Kisandu: Taarifa kwa umma

Kisandu: Taarifa kwa umma

Unafikiri anaweza kufanya zaidi ya hapo alipofikia? Hiyo IQ hana ........huyo ndio aliandaliwa press conference na kupokelewa kama shujaaa...

Mkuu tunakazi, hii ni aibu ya mwaka huyu anapewaje madaraka kilaza kiasi hiki! hakika haya ni ya firauni baada ya yale ya shonza (buwa) kujipima kwa Dr Slaa (Mbuyu).
 
anatafuta atoke vipi, jamaa ni sawa na wale wadudu wanao kuwaga kwenye msafara wa Mamba, na jamaa hata Urais wa Mke wake hafai na atakuja olewa badala ya kuoa
 
kaka tupo nyuma yako,lakini rais ajaye hawezi kutoka kilimanjaro na arusha.tunataka mzalendo na asie na ubaguzi[/Mkuu, kwani mikoa hiyo uloitaja imeshawah kutoa rais wa nchi hii? Hao marais ambao hawatoki huko, wameifanyia nini nchi hii? Acha wivu wa kike, tunahitaji rais mzalendo regardless anatoka ukanda upi.
 
Kisandu Deogratius badilisha game, hii unayocheza timu itazidi kuporomoka madaraja mpaka daraja sifuri.

Anyway, kama uwezo ndio umeishia hapa ndio basi tena!
 
Nawasilisha taarifa ya Mh. Kisandu:

TAARIFA KWA UMMA
Ndugu wanahabari kumekuwepo na wimbi kubwa sasa la viongozi wengi
hapa nchini nikiwemo na mimi kuutaka Urais wa mwaka 2015, kila mmoja
amekuwa na vigezo vyake kwa maslahi yake binafsi bila kuangalia
wananchi wa Tanzania wanataka nini haswa.

Kimsingi niliwahi kusema Rais ajaye anatakiwa awe hajawahi kuwa mbunge
au waziri au Diwani na ndio anaweza kuwa kiongozi mzuri maana atakuwa
hana chembechembe ya kifisadi kama ilivyokuwa kwa mwl. Nyerere ambaye
hakuwahi kuwa mbunge wala waziri zaidi ya uongozi ndani ya chama
chake.

Sasa leo na hili la Elimu, kutokana na kiwango cha elimu kushuka hapa
nchini tatizo inaonekana kuwa na mwingiliano wa kisiasa, wanasiasa
wengi hapa nchini hawaumiizwi na matokeo mabovu ya shule zetu za
kitanzania na hii ni kwasababu wao wenyewe wamesoma nje ya nchi na
watoto wao wanasoma International Schools huku sisi watoto wa wakulima
tukiumia na shule yatima za kata.

Kwa mantiki hii Rais ajaye wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
anatakiwa awe ni yule aliyesoma shule zetu za kata kwani hii itasaidia
kujua machungu ya Watanzania na adha ya elimu hapa Tanzania, pia
lazima awe amesoma vyuo vya hapahapa Tanzania kwani itasaidia Rais
ajaye kujua matatizo ya bodi ya mikopo, migomo ya vyuo na mahitaji ya
wanachuo.

Mimi kama mmoja wapo wa Walimu waliopitia kufundisha shule hizi za kata
na kusoma vyuo vya hapahapa Tanzania
nina nafasi kubwa zaidi ya kuwa Raisa wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwani 97% ya wanafunzi wamesoma shule hizi na vyuo hivi na
wengine bado wanasoma na ndio wapiga kura wa Rais ajaye. Hawa
waliosoma nje ya Tanzania hawatufai kabisa maana hawajui machungu ya
watanzania kabisa na wala hawajaonja ladha ya uchungu wa elimu ya
kitanzania.

DEOGRATIUS KISANDU
KATIBU WA UHUSIANO NA UENEZI TAIFA, KITENGO CHA VIJANA WA NCCR-mageuzi.
20/01/2013

​

Kisandu realy you have to change!what you are preaching is totaly out of human conciousness!
Nasema hvi kwa sababu:
1.huwezi sema raisi lazima atoke shule za kata eti kwa sababu zaidi ya asilimia 97(how far this data is valid?) wamesoma huko!kama kigezo ni wingi wa wapiga kura basi tungesema awe mkulima toka kijijini maana takribani zaidi ya 80% ni wakulima na wanapiga kura!
2.mimi nimesoma Kibaha kwa mfano but ni mtoto wa mkulima.je sina haki ya kupigiwa kura na kuwa raisi?
3.unamjua waziri mkuu wa kwanza wa tanzania?unavyosema Jk Nyerere hajawahi kuwa waziri unataka kutuaminisha nini?
4."wanasiasa
wengi hapa nchini hawaumiizwi na matokeo mabovu ya shule zetu za
kitanzania na hii ni kwasababu wao wenyewe wamesoma nje ya nchi na
watoto wao wanasoma International Schools"
Unamaanisha wenye matokeo mabovu toka shule za kata ndo wawe raisi?ulivotangaza kuutaka uraisi wewe umetokea shule za kata?
JARIBU KUFIKIRIA,ADDRES MATATIZO YA WATANZANIA NA SIO KUANDIKA KILA KINACHOKUJA KICHWANI MWAKO!SOMETIMES UNADHALILISHA ELIMU YAKO!JITOFAUTISHE NA KINA NAPE et al!
 
