Watanzania, Mtego Hunasa Waliomo na Wasiokuwemo!!

Mchokoo

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
1,179
1,579
Baba mwenye nyumba mmoja, aliyechoshwa na panya wasumbufu waliokuwa wakila mahindi ndani storeroom yake; aliamua kwenda katika duka la vifaa vya kilimo ili anunue mtego utakaomsaidia kuwangamiza viumbe hao wadogo. Katika kuhakikisha kuwa nyumba yake inakuwa kwenye hali ya uturivu wakati wote.

Pale sokoni muuza duka alimwonyesha aina mbalimbali za mitego. Karibu kila mtego uliokuwepo pale dukani ulielezewa matumizi yake kwa usahihi mno! Na kwa umakini mkubwa yule baba mwenye nyumba alifanikiwa kuchagua aina mojawapo ya mtego ilikuwa inafaa zaidi.

Ilikuwa ni jioni wakati ambapo yule baba aliporejea taratibu nyumbani kwake, huku fikarani mwake akijua kwamba amepata suruhu ya kero ya mapanya na hasa wakati wa usiku.
Pale nyumbani; mkewe kipenzi, pamoja na wanawe, wote kwa pamoja waliukubali sana ule mtego; kwa namna walivyopata maelezo toka kwa mzee wao kuhusiana na utendaji wa hicho chombo!
Mara baada ya chakula chafamilia kama kawaida; familia ile ilitawanyika kwenda kulala ingawa yule baba yeye alielekea storeroom kwa lengo la kuutega mtego ule.

Akiwa na mtego mkononi yule mzee alitafuta mahali ilipo roundabout (mahali njia nyingi za panya zinapokutania) na polepole alikiweka kifaa hicho cha kufyatu; halafu akanyata kuelekea chumbani kwake huku akisubili kuona kile kitakachotokea.

Baada kitambo kidogo usingizi nao huwa hauna mbabe!!

Pale storeroom panya vijana walikuwa wa kwanza kujimwaga mitaani.

Na kama kawaida yao walianza kuitana kwa mbinja.

Hawa Chuuuuuu!! Wale chuuiiiiii Huku chooooleeeee!!!!!!!
Basi ikawa ni wakati wa panya kujinafasi katika utawala wao huo pendwa.
Hata hivyo kelele hizo zilikata ghafla pale walipoona kitu kigeni kilichokuwa kimewekwa katikati ya roundabout kuu!
Hiki ni kitu gani?
Wengi wao waliuliza kwa mshangao mkubwa!

Na kwa mwendokasi hatari; baadhi ya panya vijana waliwaendea wazee wao na kuwapasha habari juu ya tukio geni lililoikabiri jamii hiyo siku ile , ambapo punde si punde mazee ya panya, tena masomi, ambayo hayana hata muda hata wa kuchana ndevu zao yaliwasiri eneo la tukio pale roundabout.
Ndiposa baada ya kukitazama kile kitu kwa umakini mkubwa, iliamriwa kwamba kutokana na dharura ile kuu; panya wote waitwe kwenye ukumbi mkuu wa mikutano ya kitaifa kwa ajili ya kusomewa ripoti ya kitaalamu kuhusiana na kitu kile kilichopo pale roundabout.

Wakati mwenyekiti wa panya taifa akimkaribisha prof chisweswereiii asome ripoti hiyo maalum, ukumbi ulikuwa ulikuwa umetapika! Haijapata kutokea!!
Kwa sauti isiyo na bashasha kama isivyo kawaida yake Prof Chisweswereiii alianza kuisoma ripoti aliyoandaliwa na jopo la mapanya wataalamu, akasema:
Ndugu Mwenyekiti, ndugu katibu mkuu, ndugu spika wa bunge la jamhuri ya panya, wakuu wa usalama wa panya, viongozi wote, mabibi na mabwana; itifaki imezingatiwa.

