Kisa cha mwanafunzi Fikiri... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kisa cha mwanafunzi Fikiri...

Discussion in 'Great Thinkers' started by ZeMarcopolo, Sep 27, 2012.

 1. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #1
  Sep 27, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Fikiri ni mwanafunzi katika shule ya sekondari Mabadiliko. Yuko kidato cha pili.

  Shule ya sekondari Mabadiliko imekuwa na uhaba wa walimu. Katika masomo tisa anayosoma Fikiri ni masomo matatu tu yenye walimu, ambayo ni hisabati, jiografia na kiswahili. Masomo haya pia yamepatiwa vitabu vya kutosha kwa sababu rasilimali zote za shule hiyo zinaelekzwa kwenye masomo hayo yenye walimu.

  Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Mabadiliko anategemea mwaka ujao wa fedha walimu watakubali kuja kufundisha shuleni hapo kwa kuwa tarafa yao kwa mara ya kwanza itapata nishati ya umeme. Vilevile tayari kijiji kimeshapatiwa kisima cha maji. Ukosefu wa maji na umeme uliwafanya walimu kukataa kabisa kupangiwa kazi katika shule ya Mabadiliko.

  Fikiri amekuwa akirudia kidato cha pili kwa miaka miwili sasa. Ameshindwa kupata alama za wastani wa kumuwezesha kuingia kidato cha tatu. Wanafunzi wengine wamefanikiwa kupata alama hizo na wanaendelea katika vidato vya juu.

  Wazee wa kijiji wanafahamu kuwa Fikiri hatilii maanani masomo yake. hivyo waliamua kumuweka chini na kumhoji. Alipoulizwa sababu za kushindw kupata wastani wa kuendelea kidato cha tatu, Fikiri alisema kuwa swali hilo linamtia hasira. Amesema hali ya shule yao kukosa walimu kila mtu anaifahamu na kwanini washangae yeye kukosa wastani wa kufaulu. Katika mitihani yake Fikiri hupata F za masomo nane na D ya somo la Kiingereza.

  tangu kipindi hicho Fikiri amejenga chuki na wazee wa kijiji cha Mabadiliko na amekuwa akilaani kitendo chao cha kumuona yeye mzembe wakati wanajua hali ya uhaba wa walimu ilivyo. Fikiri amejitoa katika kushiriki shughuli za maendeleo kijijini na marafiki zake wengi amegombana nao.

  Somo: Pamoja na shule ya mabadiliko kukosa walimu wa masomo mengine, lakini uwepo wa walimu wa Hisabati, jiografia na kiswahili ulipaswa kutumiwa ipasavyo na Fikiri katika kujiendeleza kimasomo na kupata wastani wa kuendelea vidato vya juu.

  Fikiri alitoa kipaumbele zaidi kwenye kulalamikia udhaifu uliopo ambao kwa kiasi kikubwa uko nje ya uwezo wake kuutatua badala ya kuzingatia zaidi nafasi yake katika kutekeleza wajibu wake.

  Je, walimu wa masomo mengine wakiripoti Fikiri atabadilisha tabia yake na kuanza kufanya bidii? au tabia hiyo itakuwa ndio mfumo wake wa maisha na atakachofanya ni kutafuta sababu nyingine ya kulalamika?
   
 2. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Ni darasa nzuri. Ninamuona Fikiri kama mwakilishi wa Watanzania wengi ambao huficha udhaifu wao katika mapungufu ya serikali na nchi.

  Kwa sababu hatuna mfumo wa uwagiliaji maji na vifaa vya kisasa vya kilimo na uvuvi, tunaacha kulima na kuvua kwa kutumia vile tulivyonavyo, badala yake tunakaa vijiweni kukosoa na kusubiri serikali ifanye...ifanye hata kutengeneza madawati na vikalio wakati tumezungukwa na misitu, ifanye hata kufyeka pori, ifanye hata kusafisha uwanja wa nyumba yetu seuze mtaro unaopita kijijini petu.

  Kwa kuwa Fikiri ni mtu wa kusubiri kufanyiwa, ataendelea kulalamika hata baada ya kila kitu kuwepo.
   
 3. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Sawasawa,
  Kwa hiyo in summary tunaweza kusema "if you play your part and I play my part, it can be done". Hakuna viwanda au shule ya viongozi. Viongozi ni miongoni mwa wanajamii. Yale yanayofanywa na mwanajamii leo ndio atakayofanya akiwa kiongozi. je, mwanajamii anaonyesha dalili za kuwa kiongozi mzuri? je, anajali maslahi ya umma kivitendo? Je anatoa taarifa za uhalifu wote anaoushuhudia? Je, ana uchungu na nchi yake? kama mwanajamii wa kawaida hana hivi na jamii inaona hilo ni jambo la kawaida, basi tusitegemee hayo kwa viongozi hata kidogo.
   
