Kisa cha Malkia na Mafisadi wa CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kisa cha Malkia na Mafisadi wa CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Akami, Oct 5, 2009.

 1. Akami

  Akami Member

  #1
  Oct 5, 2009
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katika maandiko matakatifu (Biblia) tunaambiwa kuwa kulikuwa na malkia(mke wa mfalme),mzuri sana,mwenye kila sifa ya uzuri na mwenye tabia nzuri sana kwa watu na kwa mfalme pia.Uzuri wake huu ulisababisha wazee wawili miongoni mwa watumishi wa mfalme kumtamani na kutamani kufanya nae tendo la ndoa.Basi ili kufanikisha azma yao hiyo,wakamtegea anaoga bustanini kwa mfalme na wakamwambia kuwa hasipokubaliana nao,watapiga kelele kuwa wamemfumania na kijana mmoja ambaye katika purukushani za kumkamata amewatoroka.

  Basi Malkia kwa kuwa alimcha Mungu na kumtii mume wake ipasavyo,akakataa na wale wazee wakapiga kelele kweli kwamba wamemfumania malkia wao akizini na kijana ambaye amefanikiwa kutoroka.

  Hivyo basi kesi ikasikilizwa mbele ya jopo la viongozi akiwapo mfalme mwenyewe,lakini kutokana na Busara za mtumishi wa Mungu Daniel,wakaweza kuwabaini wale wazee kuwa ni waongo walimsingizia malkia kwa ajili ya tamaa zao za mwili.na kweli wale wazee wakakili kusema uongo na wakahukumiwa kunyongwa kama ilivyokuwa sheria yao,malkia akawa huru.

  Sasa basi kilichotokea baada ya hukumu hiyo,mfalme akasimama na akamshukuru malkia kwa kutoitia aibu familia ya kifalme lakini akaongeza kuwa,ingawa imethibitishwa pasipo shaka kuwa umesingiziwa,lakini kitendo chako cha KUTUHUMIWA tu kinakuondolea sifa ya kuwa Malkia(mke wa mfalme).Hivyo kuanzia sasa wewe si mke tena wa mfalme.

  Tumesikia tuhuma nyingi sana za viongozi na wengine wanachama wa CCM kuhusu rushwa na UFISADI,viongozi wengi san wametuhumiwa,wengine kesi ziko mahakamani,na wengine,labda ndo wamekishikilia chama maana hata haijulikani ni lini nao watafikishwa kwa pilato.Katika sijui znaitwaje zile za CCM kuna moja inasema RUSHWA NI ADUI WA HAKI,SITATOA WALA KUPOKEA RUSHWA''

  Sasa jamani tuhuma hizi zimekuwa nyingi na hazivumiliki kwa kweli,kwa nini wewe tu Rostam wala hasituhumiwe mwingine?Kwa nini wewe Ben,kwa nini wewe Kagoda,kwa nini wewe Chenge?

  Wakati wa kumuiga mfalme na hukumu yake umefika sasa ndo huu,Mheshimiwa Ben,Rostam,Chenge,Lowassa,Mramba n.k,kitendo tu cha kutuhumiwa kuhusika na rushwa kinawaondolea sifa ya kuwa wanachama wa chama chetu safi cha CCM,hivyo kuanzia sasa tunawavua uanachama wa CCM,anzisheni chama chenu cha mafisadi huko tutakisajili.

  CCM mkifanya hivyo mtakuwa mmewatendea haki watanzania walionyonywa na hiyo mifisadi(samahani kwa lugha mbaya,wanakera),ningekuwa hakimu ningesema wafungiwe mawe ya kusagia mashingoni mwao na watupwe baharini!,Watoto wangapi wanakufa mahospitalini kwa kukosa huduma,wanafunzi wangappi vyuoni wamefukuzwa kwa kukosa ada wakati nyie mnajilimbikizia mali kwa kuwaibia?Alafu jitu linsimama na kusema 25bilioni ni vijesenti!Wakati kuna wazazi wameshindwa kulipa hata ada sh 20000 tu za watoto wao,watoto wako wanahangaika wamegeuka ombaomaba na machangudoa mitaani!
   
  Last edited: Oct 5, 2009
 2. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kwa sasa tunaishi katika utawala wa sheria. Na huwezi kumwambia mtu ondoka kwa sababu ya shutuma. Dawa ya kuwamaliza ni kuweka evidence wazi. Tatizo ni kwamba evidence inawa-impliment wote. Na ndio maana imefichwa! Wewe unadhani leo ikateremshwa dili nzima ya EPA, Kikwete atapona? CCM itabaki na kina nani?
  Katika kuiweka sawa na mfano wako wa malkia - ni sawa na huyo mfalme kuwa alikula hiyo njama na hao wazee. Unadhani mfalme angekubali siri itoke?...hahahaha
  Ndo maana...dawa imebaki moja tu....
  kuiondoa CCM.
   
 3. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ufisadi+CCM+Umaskini+Mikataba feki+ Elimu duni+ wizi wa mali za umma+Tanzania=TANZANIA. Kweli tuna kazi kubwa sana katika mambo ya msingi katika Taifa letu
   
 4. Mwana va Mutwa

  Mwana va Mutwa JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2009
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 429
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  labda wakuu bado wanasubiri uchunguzi ufanyike kwanza kama ambavyo mfalme alisubiri uchunguzi kwa malkia uishe na kumtoa kwenye nafasi yake
   
 5. Akami

  Akami Member

  #5
  Oct 8, 2009
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mmhh Ndugu yangu Mtoto inaonekana epeo wako wa kuelewa mambo uko juu sana,nimeapreciate,kwamba inawezekana mfalme alikula dili na wale jamaa ili siri isitoke nje!GREAT THINKERS!

  Sasa why JK asile dili na mahakimu wakakayatosa hayo majamaa?
  Unajua ukiangalia zile picha za watoto wa shule za Mbagala,mpaka ndugu yetu Ngida anataka kujitoa JF zinauma!

  Nani sasa wa kumfunga paka kengele?
   
 6. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #6
  Oct 9, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Jk akila dili na mahakimu atakuwa ameua system nzima ya separation of power na uaminifu wa wananchi katika utendaji wa mahakama. Hivyo kama anataka kuleta mabadiliko ya kweli, ajitoe muhanga na kukubali kufa kisiasi kwa kuleta uwazi wa kweli. Yani aseme "kama siri zangu zitatoka na kunidhuru kisiasi, nakubali, but all for the good of my beloved country Tanzania." Maana kusema kweli, viongozi wote wa CCM walio juu wamekula ma-deal in one way or another. Kwa wale ambao hawajala - mfano Pinda, hawawezi kuleta mabadiliko maana waliowazunguka wameoza. Hivyo solution ni mbili:
  1) Mmoja ajitoe muhanga ndani ya CCM; au
  2) tuchague Chama kipya cha kutuongoza.
   
Loading...