Kisa cha chenye mafunzo cha kuweza kung'amua

Omari Makoo

Member
Sep 6, 2016
78
39
Hapo zamani kulikuwa na nchi mbili moja ikifahamika kwa jina la Uganzo na nyingine ikifahamika kwa jina la Nzotani. Siku moja waziri wa mambo ya ujenzi wa Nzotani aliamua kumtembelea waziri wa wa ujenzi wa nchi ya Uganzo.

Alipofika nchini Uganzo alishangazwa sana na jumba kubwa la waziri wa nchi hiyo ya Uganzo hivyo ikabidi amuulize, mwenzangu ulifanikiwaje kupata pesa ya kujenga mjengo huu, waziri wa uganzo akajibu kwamba ili ufahamu hayo twende rotion ya juu ya nyumba yangu.

Walipofika juu wakawa wanaiona nchi ya Uganzo kwa uzuri kabisa hivyo akaanza kumwambia unaliona daraja lilee, waziri wa Nzotani akatizama kwa umakini na kuliona daraja hilo lililokuwa mbali na pale walipo.Basi chenchi ya daraja lile ndio nyumba hii.

>>>>>>>>>>>>>Miaka kadhaa ikapita<<<<<<<<<<<<<<<<<<<

Wazii rwa Uganzo nae akaenda Nzotani alipofika huko Nzotani akakaribishwa kwenye jumba la kifahari la waziri wa mambo ya ujenzi. Alishtuka na kushangazwa zaidi na kuladhimu aulize ndugu yangu uliwezaje kujenga jumba la kifahari kama hili? Waziri wa Nzotani akajibu, ili kufahamu hayo twende ghorofa ya mwisho ya nyumba yangu.

Walipofika juu kabisa wazili wa Nzotani akaanza kumwambia unaliona lile daraja kulee? Waziri wa ujenzi wa Uganzo kila akitazama haoni kitu kiasi cha kushangazwa na kauli ya waziri wa Nzotani, hivyo akahoji busara iliyonyuma ya kauli ya waziri wa Nzotani, kisha waziri wa Nzotani akajibu kwamba pesa yote ya daraja ambalo lilitakiwa kujengwa pale ndio nimetumia kujenga nyumba hii.

JE UMEJIFUNZA NINI KUTOKANA NA KISA HIKI?
 
Back
Top Bottom