 4. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #4
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Tunafanya hivyo kwa sababu viongozi wetu wakati wa kampeni walituahidi kufanya hayo yote. Inshalah sababu tumekwishang'amua tumejirekebisha lakini sio hivi hivi tu. na wao tunawatosa pia.
   
 5. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #5
  Sep 27, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Tatizo letu ni kuwa system tuliyonayo imeoza. Kwa sisi tuliozaliwa na kukulia ndani ya enzi ya ujamaa (pamoja na mapungufu yake) tulikuwa tunagawana umasikini wetu na tunaridhika na tulichonacho, kiasi ikafika wakati kila mwananchi anajiona sehemu ya taifa, analinda mali ya taifa. Ni kweli walikuwepo wakorofi wachache lakini walikwa wanahesabika. Miradi mingi iliyoanzishwa ilikuwa nguvu za wananchi wenyewe kwa hivyo waliitumikia na kuilinda, leo unamhamisha mwananchi kwa nguvu, bila ya kumtafutia pengine wala kumlipa fidia, fedha zilizotengwa kulipia fidia zinaishia mikononi mwa wajanja na wanasiasa walafi, unatarajia wananchi wataulinda mradi huo?

  Lilipokuja suala la kukaza mkanda tulikaza wote, watoto wa viongozi walisoma nchini, baba zao tulikuwa tunapigana na vikumbo kwenye foleni za kilo ya unga na sukari na hospitali, wabunge walikuwa wakienda Dodoma ndani ya basi moja, leo wanadiriki hadi kupanda ndege. Leo hakuna nyongeza ya mshahara wa mwalimu, daktari, polisi, bwanashamba, lakini za kuwaongezea mishahara na posho wabunge pamoja na kuwapa kiinua mgongo cha maisha yao zipo. Leo watoto wao wanasoma nje au kwenye Internationals, wetu wanagaragara kwenye vumbi, wao wakishikwa na homa wanatibiwa nje, sisi tunalala hospitali mpaka kwenye sakafu. Na ndio maana uzalendo umepotea, sasa takriban sote tumekuwa wakorofi kwa sababu mfumo umetufanya tuwe hivyo.

  Mwanajamii anaweza kuwa kiongozi mzuri ikiwa alipata kuongozwa na kiongozi mzuri. Nadra kwa leo kupata kiongozi mzuri kutoka miongoni mwa wanajamii wakati yeye aliongozwa na kiongozi mbinafsi, mhujumu wa mali ya umma na mbinafsi.

  Fikiri ni zao la mfumo wetu, hivyo usitarajie kuwa Fikiri atakuja kuwa kiongozi mwema.
   
 6. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #6
  Sep 27, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Mammamia,
  ninachoona ni jamii kujiadhibu yenyewe.
  Katika saikolojia tunafundishwa jambo likisemwa vizuri, basi huwa linapendwa kufanywa na wengi. Mtoto akisikia kufaulu kunasemwa vizuri basi atajitahidi afaulu.

  Jamii yetu ilikuwa na viongozi wazuri. Lakini kwa vile nchi yenyewe bado uchumi wake unachechemea na mfumo wa mafao uko dhaifu, viongozi hao wazuri walipostaafu hali zao kimaisha zilibadirika na kuishi maisha ya chini. Kukawa na baadhi "wakorofi" ambao walifanya ubadhilifu na walipostaafu wakaendelea kuishi maisha mazuri pengine zaidi ya wakati wakiwa madarakani.

  Wale viongozi waadilifu wanasemwa na jamii kuwa "wamechezea nafasi". na wale wabadhilifu wanapongezwa kuwa "watu wa deal". Juzi ulipotokea msiba wa aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Bagamoyo mama Hawa Ngurume, tuliona watu wakidhihaki hali ya mama yake mzazi kuwa na nyumba inayofanana na wanakijiji wengine. Ilisemwa kuwa mama Ngurume R.I.P amechezea nafasi badala ya kujiimarisha kiuchumi. Kwa anayeifahamu kazi ya ukuu wa wilaya na mafao yake anajua wazi kuwa ukuu wa wilaya haumuwezeshi mtu kuwa tajiri iwapo atakuwa mwadilifu. Kwa hiyo kilichosemwa ni kwamba mama Ngurume amefanya kosa kutokuwa mbadhilifu.

  Hivi ndivyo jamii inavyojiadhibu.

