Kisa cha Mtanzania aliyehukumiwa kunyongwa bila kuua

Nashauri kama Kuna wanasheria humu jamii forum au unamjua mwanasheria yoyote kwa umoja wenu muende mukamsaidie huyu bwana kudai fidia, tena fidia ya UHAKIKA, hata zile jumuiya za kimataifa za wanasheria au wanasheria wasio na mipaka tuwatafute wamsaidie huyu bwana
Wanasheria wa Bongo wao wanataka pesa mbele! Hawana akili za kukamata kesi zenye fidia kubwa Kama hizo na ku invest kwanza!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Nimesikia mwanasheria mmoja (nadhani nae ana PhD) akihojiwa na clouds na kusema kufumaniwa na mke wa mtu sio kosa la jinai Ila ukimdhuru mgoni wako una kosa la jinai.

Kwanza nilicheki masikio yangu Kama yako vizuri ndio nikakumbuka Kuna jamaa alifumaniwa na waliomfumania wakamfanya kinyumenyume. Huyo aliyemfumania mwenzake Leo hii Yuko gerezani.

Kumbe ndio maana wachungaji wanajichukulia wake za watu nje nje.

Kumbe Sheria inasema ukimfumania mtu inabidi uwe mpole.
Nimecheka kwa kusikitika sana, hii dunia hakuna haki, wanaotafuta usawa waongeze sauti na kelele, daaa!!
 
Swala la kufumaniana ni la binafsi kati yenu hivyo serikali haihusiki, inabidi mkubaliane tu kulipana fidia au kukabidhiana mke au mume. Hiyo aliyejichukulia uamuzi wa mkimbo kumgegeda mwenzake aliihsmisha kesi toka kwa mtu na mtu kuwa mtu na serikali yaani sasa ni jinai.
Nikikukuta unaiba mapapai yangu shambani nalo Hilo sio suala la serikali inabidi unilipe fidia. SI NDIO??
 
Serekali lazima iwee na utaratibu wa kuwalipa Hawa watu fidia,miaka kumi na mojaa mnampa buku real?

Sent from my TECNO B1p using JamiiForums mobile app
Hiyo buku ni nauli ya kukutoa eneo la gereza uende uendako, ukiwa mjanja unaweza buku ikazalisha zaidi na zaidi mradi tu vidole vyako viwe vyepesi kwenye mlango wa daladala, mjini fomu siksi.
 
Nashauri kama Kuna wanasheria humu jamii forum au unamjua mwanasheria yoyote kwa umoja wenu muende mukamsaidie huyu bwana kudai fidia, tena fidia ya UHAKIKA, hata zile jumuiya za kimataifa za wanasheria au wanasheria wasio na mipaka tuwatafute wamsaidie huyu bwana
Duuuh kabisa aisee
 
Uko sahihi kabisa Mkuu wangu! Jitihada zinahitajika sana ili tumsaidie ndugu yetu huyu!
 
Inauma sana, duniani hapa kuna watu wanapitia shida jamni, just imagine since 1990 mtu yuko gerezani tena kimakosa! Inauma sana lakini kila kitu ni kumuacha Muumba, inauma zaidi unaachiwa huru unakuta dunia inaenda kasi Sana huku kukiwa na janga la virus vya Corona inauma, unakutana na presha zaidi, maisha magumu huna pa kwenda huku umri ukiwa umeyoyoma!!

Mungu AMSAIDIE , naamini kuna kila la kushukuru !!
 
Nimesikia mwanasheria mmoja (nadhani nae ana PhD) akihojiwa na clouds na kusema kufumaniwa na mke wa mtu sio kosa la jinai Ila ukimdhuru mgoni wako una kosa la jinai.

Kwanza nilicheki masikio yangu Kama yako vizuri ndio nikakumbuka Kuna jamaa alifumaniwa na waliomfumania wakamfanya kinyumenyume. Huyo aliyemfumania mwenzake Leo hii Yuko gerezani.

Kumbe ndio maana wachungaji wanajichukulia wake za watu nje nje.

Kumbe Sheria inasema ukimfumania mtu inabidi uwe mpole.
Inategemea. Kuna wanaofumania na kuua mgoni wake lakini wanaachiwa. Kwa mfano wanasema umetoka zako shambani kulima ukasukuma mlango wa chumbani ghafla ukakuta mke wako kitandani na jamaa. Na wewe kwa mshtuko na hasira ukamtandika jembe moja kali sana la kichwani na kuua. Sheria inaweza kukulinda kwani utajitetea uliua kwa hasira na hukuwa na muda wa kufikiri. Kuna kesi nyingi tu za aina hii watu wameachiwa au kufungwa kifungo kifupi sana. Mbaya ni ile inaonyesha kabisa ulikuwa na muda wa kutafakari na pengine ukarudi nje ukachukua silaha ukaanza kumashambulia mpaka akafa. Kinachoangaliwa ni ile hali ya ''premeditation'' isiwepo bali iwe umeua kwa kupoteza uwezo wa kufikiri kwa ajili ya hasira kali. Kuhusu yule aliyemfanya kinyume mgoni wake, ni kweli alifungwa nadhani miaka 30 au maisha (sikumbuki vzr) ila alifanya kosa la kwenda kuanika zile picha kwenye mtandao. Angekuwa ametafuta njemba kimya kimya ikamfanya mgoni wake huku anarekodi (wafunike sura) na yeye asijionyeshe asingepatwa na masaibu hayo. All in all mimi nadhani dawa ni kumtimua mke wako japo wakati mwingine hasir zinakufanya upoteze mwelekeo. Kuna clip moja iko Youtube jamaa fundi umeme huko Arusha kakatwa masikio baada ya kukutwa amebana kwenye michongoma usiku na mke wa mtu. Eti akajitetea alikuwa anamwekeza namna anavyoweza kuwasiliana na Polepole wa CCM amsaidie kupata shule.
 
Polisi na kubambikiana makosa. Hii kada ina laana.
Na sasa serikali imeweka sheria ya kubambikia wananchi wake makosa, kuwasweka ndani, kuwanyima dhamana, ushahidi haukamiliki, kuwanyima raia wake uhuru wa kuishi huru.
Alaaniwe mwanadamu aliyeleta wazo hili!
 
So unampiga Limbwata jamaa aliekua anaiba shambani kwako ili iwe aje Chief?!
You are not paying attention.
Huyu dawa yake Ni usinga. Anaharisha ndani ya masaa matatu anakua Hana maji mwilini. Kibaya zaidi meno yanagandana ili asinywe maji.
Mbondei unamjua au unamsikia?
 
Back
Top Bottom