Kipindi maalum: Bi. Titi Mohamed

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,925
30,273
MWANZO MEDIA: MATENGENEZO YA KIPINDI MAALUM KUHUSU MAISHA YA BI. TITI MOHAMED (1926 - 2000)

Mwanzo Media wamenihoji kuhusu maisha ya Bi. Titi Mohamed.

Huu ni upepo mpya kuona kumekuwa na mwamko mpya wa kutaka kujua historia ya uhuru wa Tanganyika na mashujaa wake ambao kwa miaka mingi walikuwa wamefutwa katika kumbukumbu za TANU na historia ya uhuru wa Tanganyika.

Nimeamua kwa makusudi kabisa kuweka picha za Bi. Titi akiwa msichana mdogo wa kiasi cha miaka 26 ili msomaji wangu upate ladha ya historia hii kama ilivyokuwa katika miaka ya mwanzo ya chama cha TANU.

Angalia picha mbili za mwisho ya kwanza kulia ni Bi. Titi Mohamed, Maria Nyerere, Julius Nyerere, Rashid Kawawa, nyuma ya Nyerere ni Tewa Said Tewa.

Hii ni moja katika picha alizopiga Mohamed Shebe.

Mwangalie mama yetu Bi. Biti Mohamed na haiba yake alivyokuwa msichana.

Picha ya mwisho wa kwanza kuliani Bi. Titi Mohamed katika moja ya mikutano ya mwanzo ya TANU Viwanja Vya Mnazi Mmoja.

(Mwangalie Bi. Titi amevaa baibui la ukaya na alikuwa akihutubia mikutano akiwa ndani ya baibui).

Anaefuatia ni Clement Mtamila, Sheikh Suleiman Takadir na mwisho ni Julius Nyerere.

Nyuma kulia ni John Rupia na Rajab Diwani.

Baada ya uhuru kupatikana mwaka wa 1961 baadhi ya wazalendo hawa katika picha hizi mbili watajikuta katika hali ambayo hakuna aliyeitegemea wala kuwaza huenda ikatokea..

Hapa ndipo anapoingia Bi. Titi; kuanguka kwake na kujikuta anatumikia kifungo cha maisha na kupoteza mali zake, heshima yake na kufutwa jina lake katika historia ya uhuru wa Tanganyika.

Lakini kwa kasi ya ajabu Bi. Titi akatoka kifungoni, akarejeshewa mali zake na heshima yake.

Haya yote yakitokea bila ya kutetewa na yoyote.

Bi. Titi sasa anatajwa na kuadhimishwa kama inavyostahili.

Kipindi hiki In Shaa Allah kitakuwa hewani hivi karibuni.

Screenshot_20211022-191538_Facebook.jpg
 
Back
Top Bottom