Kisarawe: Jimbo maskini kuliko yote Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kisarawe: Jimbo maskini kuliko yote Tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kisarawe 2015, Oct 5, 2011.

 1. K

  Kisarawe 2015 New Member

  #1
  Oct 5, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ki historia, ni wilaya ya kwanza kuanzishwa Tanzania na mkoloni

  Lakini kimaendeleo ni maskini kuliko zote Tanzania na hata wilaya ya Mafia ina afadhali

  Pia msisahau kuwa ni wilaya ambayo jimbo lake limekuwa likiwasilishwa na CCM tokea uhuru...na moja kati ya waliowahi kuwa wabunge wa Kisarawe ni pamoja na Marehem Kigoma Malima (ambaye mwanae Adam ndiye mbunge wa Mkuranga), Athumnani Janguo (aliyewahi kuwa mkurugenzi wa Bandari ) na sasa hivi jimbo hili limeshikiliwa na jamaa anayeitwa SULEIMAN JAFO ambaye ame spend si chini ya milioni 400 ili jina lake lipitishwe kwenye Chama na baadae kushinda kirahisi kwenye ubunge. Sasa hizo pesa zenyewe kumbe alikuwa kaziiba kule alikokuwa anafanya kazi kwenye NGO ya PLAN INTERNATIONAL sasa hivi amekubaliana nao kuwa atazirejesha kidogo kidogo.  Tangua ateuliwe kuwa mbunge hakuna lolote alilolifanya la maana. na tunaweza kusema kuwa kazi kubwa inafanya na NGO ambazo zinachimba visima vya maji na kutoa huduma za afya. Sasa CCM hatujui mmetuletea mbunge dizaini gani kwani hana uadilifu. Kama aliweza kuwaibia hao Plan International ndio atashindwa kutuibia sisi wananchi wa kawaida?  Lakini kama mbunge hajafanya lolote zaidi ya kula posho za milioni 15 kila mwezi kama mbunge huku jimbo lake likiongoza kwa watu walio wasio jua kusoma au kuandika.

  So far alichokifanya ni kutoa ardhi yenye hecta 200,000 kwa shirika la kidini ambalo limesema kuwa ile ardhi ni kwa ajili ya investment ya kujenga nyumba za ibada

  Jamani hicho ndio kilio chetu wana Kisarawe. Na tunaomba msaada wenu wa kimawazo namna ya kufanya ili hali zetu ziwe walau na afadhali.
   
 2. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ayaaaaaaaaaa... Kumbe kashikaji kajizi, aiseeeeeeeee.... Ebwanaeeeeeee....... Sasa mnasubiri nini Kuka- Kolimba. Hii inanikumbusha jinsi Waziri mmoja mwenye dhamana alivyotumia na kujishindia mihela kiasi cha sh. milioni 700,000,000/= kwakujenga matundu manne ya vyoo vya shimo. Halafu bado mpaka leo anadunda tu Wizarani.
   
 3. kikahe

  kikahe JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2011
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Na bado si wanaendekeza U sisiemu? Shauri yao na Mbunge wao
   
 4. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 892
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  kisarawe mtapata maendeleo endapu tu mtakubali damu ya mabadiliko
   
 5. m

  massai JF-Expert Member

  #5
  Oct 5, 2011
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  ukisikia uswhili kule ndio chimbuko lake,brain washed ,kwahiyo akitokea mjanja mmoja akiwajaza ujinga ni mpaka karne hata akitokea wa kuwaambia jamani mnaibiwa wao hawaelewi alafu ukiwachomekea na udini tena ndio unakua umewamaliza kabisa
   
 6. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #6
  Oct 5, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Sasa mheshimiwa unashauri nini juu ya hawa watu
   
 7. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #7
  Oct 5, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  mpaka mtakapoamua kufanya mabadiliko ya akili zenu
   
 8. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #8
  Oct 5, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 22,007
  Trophy Points: 280
  hata kwa Ngeleja hovyo kabisa
   
 9. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #9
  Oct 5, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  upuuzi wenu kama wana igunga unauleta humu,mtakoma ndo kwanza mwaka1 bado4.acheni upumbavu.
   
 10. d

  dicaprio Member

  #10
  Oct 5, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  kwa ccm watakuambia wanajipanga, wana mikakati na pia wataleta maendeleo kwa wananchi kwani iko katika ilani
   
 11. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #11
  Oct 5, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Ni maeneo mengi sana Tz ndivyo yalivyo na si Kisarawe tu!!!!mengi ya maeneo haya masikini sana ni yale yliyoshikiliwa na magamba kwa mda mrefu!!!!muhimu ni kuamua wenyewe kumweka mwana harakati asiyeangalia tumbo lake bali mahitaji na shida za watu wake
   
 12. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #12
  Oct 5, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,549
  Likes Received: 18,220
  Trophy Points: 280
  Kisarawe 2015, kwa vile title yako ni hiyo, inaonyesha wewe ni interested party for 2015, hivyo nakushauri usitake platform ya kupandia kwa kuwabomoa waliopo, wewe kama ni Mwanakisarawe, fanya mambo wananchi watakuona na kukusupport.

