mno , eti za kuishambulia chadema
 
Nikamuona mfalme amekaa kwenye kiti chake cha enzi naye amejifika kwa mavazi ya fedha, aliyeshika mkononi kitu kama mti mkavu wenye moto wa kufisha.

Akauvunjavunja mti ule vikatokea vijiti viiiingi vyenye uwezo sawa na tabia za kufanana.

Vijiti vile akavigawa kwa kundi kubwa la watu wasioonekana, wote wakawa tayari kuvitumia pindi amri ikitolewa!

Vijiti vile vina miisho minne, ambayo hutoa moto uuao wote wamwaduo MUNGU.

Nikaona moto na kusikia kishindo kishindo kama cha mtu anakohoa mfululizo, mtu mmoja asiyeonekana aliyepewa kijiti kimoja aliamriwa kukitumi!

Alipigwa Mtumishi wa Mungu Ponda bali mauti haikupewa mamlaka juu yake.

Hapo awali Kijiti kilitumika kwa majaribio kikamuua yule askari shupavu Kombe!

Nikakiona kijiti maeneo ya dodoma kikiwa tayari kutumika, nao waliokibeba nikawatambua, mimi tu ili kukujuza wasioonekana hao!

Wakaifyatua mitego ya mioto ile kunielekea, lengo kuu ni kunipeleka kuzimu.
MUNGU akasimama kumkemea shetani pamoja na mfalme!

MALAIKA AKAPAAZA SAUTI KUU AKISEMA OMBENI MSIJE MKAINGIA MAJARIBUNI

Maana tazama wametumwa akina Wakudadavuwa, simiyu, kipara kipya, Barbarosa na Lemutuz ili kumfariji mfalme kwa kujikakamua kuficha uovu unaomchukiza MUNGU upeo.

====UFUNUO UNAENDELEA====
Mkuu umetisha mbaya
 
mkikaa sawa.. tunaweza toa dini apa miaka 3027 uko.. mko vizuri wakuu! nimecheka sana..
 
Wana wa makinikia wakamililia Mungu juu ya mateso waliyopewa na mfalme wao, ndipo neno la BWANA nikamjia antipas, liwali wa mji wa ukanda wa kati katika nchi ya wamakanikia , kwamba aende akahubiri habari za dhuluma, rushwa, uhuru na haki za watu kufanya makutano,.
 
ndipo mtukufu akauliza nimtume nani dar es salaam akaokoe wana kondoo wangu wanao angamia kwa madawa,
ndipo mwanawe mpendwa akasema nitume mimi baba,
ndipo mwana wa mtukufu akashuka kutoka kwenye kiti cha enzi na kuja dar,

Na baada ya kushindwa kuokoa wanakondoo wa mtukufu akasikika akisema "BABA IKIKUPENDEZA NA KIKOMBE HIKI KINIEPUKE"

ndipo mtukufu akamtoa mwanawe mpendwa katikati ya wagalatia na kumpa mtu mwingine aubebe ule msalaba
waraka wa MANJIno 3:20-28
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom