Kisandu: Taarifa kwa umma

Kisandu: Taarifa kwa umma

Katibu wa mawasiliano na uenezi Taifa
Kitengo cha vijana wa NCCR.

Duuuuh!!
Huyu jamaa ni boga bovu.
 
Hawa vijana wa vyama vya upinzani ni aibu tupu kumbe hata alipotimuliwa hawakukose hata kidogo


Huyu kijana ni kichaa sana sasa hata Makupa kasema haya ? Kisandu wewe ni laana kubwa .
 
Dogo huyu ni mwepesi sana anadhani kusoma nchini kinaweza kuwa kigezo cha kuwa mzalendo!

Kweli hafai kuwa kiongozi wa watu maana hajui kufikiri vyema!
 
Hawa vijana wa vyama vya upinzani ni aibu tupu kumbe hata alipotimuliwa hawakukose hata kidogo

Mkuu Makupa leo naona walau umeelewa kwanini Chadema inafukuza hawa Masalia wajingawajinga..!
 
Last edited by a moderator:
ameishia kidato cha ngapi????????????

anazitafuta akili za chuo kwa nguvu ambazo hana..... ubongo wa vidato hata ukifika chuo umejaa matope.

Eti huyu ndiye alikuwa mkuu wa ufundi wa kundi la Masalia.Wakati mwingine unaweza kujiona kama unajidhalilisha kujibizana na mtu wa hovyo hivi.
 
anatafuta atoke vipi, jamaa ni sawa na wale wadudu wanao kuwaga kwenye msafara wa Mamba, na jamaa hata Urais wa Mke wake hafai na atakuja olewa badala ya kuoa

Halafu wakati mwingine nakilaumu chama changu Chadema ilikuwaje wakapitisha kituko hiki kugombea ubunge Lushoto?

Come on Dr Slaa this boy was too low for Chadema....!
 
taarifa kwa umma upi?
hivi kila mtu anaweza kutoa taarifa kwa umma?
nadhani huyu bwana na kadegree kake ka kudesa anatapatapa
agombee kwanza udiwani au mwenyekiti wa kijiji
urais mbali sana,sidhani kama anafahamika zaidi ya hapa JF na huko TANGA alikotimuliwa
tehe tehe teheeee eti urais. dah
 
Hapo anamaanisha asiwe amezidi miaka 25 kwa sababu shule za kata wameanza kugraduate juzijuzi tu!
 
Kama mtu mwenye digrii yupo hivi,basi digrii hapa Tz ni sumu na hazifai bora wa tz wote tukasome VETA!Ndio maana nchi tajiri watu maskini viongozi dizaini hii!hafai hata kuwa meneja wa bar!Na ninyi walimu mliomfaulisha digrii ni aibu tupu!
 
Huyu dogo inaelekea starehe yake ni kukashfiwa ndio maana hajaacha kupost pumba zake humu.Ajiulize kwanza wezi wa pesa za epa kama wote wamo kwenye nafasi kati ya alizozitaja.
 
Huyu ndiyo alikuwa analilia kupewa nafasi za kwenda kufanya operation za CDM mikoani kwa uharo huu anaomwaga hapa? Mbatia kaokota garasa hapa, historia haijui, statement ipo too illogical, haijui majukumu ya urais hata kidogo ana kazi ya kubwabwaja. Mpuuzi kaandika upuuzi na kwa hyo hatuna budi kumpuuza.
 
Ulikuwa halali kabisa kukimbia Chadema.Nyerere hajawahi kushika wadhifa wowote isipokuwa ni wadhifa wa kichama.Hata kale kawadhifa ka uwaziri mkuu wa Tanganyika aliko kuwa nako hukajui halafu unataka kuwa rais wa tz.kumbe akina Mulugo mko wengi ambao hamjui tz ni muungano wa nchi ipi na ipi.
 
Hivi huyu Kisandu ni lazima aandike kila siku humu Jf ? Aliingiaje Cdm huyu naye ?
 
Utumbo mtupu hapa chini!

Ndio hoja gani ya mtu anayetaka kuwania uraisi?

We unapoteza muda kumbe hata ukatibu kata hufai!

TAARIFA KWA UMMA
Ndugu wanahabari kumekuwepo na wimbi kubwa sasa la viongozi wengi
hapa nchini nikiwemo na mimi kuutaka Urais wa mwaka 2015, kila mmoja
amekuwa na vigezo vyake kwa maslahi yake binafsi bila kuangalia
wananchi wa Tanzania wanataka nini haswa.

Kimsingi niliwahi kusema Rais ajaye anatakiwa awe hajawahi kuwa mbunge
au waziri au Diwani na ndio anaweza kuwa kiongozi mzuri maana atakuwa
hana chembechembe ya kifisadi kama ilivyokuwa kwa mwl. Nyerere ambaye
hakuwahi kuwa mbunge wala waziri zaidi ya uongozi ndani ya chama
chake.

Sasa leo na hili la Elimu, kutokana na kiwango cha elimu kushuka hapa
nchini tatizo inaonekana kuwa na mwingiliano wa kisiasa, wanasiasa
wengi hapa nchini hawaumiizwi na matokeo mabovu ya shule zetu za
kitanzania na hii ni kwasababu wao wenyewe wamesoma nje ya nchi na
watoto wao wanasoma International Schools huku sisi watoto wa wakulima
tukiumia na shule yatima za kata.

Kwa mantiki hii Rais ajaye wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
anatakiwa awe ni yule aliyesoma shule zetu za kata kwani hii itasaidia
kujua machungu ya Watanzania na adha ya elimu hapa Tanzania, pia
lazima awe amesoma vyuo vya hapahapa Tanzania kwani itasaidia Rais
ajaye kujua matatizo ya bodi ya mikopo, migomo ya vyuo na mahitaji ya
wanachuo.

Mimi kama mmoja wapo wa Walimu waliopitia kufundisha shule hizi za kata
na kusoma vyuo vya hapahapa Tanzania
nina nafasi kubwa zaidi ya kuwa Raisa wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwani 97% ya wanafunzi wamesoma shule hizi na vyuo hivi na
wengine bado wanasoma na ndio wapiga kura wa Rais ajaye. Hawa
waliosoma nje ya Tanzania hawatufai kabisa maana hawajui machungu ya
watanzania kabisa na wala hawajaonja ladha ya uchungu wa elimu ya
kitanzania.

DEOGRATIUS KISANDU
KATIBU WA UHUSIANO NA UENEZI TAIFA, KITENGO CHA VIJANA WA NCCR-mageuzi.
20/01/2013

​
 
Back
Top Bottom