Ana shahada ya ualimu ya ualimu, lakini sidhani kama ni kutoka udsm,lazima itakuwa nii kutoka kwenye hivi vyuo vya voda fasta[/Q Mkuu, sidhani kama viongozi wazuri wanatoka UDSM pekee. Kumbuka matatizo ya nchi hii yamechangiwa kwa kiasi kikubwa ma hao UD gradute.
 
Nimekaa hapa peke yangu navuta picha wakti huo kisandu ndio rais. Du bora jk mara 100000.
 
Huyu kijana kumbe hana akili Nyerere aliwahi kuwa mbunge wa jimbo la pwani, na akawa waziri mkuu kabla nchi haijawa jamhuri!
 
kiwatengu bana hahahahaaaaa kwa hiyo huyu kisanduku/kisandu hawezi jua kama atakuwa kauziwa nyau baadala ya sungura

huyu jamaa c boya? hana mbele wala nyuma...anakera sana!! ts better awe anatulia..
 
Nawasilisha taarifa ya Mh. Kisandu:

TAARIFA KWA UMMA
Ndugu wanahabari kumekuwepo na wimbi kubwa sasa la viongozi wengi
hapa nchini nikiwemo na mimi kuutaka Urais wa mwaka 2015, kila mmoja
amekuwa na vigezo vyake kwa maslahi yake binafsi bila kuangalia
wananchi wa Tanzania wanataka nini haswa.

Kimsingi niliwahi kusema Rais ajaye anatakiwa awe hajawahi kuwa mbunge
au waziri au Diwani na ndio anaweza kuwa kiongozi mzuri maana atakuwa
hana chembechembe ya kifisadi kama ilivyokuwa kwa mwl. Nyerere ambaye
hakuwahi kuwa mbunge wala waziri zaidi ya uongozi ndani ya chama
chake.

Sasa leo na hili la Elimu, kutokana na kiwango cha elimu kushuka hapa
nchini tatizo inaonekana kuwa na mwingiliano wa kisiasa, wanasiasa
wengi hapa nchini hawaumiizwi na matokeo mabovu ya shule zetu za
kitanzania na hii ni kwasababu wao wenyewe wamesoma nje ya nchi na
watoto wao wanasoma International Schools huku sisi watoto wa wakulima
tukiumia na shule yatima za kata.

Kwa mantiki hii Rais ajaye wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
anatakiwa awe ni yule aliyesoma shule zetu za kata kwani hii itasaidia
kujua machungu ya Watanzania na adha ya elimu hapa Tanzania, pia
lazima awe amesoma vyuo vya hapahapa Tanzania kwani itasaidia Rais
ajaye kujua matatizo ya bodi ya mikopo, migomo ya vyuo na mahitaji ya
wanachuo.

Mimi kama mmoja wapo wa Walimu waliopitia kufundisha shule hizi za kata
na kusoma vyuo vya hapahapa Tanzania
nina nafasi kubwa zaidi ya kuwa Raisa wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwani 97% ya wanafunzi wamesoma shule hizi na vyuo hivi na
wengine bado wanasoma na ndio wapiga kura wa Rais ajaye. Hawa
waliosoma nje ya Tanzania hawatufai kabisa maana hawajui machungu ya
watanzania kabisa na wala hawajaonja ladha ya uchungu wa elimu ya
kitanzania.

DEOGRATIUS KISANDU
KATIBU WA UHUSIANO NA UENEZI TAIFA, KITENGO CHA VIJANA WA NCCR-mageuzi.
20/01/2013

​

Hivi huyu ndio anagombea urais????!!!! Dunia imekwisha, Mungu turehemu Tanzania! Kweli amesoma shule ya kata!
 
Sitaki ni amini kama uwezo wake wa kufikiri au ni Viroba vya wikend
 
Hizi ni akili za analogia..zilizimwa na mitambo yake wakati wa digitali....hamna kitu kichwani humu!loooo looh nyeee khaaa mkwi dadee umwana wa Sekavindi nene!uhuro
 
Hahahahaha, and this claims to be a presidential materials. TUMEVAMIWA....!
 
Nashindwa kuelewa NCCR ni chama cha namna gani? Hivi kesi ya kafulila bado ipo au alisamehewa?
 
Sidhani kama kuna waandishi wa habari wa kupoteza muda kuandika utumbo kama huu.
 
CDM hawakukosea kumfukuza huyu jamaa!
Mawazo hafifu kabisa! Bila aibu!

Wanahabari nao wana kazi sana, huyu nae eti pia anawaita na kuwapa taarifa kwa 'umma!!' Upuuzi mtupu!

Kwa uvivu wa kufikiri anadhani wale wote wanaotuibia rasilimali za taifa letu na wale tunaowalalamikia kwa kukosa uzalendo wamesoma nje ya Tanzania?!?

Hapa suala sio nani kasoma wapi, suala ni namna mtu huyo anaweza kusimamia misingi ya utaifa kwa uzalendo mkubwa!
Hata asipokuwa na elimu kubwa, aweze tu kuwa na maono juu ya pale taifa linatakiwa kwenda na asimamie hilo kwa maneno na matendo!

Kwa taarifa tu, huyu raisi wetu aliyesema hajui kwa nini sisi watanzania ni masikini kasoma humu humu pia! Sasa anataka kutuambiaje?
 
Back
Top Bottom