Kisa cha David Crespi na mauaji ya mabinti zake mapacha

Kisa cha David Crespi na mauaji ya mabinti zake mapacha

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,443
ht_samL_tessR_080603_mn.jpg


ht_twins_080603_ms.jpg


article-2212289-15543B46000005DC-904_634x390.jpg


Mnamo Januari 2006 lilitokea tukio moja la kutisha nchini Marekani. Yapo matukio mengi ya kutisha yanayotokea nchini humo, lakini hili lilikuwa ni la aina yake na kwa kweli lilivuta hisia za watu wengi.

Mtu mmoja aitwae David Crespi ambaye alikuwa ni makamu wa rais wa benki moja maarufu nchini Marekani, aliwauwa watoto wake mapacha wa kike waliokuwa ana umri wa miaka mitano kwa kuwachoma kwa visu mara kadhaa mwilini na kisha kupiga simu Polisi na kutoa taarifa kuwa ameuwa.

Mkasa wenyewe ulikuwa hivi:

Siku ya tukio bwana David ambaye alikuwa na tatizo la msongeko (Depression), alikuwa nyumbani kwake katika jimbo la North Carolina na mkewe, ambapo alikuwa na mapumziko ya wiki mbili kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya tatizo hilo la msongeko.

Baadaye mkewe alimuaga kuwa anakwenda kutengeneza nywele na kumuacha na watoto wake wawili mapacha. Alipoondoka wale watoto walimuomba baba yao wacheze mchezo wa kujificha, na wakati wanaanza kucheza, baba yao alikwenda jikoni na kuchukua visu viwili. Alikuja navyo sebuleni na kuanza kumshambulia mtoto wa kwanza aitwae Samantha kwa kumchoma kisu mara 18 kifuani, mgongoni na kichwani.

Pacha mwenzie aitwae Tessara alipoona mwenzake anashambuliwa, akaanza kukimbia ili kujificha. Alifanikiwa kujificha ili baba yake asimwone, lakini bahati haikuwa yake, kwani baba yake alimfuata huko mafichoni na kumchoma kisu mara kumi na nne.

Alipomaliza kuwauwa, alipiga simu polisi na kuwajulisha kuhusu mauaji aliyoyafanya kisha akabadilisha nguo kwa kuvua nguo zenye damu na kuvaa nguo nyingine kabla Polisi hawajafika. Wakati wote huo alikuwa hajarejewa na ufahamu wa kuona kama alichofanya ni kitendo cha kinyama na kikatili. Lakini baada ya Polisi kufika, ndipo aliporejewa na fahamu na kugundua kuwa ameuwa watoto wake wa kuwazaa.

David ambaye sasa anatumikia kifungo cha maisha gerezani, majirani zake pamoja na wafanyakazi wenzake wanamwelezea kama mtu muungwana sana na aliyeonekana kuwa mwenye mafanikio. Lakini hakuna aliyejua kama alikuwa na siri kubwa moyoni aliyokaa nayo kwa miaka 11 ya kutaka kuiangamiza familia yake mwenyewe ya mke na watoto wake watano.

Wakati anahojiwa na polisi alikiri kuliona tukio la kuwauwa wanaye kama jukumu lake, kwani kulikuwa na kitu kinamwambia auwe na aliona afanye hivyo. Pia aliona kumuuwa mmoja isingekuwa busara, kwani kwa kawaida malezi ya watoto mapacha hutendewa jambo wote kwa pamoja.

Alipoulizwa kwa nini asijiuwe yeye mwenyewe, badala yake akauwa wanaye, David alikiri kufanya majaribio kadhaa ya kutaka kujiuwa, lakini mkewe aitwae Kim alipozungumza naye na kumshauri kwamba asije akafanya tena jaribio la kutaka kujiuwa aliahidi kutojaribu tena kufanya hivyo.

Tatizo la msongeko (Depression) ni kubwa sana nchini Marekani. Matukio mengi ya mauaji yanayotokea nchini humo ni ushahidi tosha kwamba tatizo ni kubwa zaidi. Inakadiriwa kwamba watu wapatao milioni 19 wanasumbuliwa na msongeko na miongoni mwao wapo ambao wameuwa au kujiuwa kutokana na tatizo hili. Kwa tafsiri isiyo rasmi msongeko ni tatizo linalotokea ndani ya ubongo linalohusisha chembe chembe zilizoko ndani ya mishipa ya fahamu kushindwa kuwasiliana vizuri.

Sababu zinazotajwa kusababisha msongeko ni nyingi lakini kubwa kabisa zinazopelekea mtu kupatwa na msongeko ni hizi zifuatazo:

1. Kupoteza ajira au kuwa na wasiwasi wa kupoteza ajira
2. Kuishi katika lindi la umasikini wa kupindukia kiasi cha kukosa matumaini ya kujikwamua.
3. Kutoridhika na hali aliyonayo mtu kiuchumi na kushindwa kukubaliana nayo kutokana na shinikizo la watu waliomzunguka hususan kwa wanandoa.
4. Migogoro ya ndoa isiyokwisha au ya kifamilia.
5. Matukio kama vile vifo vya wazazi, kutelekezwa utotoni na udhalilishwaji wa kijinsia
6. Maradhi sugu

Dalili za mtu aliye na msongeko zinatofautiana kati ya mtu na mtu, lakini nitajaribu kutaja chache:

1. Kukosa usingizi au kuwa na usingizi mzito usio wa kawaida
2. Kukosa raha
3. Kujiona ni mwenye hatia
4. Kuwa na wasiwasi
5. Kuishiwa na nguvu kusiko kwa kawaida na kukosa hamu ya kula au kuwa na hamu ya kula kupita kiasi hivyo kupelekea kupungukiwa na uzito au kuongezeka uzito.
6. Kukosa matumaini na kuyaona maisha kama hayana maana
7. Kuwa na mawazo ya kuuwa au kujiuwa ya mara kwa mara.

