Kisasi: Mke wa Boss ndani ya 18 zangu

Baba jayaron

JF-Expert Member
Jun 29, 2015
4,277
5,838
Pongezi za kuugawa na kuanza ngwe nyingine ya mwaka.

Katika msimu huu wa sikukuu tukufu tulipata bahati yakukutana sisi wafanyakazi wa kampuni yetu hii kwa upande wa kanda ya kaskazini.

Tulikutana ma branch manager woote jijini Arusha tukiwa na Zonal manager wetu.

Zonel manager wetu ni kijana tu ambaye tumelingana na sote tulikua ma branch manager sema mwenzangu akawa promoted to Zonal manager.

Chaajabu tangia awe Zonal manager akabadilika vibaya mno akawa hatusalimiani anatufokea kama watoto wadogo mbaya zaidi anatutukana even mbele ya watu tunaowaongoza.

Amenipa hard time saana kazini mpaka nikafikiria niache kazi lakini niliona upumbavu nikiacha kwa ajili yake so nikajitahidi kumchanchia na yeye at least twende sawa, mpaka nimemzoea.

Sasa katika kukutana na kusheherekea sikukuu ya Eid kiofis ndo ilibidi tukutane Arusha, kwa upande wangu sikwenda na mke wangu nikijia huyu tunaenda kukutane nae anaweza nidhalilisha mbele ya mke wangu.

Kufika Arusha managers wenzangu walifika na wake zao akiwa na yeye Zonal, Jamaa alimsifia saana mke wake akidai ni mzuri kabla hajafika.

Hamadiii...huyooo akafika ghafla kutaamaki ni Xgirlfriend wangu kipindi nasoma Advance, mbaya zaidi nilimsaidiaga sana katika matatizo aliyokua nayo hata ya kifamilia financialy.
Tulikuja kupoteana nae baada ya mimi kwenda Uganda kusoma na kurudi pale kwao walihama na mimi nikaanza mishe na wanawake wengine.

Kiukweli tulishikwa na butwaa saana hatukuisha kutazamana hasa yeye akiwa na macho ya machozi flani hivi.
Wakati naenda chooni nae aliinuka baada ya muda akaelekea huko huko kwakua ni sehemu iliyotenganishwa na ukuta kumbe alikua akinisubiri...

Alinikumbatia nakuanza kulia akisema hato nisahau katika maisha yake na bado hakuna aliweza chukua nafasi yake, maneno yake yalinichoma sikuweza kumjibu kitu nikamuacha mpaka tunaondoka kuagana.

Tatizo:
Amepata namba yangu na leo amenipigia simu akidai anamaongezi na mimi nilicho mjibu nina kazi niko bize.
Je akileta mambo yakuridiana nimkubalie ili nimkomeshe huyu Zonal Manager wetu kwa matusi na dharau anazo nilitea?? Au nimpotezee nitafute kisasi kingine???

Karibuni kwa ushauri.
 
Achana na pepo la visasi, usirudi nyuma, huyo X wako hakutakii mema, utajafukuzwa kazi kwa aibu na kuchafua CV yako buree! Wambili havai moja, boss wako ni boss tu kakutangulia! Kumbuka kisasi huzaa kisasi, violence breeds more violence, do away with that evil attitude and move on! Blessed.
 
Mke wa mtu sumu baba tafadhali sana achana naye kabisa.Wala hakuna kisasi hapo bali upumbavu mtupu.
 
kwa mfano sasa utakuwa umemuumiza vipi kama ukimtafuna mana utamwambia kuwa unamgonga mkewe au na ikiwa hivyo si itakuwa ugomvi
siyo poa 7bu wewe mme wa mtu na yeye ni mke wa mtu mkaushie
chakufanya kama unataka umuumize na heshima iwepo
tengeneza mazingira ajue kuwa wewe huyo alikuwa demu wako na ushamkanyaga sana kipindi hicho cha nyuma
hapo heshima itarudi 7bu ukimjua aliyekuwa anamla demu wako kabla lazima saluti ziwepo
 
usitake tenda dhambi kwa kutumia mgongo wa kisasi,mi sion alichokukosea wewe km wewe so hata hata kisasi akiexist hapo sema tu una yakwako.....daah ila ndoa hizi yaan unaoa ex wa mtu wakikutana ndo km hvyo....mi sioi
 
Bwana Branch Manager, naona umeassume kwamba Mr Zonal Manager ni ''mshamba''mno na hawezi kua JF member? Wewe endelea tu kuomba ushauri wa kumtafunia my wife wake. Usikute na yeye yumbo anaomba ushauri mtaani jinsi ya kukufumua marinda yako. Be warned.
 
Back
Top Bottom