Kisa cha Mama Panya kinatuhusu Watanzania

Kisa cha Mama Panya kinatuhusu Watanzania

John Manoni

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2020
Posts
611
Reaction score
381
Mama Panya aliona mtego wa panya uliotegwa na binadamu, alisononeka sana kwa sababu ya mtego ule uliokuwa unatishia kuangamiza maisha yake na watoto wake.

Alimfuata Jogoo, akamuomba amsaidie kuutegua ule mtego lakini Jogoo alikataa, alipomfuata mbuzi alimfukuza, akaenda kwa Ng'ombe akamjibu, 'mambo ya mtego wa panya yanakuhusu wewe panya mimi Ng'ombe sina ugomvi na binadamu sasa mtego unanihusu?'

Wote hao hawakujua kwamba, mtego wa panya hunasa waliomo na wasiokuwamo! Mtego ulimnasa Nyoka, naye akamuuma binadamu, ndipo wale wote yalipowafika mauti!

Uchaguzi huu unawahusu walimu, polisi na wafanyakazi wote, unawahusu wakulima na wafanyabiashara, unawahusu wavuvi na wafugaji, unawahusu mijini na vijijini. Hata wanajidanganya kuwa wanalipwa mshahara na CCM unawahusu pia, kwa sababu kila mshahara ni kodi za watanzania.

Mwaka wa 59 wa uhuru bado tunafokewa kunyimwa maji! Bado wanahabari wanatetemeka! Nchi nzima hakuna kusema mfalme yuko uchi eti kwa sababu limejengwa daraja!

Wasalaam.
 
Hiki ndio Kingereza cha hali ya juu kabisa cha anayetaka kutunyima maji kwasababu tumemkataa Silinde
"We suppose to focus according our direction, according our environment, that's only way we can help our peoples. No body should come and say that his there to save the problems of our peoples, we are the one we are leader we suppose to change the direction
 
Back
Top Bottom