Kisa Cha Wamakonde

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,809
Nakumbuka miaka mingi nyuma, kipindi kile cha mapigano kule Msumbiji, wamakonde wengi waliingia Mtwara kwa njia za panya. Na serikali ikaamua kuwatafuta na kuwaweka wamakonde wote wa Msumbiji kwenye camp maalum.

Nakumbuka watu wengi walikamatwa wakiwemo Watz na hao wa Msumbiji, tatizo likawa kila mtu anadai kuwa yeye ni Mtz.

Ikabidi Mkuu wa Kituo cha pale Newala kuwatumia Askari wa JKT watumie mbinu moja ya kuwauliza maswali na kusikiliza rafudhi zao. Na mnajuwa tena enzi zile JKT, walivyokuwa na nongwa... (Kumbuka kipindi kile cha wahujumu uchumi... Nakumbuka kuna jamaa mmoja alikamatwa na sabuni moja ya Lifeybouy... yaani alikoma...!! Aliambiwa apige push up kwa maelekezo ya Afande wa JKT, kwa kuambia hivi... Nikisema UP unakwenda UP nikisema JUU unakwenda JUU, sawaaa... haya Juu... Up... Juu... Up... Juu... Up..., jamaa kaganda ajui afanye nini. Akaambiwa unajifanya Fwara sisi ndo mafwara yenyewe kabisa...)

Tuendelee na kisa chetu cha Wamakonde... sasa mambo yalikuwa Hivi:

Baada ya watu wengi kukamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi halali wa serikari ya jamuhuri ya Bongo, mahojihano na watuhumiwa yalianza.

Kulikuwa na makundi mawili, kundi la kwanza (A) ni lile ambalo ni raia halali wa Bongo na kundi la pili (B) ni la kutoka Mchumbiji, I mean Msumbiji...

Afande wa JKT: Jina Rako rinani kijana

Mtuhumiwa1: Naitwa Chikirimu...!

Afande wa JKT: Kaa kure kundi 'B'

Afande wa JKT: Na wewe ndo rinani...!?

Mtuhumiwa2: Chigara

Afande wa JKT: Kaa kureeee... kundi 'B'

Afande wa JKT: Na wewe...?!

Mtuhumiwa3: chelikali Kuu (Huku akitoa mimacho kumtisha Askari wa JKT kwa jina lake)

Afande wa JKT: kaa kundi 'B', tafadhari

Afande wa JKT: Na wewe jina rako ri nani

Mtuhumiwa4: chipoti

Afande wa JKT : kure kundi 'B'

Afande wa JKT : na wewe...

Mtuhumiwa5: miye chichemi kitu

Afande wa JKT: Kundi 'B'

Mtuhumiwa5: lakini chijachema kitu...( huku akikokotwa na askri kuelekea kundi 'B')

Afande wa JKT: na wewe

Mtuhumiwa6: Mi jina langu refu chana...

Afande wa JKT: sawa lakini tuambie tupate kuandika

Mtuhumiwa6: Naitwa reli ya kati (akifikiri kuwa kwa kuwa reli ni ndefu watashindwa kumsajiri).

Afande wa JKT: iri jamaa rijamaa ra kundi 'B' tuu...

Afande wa JKT: na wewe...!

Mtuhumiwa7: Jina langu la ntu nkubwa

Afande wa JKT: ndio tuambie unaitwa nani...?

Mtuhumiwa7: (kwa kunong'ona) Naitwa Chintu binti Karume Nyerere

Kuangalia muda wangu ukawa unaniishia ikabidi niawaache niendelee na shughuli zangu, nikawaacha wakina Chantumavi, uchingizi nuchu, churuali ya nchungu na wengine wakisubiri zamu zao...
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom