Kisa cha kweli: Mama wakwe wengine pasua kichwa

Kisa cha kweli: Mama wakwe wengine pasua kichwa

Mima white cute

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2017
Posts
740
Reaction score
1,305
Ni kisa cha ukweli kabisa na hii ndoa sasa IPO mashakani.Hivi nachokifanya huyu mkwe ni sawa au yupo nje maadili.

Ni hivi huyu mama ana mtoto wa kiume ambae ameoa mwaka 2005 katika miaka ya elfu mbili na kumi mke huyu jamaa alipata mtihani wa maradhi ambayo aliumwa kwa muda wa miaka mwili.KAma unavyojua mwanaume akawa anachepuka pembeni mpaka akamtia mimba mwanamke mwingine na wakazaa mtoto wakiume muda huo alishazaa na mkewe mtoto mmoja na hawakuwa wameachana isipokuwa mke alikuwa anatibiwa maradhi yaliuyokuwa yanamsumbua ya kiswahili.MW mungu akajaalia mke akapona.

Sasa hapa utata uliokuwepo ndugu wa mume wanamsema huyu Dada kwa nini anakataa kulea mtoto wa mumewe na anashutumiwa ana roho mbaya sana.Jamanii hivi kweli ni sawa mwanaume kukuletea mtoto aliyakuwa mpo wote hamjaachana ila yeye kachepuka ni sawa kweli kwa nini huyo mtoto asilelewe na mama yake.yote tisa kumi

Huyu mkwe amejifanya kwenda kumchukua yule mtoto kinguvu ili tu amkomeshe mke wa mwanae amlee yule mtoto.baada ya kuona yule Dada amemkataa mama mkwe kwa vishindo akajifanya kumng'ang'ania yule mtoto amlee yeye eti na unataka yule mke wa mwanae kila wiki akamfulie yule mtoto.

Na anachokifanya anamtumia huyu mwanamke aliyezaa na mwanae kumrusha roho mke wa mtoto wake.basi neno si neno kapigiwa simu huku ukweni kwa sababu kazaa na mwanae.

Wiki kazaa zilizopi eti kapigiwa simu mtoto wake kamaliza chekechea wafanye sherehe alafu mkwe ndio yupo Benet na yule aliyezaa namwanae.DAda wa watu uvumilivu umemshinda ilibidi aulize kwani mama dhamira yako nini kwa hayo unayoyafanya au ndio unaamua kumletea mwanao mke wa pili..mama wacha ajilize katukanwaaa..basi mume wa mtu alivyoambiwa na mama yake mkeo kanitukana karudi kwake kafura na talaka kaandika tayari lakini bado anatembea nayo tu mfukoniii😀😀😀 bado ajamkabidhi anatishia kumuacha.

Hivi wiki sasa inafika nyumba yao aina amani kila MTU anaishi kimpango wake ..kwa sababu ya fitna za huyu mama mkwe..

Sasa najiuliza maswali haya

1 Haoni alipokosea mwanae kwenda kuchepuka mpaka kuleta mtoto akiwa na mke tayari

2 Na kama kosa lishatokea tayari kwa nini amkumbatie hivyo huyo mwamke aliyedhini na mwanae .kama kweli lengo mjukuu wake kwa nini asiendelee kukaa na mjukuu wake bila kuleta mbwembwe zote hizo

Tena huyu mama mkwe wa huyu Dada mume wake miaka ya nyuma alichepuka pia kaja kujua mtoto wa mumewe amekuja akiwa binti wa miaka 25 mkubwa mzima na chozi lilimtoka kwa nini mumewe alichepuka iweje unaona kitu nahisi kwa mwenzie kama yeye MTU mzima nauvumilivu ulimshinda.

OK nisiwachoshe hivi kwa upande wenu mnamchukuliaje mama mkwe wa aina hiii.
 
Kwanza pole kwa mhusika wa hiki kisa

Ujue maisha yana mengi na katika mengi lazima uvumilivu uwepo

Swala la kulea mtoto wa mwingne inabidi akubali maana wakati mwingine ili kuweka mazingira ya kipato sehemu moja akikataa inaweza ikawa mwanaume anatoa garama za malezi ambazo zilipaswa ziliwekwe sehemu moja
 
Kuna kitu kinaitwa Karma... Huyo mwanaume na mama yake siku moja karma itawatafuna...

Huyu mdada anaefanyiwa haya kwanini asiondoke kwao?
A nawaza watoto wake kwani sasa tayari na yeye ana watoto wa tatu.....ila Mimi kwa ujeuri wangu ningeondoka tu
 
Kwanza pole kwa mhusika wa hiki kisa

Ujue maisha yana mengi na katika mengi lazima uvumilivu uwepo

Swala la kulea mtoto wa mwingne inabidi akubali maana wakati mwingine ili kuweka mazingira ya kipato sehemu moja akikataa inaweza ikawa mwanaume anatoa garama za malezi ambazo zilipaswa ziliwekwe sehemu moja
weeee usifanye utani na kuletewa mtoto ukiwa upo kwenye ndoa bola Mara mia umkute nae...Mimi siwezi binafsi na sina moyo huo nikimkuta sawa ....yahni Mimi Nike kuhudumia mtoto kumfulia kumfanyia kila kitu alafu wamenifanyia usaliti.....Tena Mara mia aje akiwa na akili zake timamu anaweza kufanya kila kitu
 
Mkuu kumbuka uchumi wa familia hukaa sawa pale ambapo familia iko sehemu moja ukiruhusu akatoe matumizi huko jiandae kuletewa watoto zaidi ya huyo

Hapo unapaswa kusamehe na kuruhusu maisha yaendelee
 
Kiumbe mwanamke ni kidhaifu sana.Na hawa wake zetu ni mama wakwee wa baadae.

Let us keep watching
 
Mkuu kumbuka uchumi wa familia hukaa sawa pale ambapo familia iko sehemu moja ukiruhusu akatoe matumizi huko jiandae kuletewa watoto zaidi ya huyo

Hapo unapaswa kusamehe na kuruhusu maisha yaendelee
Na imekaaje wanakuletea mtoto kulea alafu wao wana endelea kufanya yao kimya kimya
 
Back
Top Bottom