Kisa cha Kweli: Hawara alivyonifilisi

Status
Not open for further replies.

Elisha2004

JF-Expert Member
Feb 21, 2020
489
560
Huenda nikaokoa mtu humu au popote pale utapokisoma kisa hiki.

Umofia kwenu,
Story yenyewe iko hivi, mwaka 2012 takriban miaka minne baada ya kufunga ndoa na mke wangu kipenzi nilijikuta nikiwa nimeingia kwenye mahusiano na mwanamke ambaye tulikutana kwenye mojawapo ya Social Media maarufu sana hapa Bogoland.

Mahusiano yetu yalianza baada ya kujikuta tunashea same experience ya kwenye ndoa ambapo alisema mumewe hamridhishi kimapenzi na mimi nikatoa sababu za uongo ili kupata penzi lake.

Tulijikuta tumezama kwenye mahaba mazito, hatukuwahi kupima wala kutumia kondomu. Tulijiamini, mapenzi yakawa mubashara. Yeye aliishi mkoa wa jirani na hapa kwa hiyo mara nyingi alitunga uongo kwa mumewe ilimradi atoke tuonane.

Makutano yeti yalikuwa Chalinze zaidi maana tuliamini hakuna mtu angetufahamu. Hapa mapenzi yalizidisha utamu, mke wa mtu ni mtamu ndugu zangu. Kuna siku wifi yake alimuona Chalinze akamshtaki kwa mumewe alipigwa sana lakini hakujali kabisa.

Sikumbuki kama kuna staili ya mapenzi hatukufanyanga! Tulifurahi sana.

Baada ya mapenzi kunoga hasa zile safari za Serikali nilizokuwa nakwenda nae tuliamua sasa tuanzishe na miradi tupate kipato.

Kwakuwa nilikuwa kazini bado niliweza kuchukua mkopo nikampatia kwa maana ya kuanzisha biashara ili tupate kipato, mambo yalienda vizuri lakini sababu tulikuwa mikoa tofauti changamoto zikaanza kujitokeza. Ikabidi tufunge biashara yetu na mimi niendelee na kulipa deni la mkopo ambao pesa yenyewe haipo tena. Niliumia sana lakini sikutaka kumuonyesha kuwa nimeumia. Likapita hili.

Kuna nyakati niliiacha familia yangu bila chakula na pesa kumpatia huyu Mama ili afurahi tu. Ndugu zangu nilibeba mzigo mkubwa sana ambao sikuweza kumwambia mtu yeyote yule. Dhambi inaumiza sana. Uzinzi ni mbaya sana. Nilipomaliza deni nikasema napumua sasa, kumbe ndio ilianza tena!

Siku moja asubuhi akaniambia binti zake hawajaenda school. Hawana fees, nikakopa nikatuma. Naumia kwa machungu haya. Hili likawa chanzo cha kudumbukia kwenye madeni makubwa ili kumridhisha tu. Natamani ningeishi na mke wangu tu.

Don't make a promise you can't fulfill...

Kwahiyo nikajikuta kwenye mideni isiyolipika, nyumbani kukawa hakuna amani kiukweli sasa, kila siku watoto wanarudishwa ada.

Tukaanzisha mradi mwingine wa mgahawa na kwakuwa yeye hakuwa mwajiriwa akautaka sana huo mradi. Basi ndugu zangu, nikakopa nikampatia pesa yote.

Nasikia siku moja mumewe alimkuta na wanaume wengine hapo mgahawani akafanya vurugu sana akamkataza asifanye hiyo biashara tena kuwa ni malaya.

Hapo napo kale kahela kote kakateketeamo humo nikalipa pesa ambayo haikurudi tena.

Cha kunishangazaga mwenzangu hakuwahi kuchangia hata kufuli la mlango tu. Nikajikuta nimebeba mzigo mzito sana na siwezi kumwambia MTU, nikaanza kuisha kwa mawazo.

Kwa bahati mbaya mwaka 2016 nikaachishwa kazi! Maisha yakawa magumu vibaya sana ila Hawara sikumwacha; safari zikaisha starehe zikapungua ndio SMS za dhihaka na kebehi zikaanza toka kwa huyu mtu.

Nakumbuka siku moja alikuja na wazo la biashara flani hivi ambayo mtaji wake ulikuwa zaidi ya 10m huko nyanda za juu. Kwakuwa sikutaka kumuudhi niliamua kuuza kiwanja chetu baada ya kumshawishi mke wangu akakubali kwa shingo upande akiamini naenda kutafuta pesa. Pesa yote nikampatia na haikurudi hata thumni.

Ni kidada kilevi sana, ukikaa nacho kinapigiwa simu na wanaume tu! Kwa ujumla tulifanya project kadhaa hakuna hata moja iliyofanikiwa.

Nina maumivu makali sana moyoni mwangu! Naandika huku machozi yanatoka. Vijana jifunzeni kuepuka tamaa!

Huyu Mama hadi leo yupo kwenye mitandao akiendelea kujifanya ni superwoman anajua miradi na kwamba ni mpiganaji.

Naomba nifupishe nashindwa kuandika, kwa ufupi niliuza kiwanja, gari mbili, kijishamba changu, baadhi ya vifaa vya ndani.

Baada ya madhira yote haya na aibu, nikamtafuta auntie ikabidi aniunganishage na kiongozi wa dini, simfahamu ila niliongea nae kwa kirefu alinisaidia sana kiroho. Najuta kuhalibu familia yangu kwa starehe za muda.

Nakaribisha mtu mwenye maswali...
 
WaTanzania mna shida san,badala ya kumfundisha kua maneno fulani kama hili au lile ungeweka R na si L,nyie ni kukashifu tu na si kumsaidia mwandishi, waafrika tuna kwama sana,ujuaji mwingi usio na manufaa
Uandishi mmbovu sana kuwahi kutokea ulimwengu huu wa tatu, kwenye r" unaweka L" na kwenye L" unaweka R.

Sent using Jamii Forums mobile app

JAH Rastafari Morning Africa.Trust JAH respect nature
 
Mi mwenyewe nili tembea na mke wa mtu mapenzi yalikuwa moto moto sana kuliko hata mchumba wangu.

Nashukuru nilihamia sehemu nyingine la sivyo mingefumania siku moja maana ilikuwa balaa.
 
Ndio maana mm huwa nataman maswaiba yote hayo na mengine ya mapenz mtu apitie mapema before 30 yrs. ili akifika 30 ajue anataka mtu wa namna gan na ajenge vipi familia.

Pole Sana Kaka.
Huo msemo wako pia umechangia kuwa poyoyo.

Kwa baadhi ya Wanawake weka promise na ukishagonga, dont fulfill..



Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Huo ni ukichaa..hakuna mapenzi ya namna hio!! Labda tuu alikuwa anakupa kitu gan hasa cha totauti ambacho kwa mkeo hukuwa unakipata??? Katika vitu navomshukuru Mungu ni kunpa ubahili wa kiwango cha SGR hasa linapokujaga swala la kuhonga kwa kiwango kikubwa!
 
Ahahaha..umezungumza ukwel. Haya mambo yana cost sana. Kama hujafikia huko ni muhimu kupiga chini mapema
 
Litakwisha in Jesus name
Hapa ndo naamini kuna limbwata aisee....sio akili za kawaida hizo bro...pole sana

"My pain may be the reason for somebody's laugh,but my laugh must never be the reason for somebody's pain"

Charlie Chaplin
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom