Kisa cha Rais Ali Hassan Mwinyi kipigwa kibao akihutubia


Si kweli kwamba Uislamu unakataza categorically matumizi ya condom, si kweli matumizi ya condom huwa tu wakati wa nje ya ndoa.

Ukosefu wa elimu ya dini unasababisha tafsiri hii. rejea tundiko langu la hapo juu # 33
 
Du tz kweli noma---Pole msee wetu.

Naomba kuuliza pia Mauldi na kesho inaendelea kama siku ya mapumziko ama vipi?
 

Kama ni kweli kaleta jipya ambalo haliruhusiwi katika uIslam basi namuunga mkono mchapaji.

Lakini najikumbusha kuwa, kwenye halaiki ya watu, wengine ni machizi, pengine Mwinyi hakuleta chochote kipya au cha kuudhi bali tuu, jamaa ni chizi. Kama ni hivyo basi nampa pole Mzee Mwinyi na jamaa akapimwe akili.
 
Nimeona tendo hili la kishenzi ndani ya ITV. Kwenye picha inaonekana hata mzee Mwinyi alimshitukia mtu aliyekuja bila kutarajiwa. Alimpiga jicho kidogo halafu akaendelea na mambo yake. Jamaa akavunga kidogo halafu akamwasha kibao ambacho kimetoa hata echo.

I think this is really barbaric na I froze like ice. Watu wote niliokuwa nao really walikuwa embarassed. Kuna watu wanaongelea dini, siasa, .... Tuache upuzi tuwe wakweli katika nafsi zetu. Kitendo hicho ni cha kishenzi kabisa na aliyefanya lazima alipanga.

Suala ni kuwa tendo hili lime-expose security systems zetu vibaya mno. Hivi kweli viongozi wetu wana ulinzi wowote? Kwa jinsi nilivyoona kwenye picha.... assessment yangu inaniambia kuwa hakuna ulinzi. Yule mtu mzee Mwinyi alionekana kumsitukia. Lakini jambo rahisi, huyo mtu alikuwa kati ya watu wanaotakiwa kuonekana high table wakishughulikia vipaaza sauti? Hivi tuna ulinzi?

Siku raisi wa China alipofungua uwanja wa Taifa pale uwanjani Kikwete alilalamikia jinsi vipaaza sauti vilivyo kuwa vimewekwa. Kama vile aliyeviweka hajui urefu wa Kikwete. Hili la Mwinyi kupigwa si jambo dogo hata kidogo!

HIVI USALAMA WA TAIFA NI GENGE LA MAFISADI?
 
Nasikia watu wanaohusika na usalama walimpiga mtuhumiwa mtama na kuanza kumpiga --- sasa kama huyo mtu ana support nyuma yake basi itakuwa balaa haya ni mambo ya kuongea na kuelewana viongozi hawa wawe wanashauriwa cha kuongea kutokana n hali halisi
 

Kama hujui kama ni kweli Mwinyi kaleta kipya, ku speculate kuhusu kumuunga mkono "mchapaji" ni hatari. Unaunga mkono uchapaji bila kujua msingi wake? Hapo kuna a very central BUT.

Inabidi ujue kwanza, halafu unatoa maamuzi, sio unatoa maamuzi yaliyo na conditionalities kibao kama program ya computer.
 

Mzee kala chumvi nyingi na ametumia busara zake kuwaaza waamini wenzake watumie KONDOM kwa sababu ameshaona maadili ya UISLAM hayafuatwi na wengi.Hivyo ni bora awanusuru kwa hilo ili kama watamrudia tena MUUMBA WAO wafanya hivyo wakiwa free from HIV/aids and STDI
 
Jamani nina ombi: Kuna mtu humu ana picha ya Bush akirushiwa kiatu. Sasa tuna mtu kamchapa Mzee Mwinyi kofi: JK aliwahi kuanguka jukwaani. Je twaweza kupata picha hizi kwenye jamvi?
 
fikiria kama angekuwa na silaha sasa hivi ungekuwa msiba mkubwa bado turudi tusichanganye siasa na masuala ya dini kama viongozi wengi wanavyojaribu kufanya
 
jamani nina ombi: Kuna mtu humu ana picha ya bush akirushiwa kiatu. Sasa tuna mtu kamchapa mzee mwinyi kofi: Jk aliwahi kuanguka jukwaani. Je twaweza kupata picha hizi kwenye jamvi?

