Kiroja cha Ngerengere

Kiroja cha Ngerengere

Leo tunatambiana Mkuu wa Majeshi kaonekana Ngerengere, tunapigana vijembe vya udaku wa afya yake na tetesi za yeye "kutoweka".

Hatulizungumzii hata kidogo tukio lenyewe kubwa pale Ngerengere.

Hatujiulizi Tanzania tumekosa fedha za kujenga na kuboresha kikosi chetu cha anga mpaka tuende Uchina kuomba msaada na kufadhiliwa?

Yaani hatuna dola za kimarekani Milioni mia moja popote? ni heri hata masalia ya Escrow na EPA yangetumika hapo Ngerengere au pale Kigamboni kuliko kuonyesha utegemezi wa hali ya juu kwa China.

Wanatukopesha kujenga Bandari, mitambo ya gesi, reli, barabara, kujenga majengo, matumizi ya serikali, zana za kijeshi na sasa kambi nzima ya jeshi?

Tutalipaje hili deni? Tutalipaje hizi fadhila?

Rev. tulimchagua wenyewe... sasa anatupiga PR bila gloves wala KY
 
Nani amekuambia huu ni mkopo?

Historia ya Tanzania na China haijaanza leo. Tafuta hata historia ya huo uwanja na kambi ya kijeshi.

Hii ni mikemko ya kisiasa.

Kuna baadhi ya watu hapa Jf walihoji uwepo nchini wa Mkuu wa Majeshi lakini hatukuona thread ya kuwaambia wanachokihoji hakina mantiki. Leo Mkuu wa Majeshi amejitokeza, ghafla tunaona mnaanza kuhoji hoja za watu wanajaribu kupiga vita majungu na udaku kuhusu Mkuu wa Majeshi.

Hii ndiyo Tanzania ambayo kuwa watu walituaminisha kwa muda mrefu hata wawekewe bastola kichwani hawawezi kumchagua Lowassa kutokana na kashfa nyingi za ufisadi na rushwa lakini kwa sasa ndiyo wamekuwa wapiga debe wa Lowassa.

Huu ni unafiki wa kisiasa.
 
Mlizusha ya CDF Sasa mmeumbuka hamtaki watu wahoji hiyo tabia ya kutunga na kusambaza tuhuma ili kujipatia mtaji wa kisiasa ... Aibu zenu..... Njia ya mwongo ni fupi sana ......
Hata mimi ninawashangaa wanapoanza kuhoji hoja za watu wanaopiga vita majungu na udaku kuhusu Mkuu wa Majeshi.
 
Ina maana katika kusoma kwako hujayaona haya maandishi au haujaelewa?
Hujaelewa hoja yangu badala yake unakimbilia sentesi moja.

Kama ningekuwa sijayaona hayo maandishi unadhani ningeandika chochote?

Nimeyaona, nikayasoma na kuyaelewa! Una lingine la kuandika kuhusiana na hoja yangu?
 
Tuishie hapa maana nakumbuka siku si nyingi zilizopita ni wewe uliyeshindwa kuelezea neno mdahalo, sishangai hata maana ya neno hoja na matumizi ya neno hili kwako inakuwa ngumu kuelewa...

Hasta luego amigo!!

Kama hufahamu maana ya hoja utafahamu vipi kama swali ni sehemu ya hoja?
 
Ndio maendeleo ya Kikwete hayo, atakuambia matunda ya safari za Rais huku anatuacha na deni la trilioni kibao.

"Nchi maskini haiwezi kujitegemea kwa msingi wa fedha kama inategemea msaada wa nchi za nje" Mwenyekiti Nyerere.
2005 exchange rate: 1$ = 500Tsh
2015 exchange rate: 1$ = 2250Tsh.
Economics 101 inaonesha safari zimeinua uchumi wetu. .....Na kila mmoja akapiga makofi kushangilia!
 
rev kishoka
IPO hoja hapo!
Total country has already sold.
""haiwezekani mtu akakukopesha tu,kibaya tena na tena mfululizo!

Mkopo ni deni, na kwa mkopeshaji ni uwekezaji.

Sasa hilo deni, mtalipa ninyi na watoto wenu wakati mnakufa kwa kukosa dawa, nchi iko gizani, uzalishahi hakuna, maisha yako juu, mkijilinda wenyewe kwa sungusungu huku mkitafuna mizizi!.