Leo taifa letu limevamiwa, profesa alisisitiza huku akikatizwa na miguno ya mshangao kutoka kwa hadhira ile iliyokuwa na hamu ya kutaka kujua ukweli wa jambo lile. Baada ya kumeza mate huku sharubu zikimcheza profesa aliendelea kusema; ndugu zangu, pengine kwa ufupi sana ili nimrudishie mwenyekiti; ni kwamba, sisi wataalamu tumegundua kuwa kile kitu kilichopo katika makutano makuu ya barabara zetu kinaitwa mtego!
Hiki ni kifaa hatari sana kilichowahi kuleta madhara makubwa katika nchi za majirani zetu.
Ule mtego pale ulipo unasubiri mguso wa kitu chochote ufyatuke!!
Hati hivyo kutokana na elimu kubwa inayotolewa katika kitivo cha mitego chuo Kikuu cha panya kuhusiana na mambo ya mitego kwa aina zake; jamii yetu haiwezi kunasa kijinga katika mtego kama huu.
Sasa basi pamoja na mengi mazuri katika kuripatia suruhu jambo hili, kwa pamoja, sisi jopo la wataalamu tunashauri kwamba ili jamii yetu iwe salama kwanza ni lazima mtego huu uteguliwe.
Ukumbi mzima unalipuka kwa shangwe na makofi: waa! waa! waa
Ndugu Mwenyekiti, naomba kuwasirisha alimaliza pro kisweswereiii.
Tena, jamii yote inapiga makerere kwa sauti! uteguliwe, uteguliwe!
Ndipo sasa baada ya mashauriano marefu mkutano uliazimia kuwa kwa kuwa miguu ya panya haina nguvu za kukabiliana na mfyatuko wa ule mtego basi ni bora wamwendee jirani yao kuku aliyekuwa amelala bandani katika mji ule-ule ili yeye aje awasaidie kuupiga teke mtego ule ili ufyatuke bila kusababisha madhara yoyote!
Wale wajumbe wa panya walipofika kwa jogoo hali haikuwa kama walivyotegemea!
Kwani mr jogoo aliwalaumu sana wale panya kwa kumuharibia usingizi wake na eti kwamba
matatizo ya panya kuperekwa kwa kuku wapi na wapi? alilalama yule jogoo!
Taarifa hii mbaya ilirudishwa haraka pale mkutanoni, ambapo wajumbe waliambiwa kwamba; jogoo amekataa ombi la mkutano mkuu wa panya, kwa madai kuwa eti mambo ya panya huwa hayawahusu kuku.
Hata hivyo uma ule haukukata tamaa kwani sasa ilipendekezwa kuwa wakamwone kondoo aliyekuwa mkazi mwenzao katika mji huo.

Cha kusikitisha ni kuwa majibu ya kondooo hayakuwa tofauti sana na yale ya jogoo, hata hivyo kondoo yeye alienda mbali zaidi pale alipowatishia panya kuwa; wakiona anarudi nyuma wasifikiri ameshindwa!! akirudi pale walipo wawe wamepotea haraka!
Wapuuzi wakubwa nyie! mimi niache usingizi wangu kwa sababu ya mtego mliotegwa nyinyi.
Kwendeni zenu kwani mimi ndio nimewatuma muwe na kawaida ya kula mahindi ya watu? Kondoo alimaka kwa sauti kali.

Hatimae panya wale walienda kumwangukia jirani yao mwingine aitwae ngombe, wakidhania kuwa ukubwa wake wa umbo pengine unaweza kuwa na hekima zaidi katika kulitazama suala lile tete. Kwa ufupi ni kwamba ngombe pia alikataa katakata kuambatana na shauri la panya, huku akisisitiza kuwa wanyama hao wadogo hawawezi kumsumbua yeye kiasi hicho! Huu ni utovu wa nidhamu uliovuka mipaka yake!!
Mimi niwasaidie nyinyi kutegua mtego wenu, ninyi mtakuja kunisaidia mimi nini katika maisha haya? Aliuliza ngombe kwa msisitizo.

