Kipindi Diplomasia yetu ilipokuwa ikiwaka kama nyota

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,498
51,092
Uongo mbaya, Diplomasia ya nchi yetu kipindi cha JK ilikuwa next level ndani ya Afrika. Sasa hivi tumekuwa too local huku tukimtegemea mtu mwenye arrogance ya usomi kuwa kiongozi wa diplomasia yetu.

Diplomasia ina misingi yake, huwezi kuwa kwa sababu wewe ni profesa basi ukiingia kwenye meza za mazungumzo basi unataka kuproject ile sense kwamba "Mimi nimesoma, mimi ninajua kukuzidi, kaa kimya nisikilize niongee nikufundishe", Diplomasia haiko hivyo.

Hebu msikilize JK hapa akiarticulate mipango na mikakati ya kiuchumi ya nchi.

 
... kipindi cha JK akiwa Foreign Minister au akiwa Rais? Miaka kumi kumi kila kipindi.
 
Kiukweli, JK alikuwa bonge la presidaa ila alikosea sehemu moja tu muhimu! Rushwa! Hakupambana na rushwa ipasavyo, aliachia mambo yajiendee kienyeji. Hapo tu; otherwise, angefanikisha suala la rushwa dah! angekuwa Rais wa kupigiwa mfano duniani kote.
 
Kiukweli, JK alikuwa bonge la presidaa ila alikosea sehemu moja tu muhimu! Rushwa! Hakupambana na rushwa ipasavyo, aliachia mambo yajiendee kienyeji. Hapo tu; otherwise, angefanikisha suala la rushwa dah! angekuwa Rais wa kupigiwa mfano duniani kote.

Alipambana na rushwa kwa kufuata sheria na taratibu
Sababu inayotufanya tudhani kipindi cha utawala wake rushwa ilitamalaki ni kwa sababu aliachia uwazi, magazeti na vyombo vya habari pamoja na bunge vilikuwa huru kuandika ufisadi na kuuibua na kuutangaza mpaka wananchi wakajua.

Sasa leo hii mambo yanafanyika gizani, watu wanapiga kimyakimya Utajulia wapi?.

Hivi mkuu wa mkoa mmoja aliyekwepa kodi kwa kuingiza fenicha kwa jina la misaada kachukuliwa hatua gani?

Vipi zile Trilion 1.5, tulizoambiwa kuwa kiasi fulani kimeenda Zanzibar, mara tukaambiwa hapana kulikuwa na matumizi mengine na blah blah kibao
 
Back
Top Bottom