CHAGUENI CHAMA CHANGU CCM MUONE!.
 
Mitanzania bwana... naskia "barabara za Makufuli" etc etc utadhani hela ya kuzijenga haijakopwa. Mnaingizwa kwenye minyororo ya madeni makubwa ambayo mtalipa hadi kizazi cha kumi kijacho, huku mnakenua.

Tunataka mabadiliko. Hata jiwe liongoze, lakini siyo CCM tena. Mabadiliko. Mabadiliko.
 
Nani amekuambia huu ni mkopo?

Historia ya Tanzania na China haijaanza leo. Tafuta hata historia ya huo uwanja na kambi ya kijeshi.

Hii ni mikemko ya kisiasa.

Kuna baadhi ya watu hapa Jf walihoji uwepo nchini wa Mkuu wa Majeshi lakini hatukuona thread ya kuwaambia wanachokihoji hakina mantiki. Leo Mkuu wa Majeshi amejitokeza, ghafla tunaona mnaanza kuhoji hoja za watu wanajaribu kupiga vita majungu na udaku kuhusu Mkuu wa Majeshi.

Hii ndiyo Tanzania ambayo kuwa watu walituaminisha kwa muda mrefu hata wawekewe bastola kichwani hawawezi kumchagua Lowassa kutokana na kashfa nyingi za ufisadi na rushwa lakini kwa sasa ndiyo wamekuwa wapiga debe wa Lowassa.

Huu ni unafiki wa kisiasa.
Kwahiyo tunakopa commercial banks kulipia barabara, lakini makuruza ya washawasha tunalipa cash sio??

haya weee
 
Leo tunatambiana Mkuu wa Majeshi kaonekana Ngerengere, tunapigana vijembe vya udaku wa afya yake na tetesi za yeye "kutoweka".

Hatulizungumzii hata kidogo tukio lenyewe kubwa pale Ngerengere.

Hatujiulizi Tanzania tumekosa fedha za kujenga na kuboresha kikosi chetu cha anga mpaka tuende Uchina kuomba msaada na kufadhiliwa?

Yaani hatuna dola za kimarekani Milioni mia moja popote? ni heri hata masalia ya Escrow na EPA yangetumika hapo Ngerengere au pale Kigamboni kuliko kuonyesha utegemezi wa hali ya juu kwa China.

Wanatukopesha kujenga Bandari, mitambo ya gesi, reli, barabara, kujenga majengo, matumizi ya serikali, zana za kijeshi na sasa kambi nzima ya jeshi?

Tutalipaje hili deni? Tutalipaje hizi fadhila?

china ni rafiki wa kweli.china ni nchi ya pili kwa ukubwa wa uchumi.mikopo ya china ina masharti nafuu kuliko nchi zilizoendelea.kuna ubaya gani kukopa kwa nchi rafiki ilioendelea kwa teknolojia ya hali ya juu.kama ndege mpya tumenunua toka kwao kwa nini wasitujengee uwanja
 
Ndio maana wageni wana control mpaka dira ya kuongoza nchi, halafu tunategemea mabadiliko ndani ya ccm!!! vigezo vya mikopo ya world bank na IFM chini ya mkukuta ndio kiini cha sera za ccm...., viongozi wetu wapo tayari kugawa rasilimali kwa wageni na kutufanya tuwe wakopaji na omba omba wa kutupwa, na sisi tuna imba tu kibwagizo cha wimbo tusioujua ati "mbele kwa mbele" tukiulizwa mbele kwa mbele ndio wapi hatuna majibu.....
 
Hakuna nchi hata moja duniani yenye uwezo wa kibajeti wa kufanya mambo yake yote inayotaka. Kwa sababu hiyo nchi huweka vipsumbele na phases za kutekeleza mipango yake. Anapotokea partner wa kuiongezea nguvu serikali kufanya mambo yake mapema zaidi hakuna ubaya.
Marekani ndio nchi inayoongoza kwa kukopa pesa nyingi toka China. Wewe mtanzania ukisusia na kubeza msaada wa China unajicheleweshea maendeleo yako bure.

By the way, ni sahihi watu kukemea tabia ya kuzusha mambo kuhusu viongozi. Kujaribu kibelittle ukemeaji wa tabia hiyo ni sehemu ya kuishabikia.
 
Na China ni Nchi inayokopa pesa toka Nchi gani?
 
Back
Top Bottom