Tuiangazie Diplomasia katika kukuza uchumi endelevu

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
DIPLOMASIA BORA NI MSINGI WA UCHUMI IMARA

Na Elius Ndabila
0768239284

Diplomasia ni nadharia ambayo tumekuwa tunaitumia sana tukiwa tunalenga uhusiano baina ya mataifa duniani. Leo nitazungumzia kinagaubaga juu ya diplomasia katika sekta ya kukuza uchumi nchini.


Uchumi na maendeleo kote duniani yanategemea jambo moja kubwa ambalo ni mahusiano(Diplomasia). Kila nchi inapambana kuongeza mahusiano ya kidiplomasia na nchi nyingine ili kujihakikishia maendeleo endelevu. Zipo nchi zinatafuta malighafi na zipo zinazotafuta masoko Kwa ajili ya malighafi zao.

Dunia ya leo nchi ikijifungia ndani basi hata uchumi wake utaporomoka kwa kiwango kikubwa kwani nchi zinashindania uhusiano wa masoko.

Zamani Mataifa makubwa yalitumia nguvu kujenga mahusiano. Ukilitazama neno "ukoloni" Kwa jicho la ziada huwezi kulitenganisha na diplomasia. Tofauti yake ni kuwa ukoloni mataifa makubwa yalitumia nguvu kuzitawala nchi ambazo zina rasilinali ila zimeshindwa kuzitumia. Mataifa makubwa yalipora hizo rasilimali, wakaziongezea mnyororo wa thamani na kuja kutuuzia.

Leo linatumika neno "DIPLOMASIA" lenye dhana inayoshahibiana na ukoloni, lakini tofauti yake kwenye diplomasia unatumika ushawishi wenye mahusiano mema. Hushikiwi silaha kutengeneza mahusiano bali ushawishi. Bado mataifa yenye nguvu ndiyo yananufaika na hii diplomasia pamoja na kwamba hakuna mipaka ya nchi yoyote kutoitumia. Ukubwa wa teknolojia yako ndio unaokusaidia kuhodhi soko la dunia kutokana na ubora wa bidhaa yako.

Tanzania ni moja ya nchi ambayo ninaamini hatujaitumia vizuri diplomasia. Pamoja na kuwa na Balozi nyingi duniani, bado ninadhani balozi zetu hazijatumika sawa sawa kutengeneza fursa mahali waliko. Hatuwezi kushindana na mataifa makubwa ku-dominate soko la Dunia, lakini tunaweza kunufaika na uwekezaji mkubwa utakaotusaidia kuingia kwenye soko la Dunia. Mbona China imeweza?

Ulimwengu ulipofikia Balozi ndiye anatakiwa kufanya kazi kubwa kuliko Rais wa nchi. Balozi anapaswa kuto kulala. Anatakiwa kutumia maarifa yake yote, uwezo wake wote kutafuta fursa kwa ajili ya nchi yake. Balozi ndiye mtu wa kufungua milango. Mataifa yaliyashavuka kwenye kutengeneza mahusiano ya kisiasa, Dunia ipo kwenye mahusiano ya kiuchumi ndiyo maana kila balozi inakuwa na Consular.


Kwa mfano Tanzania Duniani ni nchi ya pili yenye vivutio vingi ikitanguliwa na Brazil katika Afrika Tanzania ni ya kwanza. Lakini pamoja na hayo Tanzania hata kwenye nchi kumi bora zenye Watalii wengi Afrika haipo. Inapitwa na Morocco, Ethiopia, Msumbiji, Zimbabwe, SA, Ethiopia n.k ambazo zinavivutio vichache. Hapa tatizo ni nchi katika diplomasia ya uchumi.


Katika Afrika Tanzania ni nchi ya tano kuwa na idadi kubwa ya watu ikitanguliwa na Nigeria, Misiri, Ethiopia na Congo. Lakini kiuchumi tunapitwa na Rwanda, Kenya, Afrika kusini n.k. Hapa tumeshindwa kuitumia idadi kubwa ya watu katika diplomasia ya kiuchumi. Takwimu za mwaka 2016 Tanzania ilikuwa ya nchi ya 10 kiuchumi.

