Kutana na Fatema wa Gaza City

Kutana na Fatema wa Gaza City

Ertugrul Bey

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
13,885
Reaction score
28,140
Screenshot_20260115-074548_SPlayer.jpg


My people,

Milio ya ndege za Kivita na mabomu yanasikika katika mji wa gaza,kwa wakazi wa Gaza haya ndio maisha yao ya kila siku

Kutana na Fatema binti wa miaka 24 mzaliwa wa Gaza ambaye katika documentary inayoitwa SHIKA ROHO YAKO MKONONI NA ENDELEA KUTEMBEA,akielezea maisha ambayo wanaishi pale Gaza

Yeye ni mpiga picha na ana mapenzi makubwa na kazi hiyo,anasema kupiga picha ndio ulimwengu wake na kila kitu kwake,kwa kiasi kikubwa picha nzuri zenye matukio mbali mbali yanayotokea Gaza zimesaidia sana dunia kujua nini kinaendelea Gaza

Anaezelea jinsi alivyopoteza ndugu zake takribani 13 kwenye vita vya Gaza, anaonyesha nyumba za majirani zake zilivyo bomolewa na mabomu na kupoteza marafiki zake vipenzi

Hakuna umeme baadhi ya majengo analazimika kwenda nyumbani kwa rafiki yake kwenda kuchaji simu yake.

Maji ni shida na si salama,chakula nacho ni shida,kuna kipindi anasema mdogo wake wa kiume,anamuuliza mama yake leo tunakula nini,maji anajibu hatuna chakula leo

Fatema kipindi kimoja akiwa anahojiwa online anasema chakula ni shida sana,na pale alipo anashindwa hata kusimama vizur kutokana na njaa

Internet nayo ni shida mara kadhaa wakati anahojiwa mawasiliano yalikuwa yanakatika mara kwa mara

Lakini nyuma ya haya yote kusema ukweli Fatema anaongea kwa kujiamini na matumaini makubwa sana,akihojiwa na mwandishi wa habari kuhusiana na maisha yao ya Gaza,anasema wameyazoea na wanaendelea kuishi kama kawaida kwani hayo ndio maisha yao ya kila siku pale Gaza

Kila mara huwa na tabasamu zuri sana anapoelezea maisha yao ya Gaza, kutokana na maisha yao vita ya kila siku,anasema si ajabu ukamuhoji mtoto wa miaka nane na kumuuliza unataka nini katika maisha? Mtoto akajibu "I want to die" ,hayo ndio maisha ya wenzetu wa Gaza

Alipoulizwa je unampango wa kutaka kuondoka Gaza, akasema hakika Gaza inanihitaji mimi na ni ngumu sana mimi kuiacha Gaza kwa kipindi hiki.

Ndugu yangu msomaji,pamoja na kuwa katikati ya vita,usalama mdogo lakini Fatema na wakazi wa Gaza hawajakata tamaa na maisha bado wanaishi na wanamatumaini makubwa ya kesho yao,kwanini wewe ukate tamaa kisa ni mwaka wa pili au wa tatu hujapata kazi,kwanini ukate tamaa kisa mpaka sasa umri umeenda hujaoa au kuolewa

Tambua kwenye maisha kila mtu ana mapito yake,utapitia kule kule ambapo umepangiwa upite,usivunjike moyo kwakuwa watu wa age yako wamefanikiwa kupita wewe hujui Mungu amekupangia nini mbele ya safari, kuwa imara na kuwa na matumaini juu ya mbele yako iliyo bora zaidi

​

Ni hayo tu!
 
Salama ya watu wa gaza ni kuachana na hamas na salama ya tanzania ni kuachana na ccm chinja chinja na watekaji
 
Back
Top Bottom