Huko mafia nasikia kama si mwislam hukai walai.Watumishi wengi wa umma huishia kuhamia maana nasikia ubaguzi ni kiwango kikubwa mno
Uongo mtupu
Airport na Bandari vyote vipo mjini, kwahiyo uwe umeingia kwa boti au kwa ndege, kama safari yako inaishi mjini basi unatembea tu unless uwe unaenda vitongoji vilivyo nje kidogo!!
Huyo mleta mada ama nae ni MUONGO au ni mtu kutoka vijijini, na wala asiseme "kwetu Mafia tunafundishwa...." bali aseme "kwenye familia yao wanafundishwa..."
Sijaenda Mafia muda mrefu sana lakini hapa nitaizungumzia Mafia ya wakati huo ambayo pengine ndiyo tungesema ni hatari zaidi kwa watu wa dini zingine!
Ilikuwa ukiteremka airport na kutembea umbali mfupi, unakutana unakutana na NMB. Kutoka NMB, hatua chache mbele unakuta mkungu na chini yake kuna uwanja! Kusini Mashariki ya Uwanja kuna kanisa, nadhani la KKKT! Kanisa hili limezungukwa na makazi ya Waislamu na watu wanafanya ibada kama kawaida!
Kwenye Uwanja twaja, watu wanatumia sana kufanya mahubiri. Home kwetu ni town kabisa kiasi kwamba nikisimama karibu na dirisha naona kila kinachooendelea hapo uwanjani! Uwanja ule ni kawaida sana tena sana kukuta Wahubiri wa Kikristo wakitoa mahubiri yao na wengi wanatoka bara!
Kuna wakati walikuja Wahubiri wa Kikristo ambao lau kama pale ingekuwa ni Dar es salaam, wallah kingenuka kwa sababu yale hayakuwa mahubiri bali kashfa za Uislamu! Lakini walikaa Mafia wiki mzima na wakaondoka bila bughudha yoyote!
And what's even more interesting, ukiwa hapo uwanjani unawasikia watoto wa madrasa wakisoma kwa sababu Madrasa ipo hapo ukishamaliza tu uwanja!!! Huu uwanja nao, umezungukwa na makazi ya Waislamu!!
Sina uhakika kama hadi sasa yupo lakini wakati ule, ilikuwa ukipita tu ile madrasa, mbele kidogo unakutana na baa ya dada mmoja alikuwa anaitwa Hellen Lyimo!! Yaani umbali mfupi kutoka ilipo madrasa unakutana na baa ambayo mmiliki wake ni Mkristo!!
Hiyo ndo Mafia mnayodanganyana kinyume chake!! Uongo ambao kwa kawaida unaenezwa na watu wenye chuki tu za kidini!!!