raisi wa china nae aliwahi kurushiwa kiatu na siku za karibuni raisi wa iran nae alirushiwa
 
fikiria kama angekuwa na silaha sasa hivi ungekuwa msiba mkubwa bado turudi tusichanganye siasa na masuala ya dini kama viongozi wengi wanavyojaribu kufanya

Umesema kweli. Jana tumeona kwenye vyombo vya habari, kuwa Mchungaji wa Illinois, USA aliyeuawa kanisani na muumini aliyeenda mbele kama anataka kumsalimia. Mnakumbuka mtu aliyemwua Rais Kabila mkubwa Ikulu. Mnakumbuka Mtu aliyemfokea Rais Mkapa wakati wa uzinduzi wa mfuko wa Waislamu, DSM. Mambo haya ni ya kuangalia sana, yanaweza kuleta msiba mkubwa kwa taifa. Idara ya Usalama wa Taifa imetekwa na mafisadi, inahangaika kuwalinda huku ulinzi wa viongozi ukiwekwa mashakani.
 
Bado natafakari vipi kama angepigwa hayo makofi na Mkristu? Pole mzee ruksa!

Nasikia jamaa alijifanya kama anakwenda kurekebisha microphone, akayeyusha kisha kamwachia bao.Kwahiyo body guard wake akabaki anaduwaa. Zikapigwa Takbir kadhaa, jamaa akashambuliwa kama mpira wa kona na waumini wenzie. Naona na yeye amepata ujira wake wa kutosha
 

Kipimapembe

Umepima pembe vema. Usalama wa Taifa watake wasitake na hata watuchukie hapa JF tutaendelea kuwaonyesha kuwa wako dhaifu.

Walikwishaona tukio lililomkuta Bush, walitakiwa na hadhari kwa kipindi hiki. Au Mwinyi hana ulinzi wa UwT?
 

Na kama Mwinyi alikuwa akiizungumzia Kondom kwa uzazi wa majira au kwa afya ya mama ndani ya ndoa basi you have got the point, otherwise, jibu unalo nadhani.
 
This is a very serious issue kwa usalama wa viongozi wetu wa kitaifa. Kama huyu mtu ameweza kumzaba kofi, ina maana kama angekua na kisu cha mfukoni angeweza kumuua.

Nashangaa mjadala huu unapoangaliwa kidini. So far, hakuna sehemu iliyoripotiwa kuwa huyo jamaa alimpiga kibao mwinyi kwa kupinga alichosema. Hakuna sehemu iliyoripotiwa dhehebu lake la kiimani. Hivyo basi mpaka sasa, hili suala linabaki kua la kiusalama na uzembe kwenye ulinzi wa viongozi wetu. Na kinachoshtua zaidi ni mtu kumfuata kiongozi mpaka high table na kufanikisha azma yake... Najua TISS watasingizia jamaa kichaa kuua noma.

Hiyo security detail yake ilikua wapi? au kumwaga mbwembwe tu na viearpeace...maana utakuta mtu yuko over 55yrs, mwili unamkaribia kapteni Komba anang'ang'ania kuwa bodyguard wa viongozi, ilimradi tu asipitwe na safari za nje au sababu ni "zamu" yake.

Mkuu Icadon ametuonyesha rika la walinzi wa viongozi wa nchi mbalimbali, mfano mzuri Israel. Jamaa ni vijana wadogo 20-30yrs, wako fit, na well armed. Kuwa openly armed in itself ni detterence tosha kwa wakorofi kama hawa.

Its about time the whole TISS iwe overhauled kabla makubwa zaidi hayajatokea.
 

Mkuu mimi nafikiri kwa maisha ya sasa sioni Kosa la Mzee Mwinyi na naamini kabisa kwamba you cant compete with nature na hili ndilo waumini wa madhehebu yote hawataki kulikubali. Issue ya ngono ni very complex hasa kwa sisi waafrika na wengineo sasa kama tutafumbia macho issue ya kondom nafikiri tutazidi kuangamia ingawa naelewa kusema kwamba watu wavae kondom kwenye dini ni kuchochea ngono ila nafikiri akili inakuwa kumkichwa kwa kila muhusika.
 

Apparently feeble and fragmented organization. What a shame on you TISS!
 

Nimekusikia, lakini msimamo wangu uko palapale, kama Mwinyi kaleta jipya la kuwapotosha waIslam ndio akazabwa kibao, basi astahili yake. Lakini kama huyo ni chizi au muhuni tuu basi nampa pole sana Mzee Mwinyi.

Huo ndio msimamo wangu, wako baki nao ungojee data zaidi.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…