Kwa masikitiko makubwa mwenyekiti wa panya taifa alitangaza hali ya hatari iliyomzuia panya yeyote kutoka nje ya nyumba yake mpaka swala hilo litakapotafutiwa ufumbuzi wake kwa njia nyingine!
Alifunga mkutano na kuwataka panya wote warudi majumbaji mwao huku akiwakumbusha kuliombea jambo lile!
Kitambo kidogo, mara baada ya panya wote kuvirejea vitanda vyao; yule baba mwenye nyumba alistushwa na sauti ya kishindo, akakumbuka kuhusu ule mtego wake. Akajiinua taratibu kutoka kitandani ili akamwondoe panya aliyenasa kisha atege tena!
Alipofika pale storeroom alipouweka mtego aliinama ili auchukue, loh! masikini, kwa ghafla aling'atwa na kitu mkononi, kutaharuki kumbe joka mkubwa mwenge hasira ya kubanwa na mtego aliyekuwa akijitupa huku na kule! Baada ya kuona hivyo yule baba alipiga kelele za kuomba msaada ingawa hata hivyo baada ya muda mfupi tu alipoteza fahamu na kulifariki dunia kwa sababu yule nyoka aliyemuuma alikuwa na sumu kali.

Ilikuwa ni huzuni kubwa kwa familia ile, ndugu, jamaa na marafiki.
Vilio vilitawala kila kona ya kijiji kile.

Na kulipopambazuka tu kilihitajika chakula kwa ajiri ya waombolezaji.
Ndipo walipotumwa vijana ili wamkamate yule jogoo kabla hajatoka bandani mwake!
Ni yule yule aliyeyesema kuwa mambo ya panya hayamhusu!
Maskini jogoo, taratibu kijana mwenye kisu alimnyoonyoa manyoya shingoni mwake!
Mwee!! mwee! mwee! Aliomboleza jogoo pasipo msaada wowote!
Hatimae kichwa chake kilitenganishwa na shingo yake! Siku hiyo ikapita!

Keshoe waombolezahi walikuwa wengi zaidi ambapo pia walihitaji chakula.
Safari hii familia ilimtoa kondoo, ni yule aliyetaka kuwapiga panya wakati walipokwenda kumsihi autegue mtego ule!
Maskini naye pia kama kuku walikiondoa kichwa chake na kuishia kuwa kitoeo cha waombolezaji siku ile.

Siku ya tatu ndiyo ilikuwa siku ya mazishi, na kwa sababu marehemu alikuwa ni mtu maarufu; kulikuwa na uma mkuu wa waombolezaji!
Na kama kawaida wote hawa walihitaji chakula cha mchana huo, hivyo iliamuriwa kuwa achinjwe yule ng'ombe mkubwa, ni yule yule aliyewaambia panya kwamba yeye akitegua mtego ule wao watamfaa kwa lipi hapa duniani?
Moooo! Moooo! Mooooo! Moooooo! Masikini ng'ombe alilalamika, ingawa vijana wachinjaji tena wenye uchu wa nyama hawakujari kitu! Chinjilia mbali, ng'ombe alipoteza uhai wake!
Ndugu yangu msomaji sote tunajifunza nini kupitia kisa hiki cha kusikitisha?

Yule baba, yule Jogoo, yule kondoo na yule ng'ombe wote hawakuwa walengwa wa mtegaji wa mtego! Hata hivyo bila kujali tofauti zao za kibaolojia wote walikuwa wahanga wa mtego ule!

Kudhani kwao kuwa hawahusiki hakukuwafanya kweli wasihusike!
Naam!
Wote waliangamia, mmoja baada ya mwingine, huku wale waliolengwa wenyewe wakiwachungulia kutoka mashimoni mwao kwa masikitiko!
Na kilichonishangaza zaidi kwenye mkasa huu ni yule marehemu baba mwenye nyumba!!!!
Eti kumbe ule mtego wake alioununua ili awatege panya kumbe alikuwa anayatega maisha yake mwenyewe, ingawa aliyenasa ni mwanzini ni nyoka ambaye kiuhalisia hakuwa mlengwa wa mtego wenyewe!

Ama kweli mtego hunasa waliomo na wasio kuwemo!
 
Hii ni falsafa kubwa sana muda ukifika nitaitafsiri
 
Acha ujinga kila siku mnaandika Makala.. Andamaneni acheni kutishia tishia... Kila siku makala mnatuchosha ingieni mtaani..
 
Back
Top Bottom