  Uvivu, majungu na fitna ni asili ya baadhi ya jamii zetu. Acha kuleta majungu na fitna ili kumdiscerdit mbunge aliyepo. Kwani Malima, Janguo na waliotangulia wamefanya nini?.

  Nyie Kisarawe ina ardhi yenye rutuba ajabu, mnaifanyia nini zaidi ya kukalia uvivu na kuteketeza misitu kwa kuchoma mkaa!. Mlikuwa na kiwanda bora kabisa cha matofali ya kuchoma, Kisarawe Brick Factory mmekifanyia nini zaidi ya kukiuawa kwa uvivu wenu!.

  Ekari zenu 8200, si mmezitoa sadaka bure kwa kampuni ya Sun Biofuels ili kulima Mibono Kaburi, kampuni hiyo inatoa ajira 1500, priority ya kwanza ni kwa wana Kisarawe, mmepewa ajira 400 za kwanza, waliopata ajira hizo wakashindwa kudeliver, sasa hawachukui tena vijana Kisarawe bali wana import nguvu kazi toka mikoa mikoa jirani, msaidiweje nyinyi?. Mnabebwa hambebeki!.

  Tena baadhi ya wadada wa Kisarawe ndio usiseme, nenda pale kitongoji cha Mayai ushuhudie kinachofanyika usiku!, bia moja, chips kuku na buku ya kuamkia asubuhi inatosha kumaliza kila kitu!, cha ajabu hata kinga hawaulizi, usipojitolea kujikinga mwenyewe, kavu kavu kwao poa, hii ni hatari mbele ya safari!.

  Mbunge mpya huyo unategemea afanye mangapi?, afadhali yeye mara 100 kuliko waliomtangulia!.

  Please acha majungu, if there is anything you can do for Kisarawe, please do it, usilete hizo za fulani hakufanya kitu, what can you 'wewe' do for Kisarawe?.
   
 13. M

  MafiaIsland2015 Member

  #13
  Oct 6, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  2015 Pwani hapakaliki
   
 14. The Spit

  The Spit JF-Expert Member

  #14
  Oct 6, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  T
  Kingi ni balaa,nimesoma minaki pale,shule nzima high school haina hata mzaramo mmoja,mpaka Shule ikatoa offer kwamba akipatikana mzaramo yeyote kachaguliwa Minaki inamsomesha bure lakini bado hawakupatikana...Wale watu lazima wabadilike,ni wavivu na wanapenda sana starehe!
   
 15. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #15
  Oct 6, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kisarawe jimbo maskini kuliko zote ndio nini?

  kaka wa Rais anafunga ndoa Ikulu sio raha hiyo?
   
 16. regam

  regam JF-Expert Member

  #16
  Oct 6, 2011
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 268
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Si ssm iliyowachagulia mbunge bali ni ninyi wenyewe. Ukijaribu kuchunguza, majimbo mengi yaliyomaskini, bado yana wabunge wa sisiem.
  Tubadilike jamani kwani nchi inahujumiwa na magamba.
  Wengi wetu tunaogopa mageuzi! Hilo ni tatizo kubwa sana. Tujifunze kwa wenzetu majirani walioamua kuukaribisha upinzani. Hali ya uwajibikaji wa serikali inakuwepo ukilinganisha na hapa kwetu.
  Hebu tujaribu na upinzani, wakikosea si tunawaondoa hata kabla ya miaka 5 kuisha!
  QUOTE=Kisarawe 2015;2598155]Ki historia, ni wilaya ya kwanza kuanzishwa Tanzania na mkoloni

  Lakini kimaendeleo ni maskini kuliko zote Tanzania na hata wilaya ya Mafia ina afadhali

  Pia msisahau kuwa ni wilaya ambayo jimbo lake limekuwa likiwasilishwa na CCM tokea uhuru...na moja kati ya waliowahi kuwa wabunge wa Kisarawe ni pamoja na Marehem Kigoma Malima (ambaye mwanae Adam ndiye mbunge wa Mkuranga), Athumnani Janguo (aliyewahi kuwa mkurugenzi wa Bandari ) na sasa hivi jimbo hili limeshikiliwa na jamaa anayeitwa SULEIMAN JAFO ambaye ame spend si chini ya milioni 400 ili jina lake lipitishwe kwenye Chama na baadae kushinda kirahisi kwenye ubunge. Sasa hizo pesa zenyewe kumbe alikuwa kaziiba kule alikokuwa anafanya kazi kwenye NGO ya PLAN INTERNATIONAL sasa hivi amekubaliana nao kuwa atazirejesha kidogo kidogo.  Tangua ateuliwe kuwa mbunge hakuna lolote alilolifanya la maana. na tunaweza kusema kuwa kazi kubwa inafanya na NGO ambazo zinachimba visima vya maji na kutoa huduma za afya. Sasa CCM hatujui mmetuletea mbunge dizaini gani kwani hana uadilifu. Kama aliweza kuwaibia hao Plan International ndio atashindwa kutuibia sisi wananchi wa kawaida?  Lakini kama mbunge hajafanya lolote zaidi ya kula posho za milioni 15 kila mwezi kama mbunge huku jimbo lake likiongoza kwa watu walio wasio jua kusoma au kuandika.