Mara nyingi dalili za mtu mwenye msongeko zinaweza kudumu akilini kwa miaka mingi bila mtu kujua. Na hata kama muathirika anatamka kwamba atajiuwa au atauwa mtu, inakuwa ni kama masihara kwa mtu asiyeelewa, lakini lazima ifahamike kwamba, wanaotamka hivyo wanakuwa wamedhamiria.

Watanzania wengi wanaosumbuliwa na tatizo hili la msongeko, lakini labda kwa sababu hatuna takwimu sahihi ndiyo sababu tatizo hili limekuwa halifahamiki. Wapo watu wengi sana wameuwa au kujiuwa kutokana na tatizo hili la msongeko, lakini kwa bahati mbaya sana watu hulihusisha tatizo hili na imani za kishirikina. Kuhusisha tatizo hili na ushirikina ni kujidanganya bure, kwani hakuna ukweli wowote na matokeo yake wengi wamejiuwa au kuuwa kutokana na kutopata tiba muafaka.
 
READ THE TRANSCRIPT OF DAVID CRESPI'S 911 CALL


The following are excerpts from David Crespi's call to 911 after murdering his daughters

Operator: 911 emergency do you need police, fire or medic?
Crespi: Matthews
Operator: I'm sorry. Do you need police?
Crespi: Matthews
Operator: Matthews police?
Crespi: Yeah
Operator: OK, your cell phone is cutting in and out, but I'm going to transfer you. Just a second.

Second Operator: Police department.
Crespi: Yeah. I just killed my two daughters.
Operator: You just what?
Crespi: I just killed my two daughters.

Third Operator: Sir, tell me what happened. OK. How. I mean, what's going on right now?
Crespi: I just freaked out.
Operator: Are you on medication?
Crespi: Yeah
Operator: Are they breathing or anything now?
Crespi: No
Operator: What did you do to them?
Crespi: I stabbed them.
Operator: You stabbed them?
Crespi: Yeah.
Operator: OK. How many times did you stab them?
Crespi: I don't know.
Operator: You don't know? Is anybody else in the house with you?
Crespi: No.
Operator: No?
Crespi: My wife just left.
Operator: Who are these girls?
Crespi: They're my daughters
Operator: Your daughters? OK. How old are they?
Crespi: Five
Operator: They're twins?
Crespi: yeah
Operator: OK. So we've got help started. Can you tell me what happened? How did you kill them?
Crespi: With a knife
Operator: And you're sure they're deceased?
Crespi: Yeah. Yeah, they're dead.
Operator: OK.
Operator: Sir, did you have a fight with your wife? Is this what happened?
Crespi: No
Operator: No? You just couldn't handle it anymore?
Crespi: Yeah.
​
 
mtambuzi ndio maana mie huwa najionea hapa jf ndipo pa kupatia liwzo palea mabpo naona kila kitu hakiendi ama la naamua kutafuta friends na kutoka nao lol!
kusubiri upate depression ni kubaya sana sana, usishangae watu wanajiua kisa ni depression.
 
Msongeko ndo masongo wa mawazo???
Hivi viswahili hivi mhh
Hao watoto nywele zao kama weaving langu.
 
Daaah huyu jamaa alikuwa unsound kabisa!

Kwakweli alifanya ukatili mkubwa sana!

Thanx Mtambuzi
 
Last edited by a moderator:
mtambuzi ndio maana mie huwa najionea hapa jf ndipo pa kupatia liwzo palea mabpo naona kila kitu hakiendi ama la naamua kutafuta friends na kutoka nao lol!
kusubiri upate depression ni kubaya sana sana, usishangae watu wanajiua kisa ni depression.

ni kweli haya mambo usipoangalia njia muafaka ya kuyahandle kujiua siyo ajabu

mojawapo ya kukwepa hizo stress ni kwenda '"leo tupo hapa Pub" na kujumuika kama siku ile

Mkuu Mtambuzi tuwasiliane kama mama Ngina hajakaba mpaka Penati
 
way to go brother, i salute you, thumb up!! ila naomba uniambie tiba muafaka uliyosema hapo mwisho, nn tiba ya depression? maana izi dalili hadi namba sita ninazo zote,..
1. Kukosa usingizi au kuwa na usingizi mzito usio wa kawaida
2. Kukosa raha
3. Kujiona ni mwenye hatia
4. Kuwa na wasiwasi
5. Kuishiwa na nguvu kusiko kwa kawaida na kukosa hamu ya kula au kuwa na hamu ya kula kupita kiasi hivyo kupelekea kupungukiwa na uzito au kuongezeka uzito.
6. Kukosa matumaini na kuyaona maisha kama hayana maana
..................nn tiba mkuu?
 
Mkuu Mtambuzi,tafadhali malizia mahojiano kati ya Mr.David na Operators au ndio yameishia apo?
 
Mtambuzi nashukuru kwa hii habari ya kutisha
naomba umalizie namna police walivo mkamata,ushahidi mahakamani na reaction ya mkewe.
kuna kesi ingine ntakupa jina baba mmoja mcheza basketball Jimmy aliuwa familia yake yote watoto wawili na mke
akampa kazi black mmoja ya kusafisha nyumba yake na gari kuficha ushahidi
natafuta majina yake kamili nimeiona discovery channel leo hii usiku.
ungetudadavulia hiyo ingekuwa nzuri sana
 
Me huo msongeko ndo ningeusonga vizuri huko huko gerezani! Mi nahis ni mapepo. Ila aisee wanangu...ptuuuu yeuwii!!
Thanx Mtambuzi
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom