Kisa gani kilichowahi kukuta na dalali ambacho huwezi sahau?! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kisa gani kilichowahi kukuta na dalali ambacho huwezi sahau?!

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by stineriga, Jun 24, 2012.

 1. stineriga

  stineriga JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 2,033
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  madadali ni watu muhimu kwenye jamii ni kweli kwamba huwezi pata nyumba hapa mjini bila kupitia wao, au labda itokee bahati tu rafiki/ndugu yako anahama mahali akuunganishie, la sivyo utasaga meno bila kuwatumia wao. pamoja na umuhimu wao wana kerooo nyingi sana na wateja wao. je umeshawahi kumbwa na kisa gani na madalali usichoweza kukisahau...??!!!
   
 2. ney kush

  ney kush JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 16, 2012
  Messages: 1,195
  Likes Received: 377
  Trophy Points: 180
  kiwanja kimoja tulinunua watu nane
   
 3. stineriga

  stineriga JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 2,033
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  ilikuwaje sasa hapo, ulifanyaje?
   
 4. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #4
  Jun 25, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Nilienda pangishwa hall 3 palechuko kikuu nyumba ya warden.
   
 5. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #5
  Jun 25, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  usichukue tu dalali wa mtaani tafuta yule ambae anajulikana ambae rafiki/ndugu yako alishawahi kuwatumia. Mi biashara yangu hua inabidi niwatumie hawa watu kwa hiyo through experience najua wale wakuaminika safi na wale ovyo..kuna wengine wanakupeleka kwenye nyumba wanakuonyesha nyumba na mwenye nyumba kabisa kumbe ni feki unatoa hela yako huwaoni tena coz wanabadilishaga namba zao mara kwa mara. Kuweni waangalifu na hawa watu
   
 6. bombu

  bombu JF-Expert Member

  #6
  Jun 25, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,134
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Dalali kanipeleka hadi kwa mwenye nyumba, tukakubaliana jioni saa kumi nije kulipa hela, kodi ya miezi kumi, vile naondoka nafika nyumbani natoa taarifa jamani nimepata nyumba jioni naenda kulipia, kumbe huku nyuma kaja mtu mwingine kalipia, kodi ya miezi kumi na mbili. Jioni narudi, heee! naambiwa nyumba imelipiwa tayari. Nikiwa na Burungutu langu la mihela, nkapiga simu kwa boyfie kuomba ulinzi. Naondoka kufika nyumbani The same dalali ananipigia simu, "dada njoo ulipie kesho asubuhi, yule jamaa kaghairi". Nlichooookaaaaa, nkasema sitaki nyumba tena
   
 7. stineriga

  stineriga JF-Expert Member

  #7
  Jun 25, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 2,033
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  dalali anakwambia nyumba ina tiles ina vioo, ipo mwakemwake, kumbe tu anaitamani 5000/= yako ya usumbufu, ukifika nyumba ni mboovvvuuu, ukimuuliza dalali ndio hii nyumba ulikuwa unaniambia au nyingine?? anaanza kujing'atang'ata...
  hii ilinitokea na mbona aliitoa 5000/= yangu kwa kumkaba!!
   
 8. GP

  GP JF-Expert Member

  #8
  Jun 26, 2012
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  asee, dalali aliniunganishia nyumba nikalipa mkwanja wa miezi 4, ile karibu mwezi wa tatu unakatika akamfuata faza hausi kumwambia apandishe kodi kuna kichwa kingine kinataka mjengo!, Mungu mkubwa faza hausi hana tamaa akanitonya chezo zima, ilibaki kidogo nimzabe vibao dalali, anazani hela inatingishwa tu juu ya mti.
  tena madalali wengine ni washenzy, mkataba unapoisha wakati wa kurenew ukifika wanaenda kwa mwenye nyumba kuchukua ganji au usipokua muelewa wanakuja kwako uwagee ganji ya kurenew mkataba.
   
 9. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #9
  Jun 26, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Nilijenga 'banda' nyuma ya dada mmoja akashitukia akageuka na kuniambia, "Pole"

  Ilikuwa imeshona
   
 10. charminglady

  charminglady JF-Expert Member

  #10
  Jun 26, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 17,856
  Likes Received: 1,131
  Trophy Points: 280
  Dah, me dalali alitaka kunipangisha frame ya biashara ambayo ilishalipiwa na watu wengine wawili... ilikuwa hivi mtu wa kwanza alilipa ili aanzishe law firm baadaye mambo yakagoma aikabidi ahairishe, basi huyo mwenye Law firm akamtafuta mdada mmoja hivi ili wamrudishie kodi.... basi mdada akampatia yule mwenye Law firm kiasi cha kodi ile bila kumtaarifu mwenye nyumba. Siku ya siku mdada akawa anaandaa ile frame ili aanze biashara ya salon, lahaula mama mwenye nyumba akaja akamkuta anaweka vioo na makabati kwa ajili ya saluni. mama mwenye nyumba akamuuliza mbona walisema kuwa wanafungua ofisi ya sheria kulikoni na vioo tena? hapo ndipo mdada akafunguka issue nzima, mama mwenye nyumba akamwambia mdada sipangishi mtu anayetaka kufanya biashara ya saluni. basi mdada akamwambia nirudishe hela zangu mama mwenye nyumba akamwambia amfuate aliyempatia hela.... mpaka leo kesi ipo mahakamani..... na frame imefungwa hakuna kupangisha mpaka kesi iishe.... dah kidogo na mie niingizwe mkenge!!!!!!!!!!!
   
 11. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #11
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,481
  Likes Received: 12,754
  Trophy Points: 280
  oooh kuna kipindi dalali alinisakia chumba akanambia nilipe kodi mtu atahama siku flani'
  nkamcheck yule mpangaji akanihakikishia atahama siku ya siku nimechimoka job
  nkaenda home kubeba virago vyangu mpaka pale nkamkuta yule mpangaji hana hata dalili za kuhama
  \nikampigia dalali bila kujua niko pale akanidanganya jamaa kaondoka jana yake nkabwaga mizigo
  nkaenda nyumba ya pili nkanywa konyagi kubwa moja nkatafta askari mmoja rafki yangu nkampigia yule dalali tukutane pale riva side bar
  ubungo tupate za kujipongza maana najua ni mroho wa bia yaani alivyokuja hakuamini kilichompata hatakaa akisahau alilazimishwa kusaka chumba kingine mpaka akipate tena muda uleule akiwa chini ya ulinzi.....i hate dalaliz
  wezi tuu wanakuzururisha hata kama wanajua vyumba hakuna au ni stoo tu ilimradi uwape 5000 shenzi kabisaa
   
Loading...