  So far alichokifanya ni kutoa ardhi yenye hecta 200,000 kwa shirika la kidini ambalo limesema kuwa ile ardhi ni kwa ajili ya investment ya kujenga nyumba za ibada

  Jamani hicho ndio kilio chetu wana Kisarawe. Na tunaomba msaada wenu wa kimawazo namna ya kufanya ili hali zetu ziwe walau na afadhali.[/QUOTE]
   
 17. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #17
  Oct 6, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,524
  Likes Received: 1,005
  Trophy Points: 280
  Ninavyomfahamu huyo mbunge wao ni mstaarabu tena mwenye huruma
  kabla hajawa mbunge kwa ushahidi wa wazi kabisa amewahi hata kuwasomesha
  na kuwasaidia watu kadhaa kwa fedha zake binafsi. Ni mstaarabu sana siwezi kuamini
  hizi shutuma. Mpeni muda naamini yaliyo ndani ya uwezo wake yatafanyika na sio
  kuja kumchafua huku jukwaani. Tena ni mtu rahisi hata kuongea nae kama unahitaji
  hana makuu.......... Unamsingizia.
   
 18. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #18
  Oct 6, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,549
  Likes Received: 18,220
  Trophy Points: 280
  Ukiweka jina la jimbo fulani na 2015 by implication unamaanisha your a countender for 2015. That being the case jenga hoja utafanya nini na sio kuingia kwa discredit aliyepo hakufanya hiki na kile etc and if there is anything you can do please do!.

  Naomba usinigeuzie kibao kuoanisha asili ya uvuvu kwa watu wa ukanda wa pwani na udini. Mbona Wapemba na Waunguja wote Waisilamu lakini wamoja wavivu wengine sio wavivu?. Mbona watu wa Bagamoyo na Watu wa Kigoma wote Waislamu wengine wavivu wengine wachapa kazi?. Hata mataifa ya Kiislamu ni vivyo hivyo, mbona Saudia na Turkey yote ni mataifa ya Kiislamu wakati wamoja ni wavivu na wengine ni wachapa kazi.

  Uvivu ni hulka ya baadhi ya jamii hauna dini. Kilimanjaro asilimia kubwa Wakristu. Watu wa Machame ni Chapa kazi sana kwenye saka pesa. Watu wa Kirua Vunjo ni wavivu lala usingizi. Wanawake wa Machame wanajishughulisha na shughuli mbali mbali wakati wale wa Marangu wabasubiri kuolewa tuu na wote ni dini moja.

  Mimi ni Msukuma wa Mwanza chapa ng'ombe tunakula ugali mlima asubuhi ni mpaka usiku ndipo tunakula tena na kushinda siku nzima na jembe mkononi. Wenzetu Wakerewe na Wakala hawako hivyo na wote tuko dini moja.

  Watu wa Iringa na Mbeya pia ni dini moja. Wadada zao wengine hujituma sana hivyo kuongoza katika soko la ajira ya sekta fulani kwa bidii ya kazi. Wengine wamepachikwa jina la maharagwe ya sehemu fulani ni maji mara moja. Hapo kuna udini?.

  Naomba tukijadili issues ambazo hazina udini usizivishe koti la udini kutafuta sympathy ili wadini wanishukie kuwa nami mdini kama walivyofanikiwa kupunguza kura za Chadema pale Igunga kwa mtandio kuitwa hijab!.
   
 19. tunalazimika

  tunalazimika JF-Expert Member

  #19
  Oct 6, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,100
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  naona una_test mitazamo yetu katika mkakat wako wa kugombea 2015 _hata ivo na wewe hutofaa kwsbb umeanzisha siasa za majitaka_Jafo ni chaguo la wananchi, dogo katoka familia masikin sana_hata suti ya kwanza kwendea bungen wananch walichangishana na iman yao kwake ilitokana na namna alivyoisimamia Plan International kwa uadilifu na kuwasaidia watoto wa masikin kuwalipia karo ktk hatua mbalimbali za masomo na kuwasaidia kutatua tatizo sugu la maji vijijini_ni kwa ajili hiyo hakutumia fedha kabisa kumuangusha Dibibi aliyekuwa mwenyekiti wa halmashaur na aliyekuwa kaandaliwa na Janguo_hata sasa Plan Inter wanamuona kama role model wao_achana na siasa zako za maji taka_kuchelewa kuendelea kwa kisarawe ni issue mtambuka co kama unavyo jaribu kufikiri_kuna mikoa kama Shinyanga imekuwepo kabla ya Nairobi na ikumbukwe huko dhahabu na almasi wananch walikuwa wanachezea bao_mbona haijaendelea? Mikoa kama Kigoma utasemaje ?
   
 20. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #20
  Oct 6, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Nikusahihishe kidogo
  Wilaya ya kwanza ni wilaya ya mbulu mkoani manyara
   
Loading...