Jokate Mwegelo kutembelea Songwe 11.11.2023, UWT yamuandalia mapokezi kama Malkia

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,315
9,743
Ndugu zangu Watanzania,

Songwe kumekucha ,Mbozi ni Kishindoo na shamrashamra,Mlowo ni hekaheka na mshike mshike juu ya mapokezi makubwa na ya kipekee kabisa kuwahi kutokea Nchini Tanzania katika ujio wa katibu mkuu wa UWT Taifa ndugu jokate Mwegelo atakapotua katika mji mdogo wa Mlowo wilaya ya Mbozi mkoa wa Songwe atakapokutana na kuzungumza na maelfu ya wana songwe.

Kila sehemu unakopita ni gumzo juu ya ujio wa ugeni huo mzito kabisa kutoka ngazi ya juu kabisa. Akina mama wa UWT wanaendelea na maandalizi makubwa na kabambe katika mapokezi ya katibu mkuu wake.nyuso za akina mama zimejaa tabasamu , Furaha, matumaini,upendo, ukarimu na shauku kubwa ya kumpokea katibu mkuu UWT Taifa.

Ambaye ndiye mtenda mkuu anayeongoza jeshi la akina mama ambalo ndio jeshi kubwa na imara kabisa na tegemeo kwa CCM na Ambalo limethibitishwa kuwa ndio jeshi bora kabisa Barani Afrika na Dunia nzima kwa ujumla wake ,ambalo pia limeapa kiapo cha uaminifu kuwa iwe jua, iwe mvua,iwe usiku iwe mchana litapita nyumba kwa nyumba ,kijiwe kwa kijiwe kumtafutia na kumuombea Rais samia kura za ndio kwa kishindo,ni jeshi ambalo limejipanga kwa zana zote na kukamilika kila idara na kusubiri tu wakati ufike liingie vitani na kumaliza vita asubuhi na mapema kwa kumpeleka Rais Samia ikulu likiwa limembeba katika mabega yake kwa mwendo wa Madaha na ujasiri.

Kulingana na maandalizi yanayoendelea na shauku kubwa iliyopo mkoani Songwe juu ya ujio wa ugeni huo,inatabiliwa na kutegemewa kuwa mapokezi hayo yatakuwa kama yale afanyiwayo na kuandaliwa malkia atembeleapo na kufika sehemu fulani,kama ilivyokuwa kwa malkia Elizabeth wa Uingereza

Kaeni kwa kutulia na kuendelea kufuatilia huku mkitega masikio na kuelekeza macho na masikio yenu mkoani Songwe kuona kishindo cha wana songwe na namna walivyodhamiria kutuma ujumbe wao Tanzania nzima kuwa Rais samia ndiye chaguo lao Uchaguzi ujao na kwamba hazuiliki katika kupeperusha Bendera ya CCM Katika nafasi ya Urais.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Makelele mengi hakuna la maana. Serikali nzima imeshindwa kujua nani mmiliki wa KADCO. Leteni mambo ya maana.
econonist uwe na moyo wa shukurani hata chembe. Unaanzia wapi kusema hakuna la maana wakati unaona maendeleo na miradi ya maendeleo na kimkakati ikichipua kila sehemu? Jiulize tulipokuwa tunapata uhuru tulikuwa na km ngapi za barabara za lami na leo zipo ngapi? Mtandao wa barabara za lami mkoa kwa mkoa na wilaya kwa wilaya ilikuwaje wakati tunapata uhuru na leo hali ipoje? Huoni kwa sasa barabara za lami zipo kila mkoa na kila wilaya?vipi hali ya elimu na afya? Tulikuwa na shule ngapi za sekondari wakati tunapata uhuru na leo zipo ngapi? Tulikuwa na vyuo vikuu vingapi na leo tunavyo vingapi? Vipi kuhusu hali ya umeme ilikuwaje wakati tunapata uhuru? Mikoa mingapi haikuwa na umeme na leo mingapi haina umeme? Huoni umeme kwa sasa umefika kila mahali?
 
Ndugu zangu Watanzania,

Songwe kumekucha ,Mbozi ni Kishindoo na shamrashamra,Mlowo ni hekaheka na mshike mshike juu ya mapokezi makubwa na ya kipekee kabisa kuwahi kutokea Nchini Tanzania katika ujio wa katibu mkuu wa UWT Taifa ndugu jokate Mwegelo atakapotua katika mji mdogo wa Mlowo wilaya ya Mbozi mkoa wa Songwe atakapokutana na kuzungumza na maelfu ya wana songwe .

Kila sehemu unakopita ni gumzo juu ya ujio wa ugeni huo mzito kabisa kutoka ngazi ya juu kabisa. Akina mama wa UWT wanaendelea na maandalizi makubwa na kabambe katika mapokezi ya katibu mkuu wake.nyuso za akina mama zimejaa tabasamu , Furaha, matumaini,upendo, ukarimu na shauku kubwa ya kumpokea katibu mkuu UWT Taifa .

Ambaye ndiye mtenda mkuu anayeongoza jeshi la akina mama ambalo ndio jeshi kubwa na imara kabisa na tegemeo kwa CCM na Ambalo limethibitishwa kuwa ndio jeshi bora kabisa Barani Afrika na Dunia nzima kwa ujumla wake ,ambalo pia limeapa kiapo cha uaminifu kuwa iwe jua, iwe mvua,iwe usiku iwe mchana litapita nyumba kwa nyumba ,kijiwe kwa kijiwe kumtafutia na kumuombea Rais samia kura za ndio kwa kishindo,ni jeshi ambalo limejipanga kwa zana zote na kukamilika kila idara na kusubiri tu wakati ufike liingie vitani na kumaliza vita asubuhi na mapema kwa kumpeleka Rais Samia ikulu likiwa limembeba katika mabega yake kwa mwendo wa Madaha na ujasiri.

Kulingana na maandalizi yanayoendelea na shauku kubwa iliyopo mkoani Songwe juu ya ujio wa ugeni huo,inatabiliwa na kutegemewa kuwa mapokezi hayo yatakuwa kama yale afanyiwayo na kuandaliwa malkia atembeleapo na kufika sehemu fulani,kama ilivyokuwa kwa malkia Elizabeth wa Uingereza

Kaeni kwa kutulia na kuendelea kufuatilia huku mkitega masikio na kuelekeza macho na masikio yenu mkoani Songwe kuona kishindo cha wana songwe na namna walivyodhamiria kutuma ujumbe wao Tanzania nzima kuwa Rais samia ndiye chaguo lao Uchaguzi ujao na kwamba hazuiliki katika kupeperusha Bendera ya CCM Katika nafasi ya Urais .

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Huyu mtoto nyota yake inang'aa sana.Nadhani ni suala la muda tu atakuja kuishtua Tanzania.
 
Huyu mtoto nyota yake inang'aa sana.Nadhani ni suala la muda tu atakuja kuishtua Tanzania.
Naunga mkono hoja, mimi nilishaandika humu jukwaani kabla hata hajateuliwa katika nafasi hii ya sasa kuwa uchaguzi ujao lazima atinge bungeni.mpaka hapa tayari ni mbunge ambaye 2025 anakwenda kuingia bungeni.ni mfano wa kuigwa kwa mabinti na wasichana wengi .kupitia yeye mabinti wengi sana wataongeza bidii katika masomo yao ili kuzifikia ndoto zao.
 
Back
Top Bottom