Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,132
- 10,514
Faith Jerop alipokutana na mwanamume Mrusi nchini Kenya, alihisi kama ameokota dodo kwenye mnazi. Upendo wao ulichanua vizuri, mdogo mdogo mpaka mahaba yakawa mazito. Na binti yao alipozaliwa, ilikuwa kana kwamba furaha yao imepata nafasi ya kuendelea kuwa imara.
Bi mdada huyu akaona isiwe kesi ngoja afanye safari aende kwa wakwe zake huko Kwa Putin, safari ya Urusi ilionekana kama ni baraka kwa mtoto wao, na fursa ya kuungana kwa ukaribu na baba yake.
Mara tu walipofika Urusi, ukweli ulionekana kuwa mwanaume huyo hakuwa na lengo lolote zuri kwa Mama pamoja na mtoto wao. Sio kuanzisha familia wala kitu chochote kile.
Jamaa alimchukua binti yao mwenye umri wa mwaka mmoja na kumfukuza Faith, hivyo Faith alilazimika kupanda ndege ili aweze kurudi Kenya, bila mtoto wake mchanga.
Wazungu wana msemo wao....
THE GRASS IS NOT ALWAYS GREENER ON THE OTHER SIDE