  Kuna wanaoanza kuamini labda kuna chama cha siasa kinaweza kubadilisha hali tuliyo nayo. Lakini sijafanikiwa kumpata mtu anayeelezea jinsi chama cha siasa kinavyoweza kubadilisha hali hii, kwa sababu misingi yake ni kuanzia kwenye familia.
  Kuna vijana wengi nimewakuta Marekani hawataki kujenga nyumbani ingawa wana kipato cha kutosha kujenga na wanapenda kujenga. Sababu wanayonipa ni kwamba experience inaonyesha waliojaribu kujenga wakiwa mbali asilimia kubwa ya pesa walizotuma zilitumiwa tofauti na madhumuni - ufisadi at family level. Hii ndio kama yale masomo ya kiswahili, hisabati na jiografia ambayo Fikiri ana mwalimu lakini anashindwa kujitahidi. Je, at family level nayo tutailaumu serikali? Kama system mbovu at least tujenge jamii ya uaminifu at family level...
   
 7. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #7
  Sep 27, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Ninakubaliana nawe kabisa mkuu katika maelezo yako yote. Ni kweli kuwa mfumo wetu umeharibika katika ngazi zote - kutoka nafsi ya mtu mmoja mmoja, kupitia ndani ya familia hadi kufikia jami kwa jumla. Lakini kusema hivi ni kujumisha wote katika kapu moja wakati bado wapo viongozi wazuri na familia zinazoendelea kuwalea watoto wao kwa maadili. Tatizo ni kuwa hawa wema wazuri wamekuwa kidogo sana kiasi hawaonekani, na pengine hawaaminiwi kuwa wao wameokoka.

  Iko haja ya kurejea katika maadili, kijamii na kitaifa.
   
 8. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #8
  Sep 27, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Tuliiacha misingi ya maadili ya kiafrika bila kujua wapi tunaelekea. Misingi yetu ilijengwa zaidi na nidhamu na ethics. Misingi ya kimagharibi ambayo tunaikumbatia imejengwa na kulindwa na sheria.

  Kwenye familia za kiafrika mtu kumshtaki ndugu yake ni jambo baya sana wakati katika nchi za magharibi ni jambo linalojadilika.

  Nchi za magharibi kabla ya ndoa kutengeneza prenuptual agreement inayoelezea jinsi ya kugawana mali iwapo ndoa itavunjika ni kitu kinachojadilika wakati katika maadili ya kiafrika ni absurd.

  Kwahiyo, jamii za kiafrika ziko katika transition towards western lifestyle na zinajikuta ni "amateur in culture". We dont master any culture at the moment, neither the natural african culture nor the western.

  Jukumu la kuishape jamii liwe zaidi mikononi mwa scholars badala ya kutegemea wanasiasa.
   
 9. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #9
  Sep 28, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  Kwa niliyesoma kwenye mfumo wa Tanzania, nadhani miaka yetu usingeweza kusoma na kufaulu masomo matatu tu na kuendelea na elimu ya juu, kwani kuna hata waliokua wanapata div II ya pt 18 na wakashindwa kuendelea mbele. Pia ili tuwe realistic ni vyema kuchambua story in its whole context... it is very unlikely kwa mtu kusoma masomo matatu tu vizuri kati ya saba na kuendelea, kwenye mazingia yanayoonyesha kupelea kwa basics za education in the named area na bado mtu akatarajiwa kfuanya vizuri

  Anyway, nadhani theme haikua realistic bali kuelezea rage ya aliyekosa kutokana na uhaba

  Si vibaya kujadili kisaikolojia, kijamii na kisayansi pia
   
 10. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #10
  Sep 28, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Mwanafunzi anahitaji wastani wa 21 kwenda kidato cha tatu. Katika masomo tisa ni alama 189. Iwapo mwanafunzi amejitahidi kupata C ya 60 katika masomo matatu, tayari ana alama 180. Kwa hiyo anahitaji alama 2 tu katika masomo mengine kufaulu.
  Wanafunzi wengine wamefaulu, Fikiri amefeli na mwenendo wake unafahamika siyo mzuri.
   
 11. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #11
  Sep 28, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Fikiri angeweza kutumia akili ya udhaifu kuufanya udhaifu wake kuwa tija angefanya la maana sana
   
 12. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #12
  Sep 28, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  huwezi kupasi kurahisi hivyo kama uko kwenye shule uliyozungumzia wewe,..... the scenario you have put, lead to more questions

  Context ndio starting point yako, umeangalia content tu, walimu watatu wapo, maxi av. ni 21 na anapata D moja ya English...

  Typical, typical... typical
   
 13. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #13
  Sep 28, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Wanafunzi wengine wamefaulu...
   
 14. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #14
  Sep 28, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  Its the context that count here... maana mwisho unaweza kuna na kusema ni genetic, babke alikua kiazi sana shule

  kumbuka hii thread ipo kwenye forum ya great thinkers na sio MMU au habari mchanganyiko
   
 15. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #15
  Sep 28, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Naona "Fikiri" wako wengi sana...
   
Loading...