Dalali kanipeleka hadi kwa mwenye nyumba, tukakubaliana jioni saa kumi nije kulipa hela, kodi ya miezi kumi, vile naondoka nafika nyumbani natoa taarifa jamani nimepata nyumba jioni naenda kulipia, kumbe huku nyuma kaja mtu mwingine kalipia, kodi ya miezi kumi na mbili. Jioni narudi, heee! naambiwa nyumba imelipiwa tayari. Nikiwa na Burungutu langu la mihela, nkapiga simu kwa boyfie kuomba ulinzi. Naondoka kufika nyumbani The same dalali ananipigia simu, "dada njoo ulipie kesho asubuhi, yule jamaa kaghairi". Nlichooookaaaaa, nkasema sitaki nyumba tena