Kisandu: Taarifa kwa umma

Kisandu: Taarifa kwa umma

Aliyemfukuza huyu CHADEMA hakukosea.Yaani ni mtupu kumkichwa.!

Kabisaa mkuu kama mawazo yake ndio haya kweli alikuwa mzigo ndio maana alipoteza jimbo la Lushoto kizembe lilikuwa letu kabisa lile!
 
Siamini Kama huyu jamaa alikuwa CDM! Yaani pumba tupu, kwa hiyo Kama Nyerere Naye alikuwa waziri mkuu Wa Tanganyika kabla hajawa rais!
Wakati mwingine ukikaa kimya unaweza keheshimiwa kwa kutojulikana
Kama ni mbumbumbu lakini ukijionesha tu kwa pumba Kama hizi
bassi Tena!
Mkuu huyu jamaa alikua CDM ila kama ujuavyo chadema ilivyo makini ilimdhibiti kwa kutotoa matamko ya ajabuajabu kama haya,alivyoona hawezi kufunga domo payuka akasoma alama za nyakati mapema na kutimkia huko NCCR ili aendeleze payuka payuka
 
ndio maana wengine husema iache CCM itawale milele kama hizi ndizo akili za wapinzani wa CCM.
 
ameishia kidato cha ngapi????????????

anazitafuta akili za chuo kwa nguvu ambazo hana..... ubongo wa vidato hata ukifika chuo umejaa matope.
 
ndio maana wengine husema iache CCM itawale milele kama hizi ndizo akili za wapinzani wa CCM.

Mkuu hilo halina ubishi kama hawa ndio viongozi wa kitaifa , ccm tuna miaka mingine 200 ya kukaa madarakani
 
Aaaaaghaaaaaaaaa!!!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
hahahaha...jamaa kapewa cheo kwenye kitengo ambacho hakipo kabisa NCCR. ni sawa leo aambiwe amekuwa mkuu wa mkoa wa Lushoto. i d.i.ots

kiwatengu bana hahahahaaaaa kwa hiyo huyu kisanduku/kisandu hawezi jua kama atakuwa kauziwa nyau baadala ya sungura
 
Napata tabu sana kumjadili huyu jamaa,kweli ametoka kwenye chama chetu? Au ndo kuchanganyikiwa?
 
kwa taarifa tu, nyerere alishawahi kuwa mbunge wa morogoro. huyu mwenye hii thread katoka kisiwa gani?
 
KISANDU akili mgando iliyooza....!! I don't think kama ujinga wako ndio uko wazi kiasi hiki...., very unfortunate to have people like you in Tanzania.
 
aaaah,kumbe cdm wakikufukuza hawakurupuki,huyu dogo kumbe ni zero namna hii.Sasa nakuonya usije ukaingilia anga za mbatia tutakusahau.Ni ushauri tu hutaki unaacha.
 
Nawasilisha taarifa ya Mh. Kisandu:

TAARIFA KWA UMMA
Ndugu wanahabari kumekuwepo na wimbi kubwa sasa la viongozi wengi
hapa nchini nikiwemo na mimi kuutaka Urais wa mwaka 2015, kila mmoja
amekuwa na vigezo vyake kwa maslahi yake binafsi bila kuangalia
wananchi wa Tanzania wanataka nini haswa.

Kimsingi niliwahi kusema Rais ajaye anatakiwa awe hajawahi kuwa mbunge
au waziri au Diwani na ndio anaweza kuwa kiongozi mzuri maana atakuwa
hana chembechembe ya kifisadi kama ilivyokuwa kwa mwl. Nyerere ambaye
hakuwahi kuwa mbunge wala waziri zaidi ya uongozi ndani ya chama
chake.

Sasa leo na hili la Elimu, kutokana na kiwango cha elimu kushuka hapa
nchini tatizo inaonekana kuwa na mwingiliano wa kisiasa, wanasiasa
wengi hapa nchini hawaumiizwi na matokeo mabovu ya shule zetu za
kitanzania na hii ni kwasababu wao wenyewe wamesoma nje ya nchi na
watoto wao wanasoma International Schools huku sisi watoto wa wakulima
tukiumia na shule yatima za kata.

Kwa mantiki hii Rais ajaye wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
anatakiwa awe ni yule aliyesoma shule zetu za kata kwani hii itasaidia
kujua machungu ya Watanzania na adha ya elimu hapa Tanzania, pia
lazima awe amesoma vyuo vya hapahapa Tanzania kwani itasaidia Rais
ajaye kujua matatizo ya bodi ya mikopo, migomo ya vyuo na mahitaji ya
wanachuo.

Mimi kama mmoja wapo wa Walimu waliopitia kufundisha shule hizi za kata
na kusoma vyuo vya hapahapa Tanzania
nina nafasi kubwa zaidi ya kuwa Raisa wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwani 97% ya wanafunzi wamesoma shule hizi na vyuo hivi na
wengine bado wanasoma na ndio wapiga kura wa Rais ajaye. Hawa
waliosoma nje ya Tanzania hawatufai kabisa maana hawajui machungu ya
watanzania kabisa na wala hawajaonja ladha ya uchungu wa elimu ya
kitanzania.

DEOGRATIUS KISANDU
KATIBU WA UHUSIANO NA UENEZI TAIFA, KITENGO CHA VIJANA WA NCCR-mageuzi.
20/01/2013

​


Am still lost completely, hii kauli yako kweli bwana kisandu?

Kama kweli ni yako hufai hata kuwa balozi wa mtaa au nyumba kumi. Mtu wa kauli hii ni zezeta.

Tafakali maelezo yako kama niwewe kweli otherwise should be somebody else who wishes to destroy you.
 
Am still lost completely, hii kauli yako kweli bwana kisandu?

Kama kweli ni yako hufai hata kuwa balozi wa mtaa au nyumba kumi. Mtu wa kauli hii ni zezeta.

Tafakali maelezo yako kama niwewe kweli otherwise should be somebody else who wishes to destroy you.

Unafikiri anaweza kufanya zaidi ya hapo alipofikia? Hiyo IQ hana ........huyo ndio aliandaliwa press conference na kupokelewa kama shujaaa...
 
kwi kwi kwi kwi

Kuna shangazi yangu aliwahi kuniambia kwamba ninapotafuta mchumba, basi nisiangalie yule kimbelembele, yule atakayependa kuongoza mzungumzo, kulia zaidi kwenye misiba, kuzungmza kwa sauti kubwa, kuchafuka kuliko wote kwenye shughuli za jamii au hata yule anayejifanya ananipenda kuliko baba yake na mama yake......... NILIMUAMINI

Tuna kakikundi kadogo ka watu ambao daima hupenda kuwa kwenye high table, haijalishi ni ya kanisa, bar (iwe ya kifahari, ya gongo nk.) haka kakikundi huwa kama vile wanawashwa, lazima wawe high table, lazima wawe wasemaji na wawakilishi wa mawazo ya wenzao, na siku hizi wengine wamejipenyeza kwenye nyumba za ibada... kuwa maimam, wachungaji, maaskofu na hata mitume!!!!!!!!

Deo is no exception..... he likes dem high tables, at any cost

One thing in common kwa hawa watu..... THEY ARE ALL MEDIOCRE, MYOPIC, SELF CENTERED, AND SADLY VERY LIMITED IN KNOWLEDGE

DEO KISANDU, YOU ARE ONE OF DEM ----- SI MBAYA KWAKO INAKUPA RAHA YA MOYO
 
Back
Top Bottom