Viashiria vinavyoonyesha kuwa bado hatujaitendea haki diplomasia kiuchimi ni pamoja na mazao mengi tunayozalisha kukosa mahali pa kuuza. Pili Tanzania kuwa na vivutio vingi lakini kupitwa na nchi zisizo na vivutio kama Tanzania kwa utalii. Pili asili ya kiswahili tena kiswahili fasaha ni Tanzania, lakini Duniani Kenya ndiyo inaongoza kutoa Walimu wengi kwenda kufundisha nje. Tatu Tanzania tuna aridhi yenye kila aina ya rasilimali, lakini bado wawekezaji kutoka nje bado hawafanani na rasilimali zilizopo. Haya na mengine mengi ni kuto kuitumia vizuri diplomasia.

Ili kuweza kufikia maendeleo tunayoyataka hususani ya Viwanda lazima tukubali kubadilisha mindset zetu. Lazima kama taifa tuwe na dira ambayo itawaongoza watu wanaoiwakilisha nchi nje ya nchi. Maana yangu ni kuwa Balozi na wasaidizi wake hasa mtu anayehisika na masoko wawe wanapewa kipindi cha mwaka mmoja mpaka miwili. Wanapewa maelekezo kwenye nchi wanayokwenda kuwa unatakiwa ndani ya miaka miwili tunataka kama nchi tunufaike na uwepo wako huko katika mambo 1,2,3......akishindwa kufanya anapaswa kuondolewa kwa kuwa hajaisaidia nchi.

Yapo mambo ambayo Rais hapaswi kuhangaika nayo. Wanapaswa kuhangaika nayo Mabalozi. Inapofikia Rais kufanya mambo ambayo yangefanywa na Waziri wa mambo ya nje Kwa usimamizi wa Balozi basi dhana hiyo inaonyesha walipewa jukumu hilo hajasimama sawasawa.

Rais wa awamu ya sita alisema kazi yake ya kwanza ni kufungua nchi. Haimaanishi nchi ilikuwa imefungwa minyororo, rahashaa! Alikuwa na maana ya kuendelea kuijenga na kuiimalisha Tanzania katika jumuiya ya kimataifa. Dhana ya Rais ni kuwa Tanzania hatuwezi kujiletea maendeleo pekee yetu lazima tuwe na wenzetu wa kufanya nao biashara.

Leo si siku ya kuhesabu faida tulizopata baada ya kuanza kuifungua nchi, ni siku ambayo nilitaka kuweka uzito kwenye kuchangamkia fursa ya Uhusiano wa kimataifa. Ni siku ambayo nilitaka kuwatia shime askari wetu ambao wapo nje kupambana yaani Balozi wetu kuwa waongeze nguvu. Uchimi wa nchi unawategemea sana wao na Rais na Watanzania tunategemea positive impact kutoka kwao. Wajue huko hawajaenda kuuza sura bali kupambana na kuifungulia Tanzania milango ya kiuchumi.

Ukizitazama Marekani, China, Japani, Ujerumani, Uingereza, Ufaransa, India, Italia, Brazil na Canada ambazo ndio nchi tajiri duniani basi unaweza kugundua zilifikia hapo kwa sababu ya ushawishi wake duniani uliotokana na kuimalisha diplomasia.
 
11 November 2022
Kenya’s Foreign Affairs minister, Alfred Mutua, speaks out on EAC trade agreements, single currency, taxation, open borders , Transportation, diaspora

Source : the new times Rwanda
 
Professor Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi Minister of foreign affaires in Magufuli Government


As a matter of principles we are part of this globe, but we will never ever allow any. anyone to undermine our dignity as human beings and our sovereignty for aid and assistance. Professor Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi Minister of foreign affaires in Magufuli Government
 
Back
Top Bottom