Uadilifu na kuheshimu misingi ya Sheria kwa nchi yetu

Dec 7, 2020
10
1
Habari zenu ndugu wana Simiyu wenzangu na vijana wenzangu, imani yangu kila mmoja anachapa kazi kwa maslahi mapana ya Taifa letu hili.

Leo nimewiwa nami kuzungumza kidogo kuhusiana na kinachoonekana kuwa ni changamoto kwa kijana mwenzetu CHIEFSON. Kijana mwenzetu na kiongozi mwenzetu ndani ya chama leo hii ni mfungwa na siyo kiongozi tena katika nafasi na wadhifa aliyokuwa nao.

Leo hii ndugu yetu hayupo huru tena. Bado ni kijana, anandoto nyingi kwa maslahi yake binafsi, familia yake, chama chake na hata taifa lake, leo hii hatupo naye tena kwenye ulimwengu wa uhuru.

Ndugu zangu na vijana wenzangu, binafsi ninayomaumivu makubwa sana kwa mambo mawili tuu;

1. Ninamaumivu kwa muda wa CHIEFSON aliyohukumiwa nao kupotea bila kuingiza chochote na kuweka doa kwa mamlaka na jamii.

2. Ninaumia kwa umri na ndoto ambazo kwa vyovyote huenda angezitimiza kwa maslahi mapana ya taifa na chama kwa kuwa tayari alikuwa kiongozi ndani ya Chama chetu Cha Mapinduzi CCM.

Ndugu zangu, tukio hili kwetu kwanza ni pigo lakini tulichukue kama case study yenye uhalisia kwa Dunia na vizazi vya sasa ambao ni mimi na wewe. Leo mimi na wewe tunazo ndoto nyingi na kubwa kwa ajili ya kuandaa kesho yako kuwa nzuri na hata kuacha alama kwa taifa lako, lakini siku moja unashangaa katika mazingira yasiyo rasmi ndoto zako zinaporomoka.

Vijana wenzangu, tumeingiliwa na ugonjwa mmoja unaitwa mitandao ya kijamii+ujuaji+ushabiki ulio na tija+dharau+kejeri, matusi, kuchafuana na kutokutii mifumo na mamlaka za kisheria+ujasiri usio na tija matokeo yake sheria kuchukua mkondo wake.

Ndugu zangu na vijana wenzangu, kaa chini utafakari kwa kina na kwa kutumia mifano halisi kwamba, hakuna aliye juu ya sheria, na hakuna mamlaka zilizo juu ya sheria. Kila mtu, kila mamlaka, kila taasisi inaongozwa na inapaswa kutii, kuendeshwa na kufuata sheria zetu za nchi na sio vinginevyo.

Tofauti na hapo ukiona umenyamaziwa na huku unajua umevunja sheria, ujue kuna busara tuu ya kiutu imetumika na siyo sheria/mamlaka zinazosimamia sheria zimekuogopa.

Mitandao ya Kijamii na Simu Janja
Ni dhahiri kuwa kila mtu anasimu/kifaa chake cha mawasiliano alichonunua kwa pesa yake, lakini sentesi hii haifuti maana na ukweli kwamba kununua wewe kwa pesa yako siyo kigezo cha kutumia unavyotaka.

Kitendo cha kutumia kifaa chako kusababishia jamii nyingine taharuki na simanzi. Hiyo haipo kwa maujibu wa sheria zetu za nchi, zaidi unalazimika kutumia kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi.

Tubapokuwa na hizi simu janja na vifaa mbalimbali vya mawasiliano, tunajisahau na kujikuta tunakiuka sheria, kanuni na taratibu za nchi, jambo ambalo ni kinyume cha sheria zetu za nchi ambazo tunauhuru wa kuzisimamia na kuzifuata wenyewe.

Ndugu zangu, wakati mwingine tumekuwa wengi sana wa kuzimalalamikia mamlaka zinazosimamia sheria, kama mahakama, polisi n.k, lakini kumbe sisi ndiyo tumekuwa tunazichokoza mamlaka hizi bila kujua ama kwa makusudi huku ukijua, lakini mwisho tunalalamika kuwa hatujatendewa haki.

Niwaombe vijana wenzangu na hasa vijana wenzangu wa @UVCCMTAIFA, tuishi kwa kufuata sheria kanuni na taratibu zote za nchi. Chama Cha Mapinduzi ni chama kinachowaandaa vijana kuwa viongozi wema na waadilifu kwa taifa kupitia jumuiya yake ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa @uvccmtaifa.

Hivyo kumbe Chama Cha Mapinduzi ni tanuri la viongozi na siyo kichaka cha kujifichia na kuficha wabadhirifu na watovu wa nidhamu kwa nchi yetu, na ifagamike kuwa, jukumu pekee tulilonalo sisi vijana hasa vijana wa UVCCM, ni kuhakikisha tunaendelea kuisaidia serikali yetu ya Chama Cha Mapinduzi na viongozi wake wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi CCM na siyo kuwabeza, kuwatusi na kuwakashfu kwa mambo mazuri na makubwa yanayofanywa na viongozi wetu.

Ni maajabu sana leo kuona kijana mwenzangu unasimama na kuhukumu, kukashfu, kutusi na kukejeri viongozi wetu wa chama na serikali. Hatua hii siyo nzuri na ni laana hata kwa mwenyezi Mungu. Kwanza viongozi hawa ni sawa na wazazi wako waliokuzaa, pili taifa letu halijaundwa na kulelewa kwa matabaka ya ukabila, na hata ubaguzi.

Mwl. Nyerere Aliposimama kuanzisha muungano, kauli yake ya kwanza alikemea sana suala zima la ubaguzi na ukabila, alipiga vita sana na kupinga hatua hizo ndani ya taifa letu. Leo kijana mwenzangu mwenye ndoto kubwa kwa taifa, ngvu kazi kubwa kwa taifa unapoteza muda na wakati wako kwa kushindwa kujihifadhi katika matamshi na kulinda heshima ya chama chetu na viongzi wake, matokeo unazidiwa na mihemko ya siasa zisizokuwa na tija.

Nugu zangu, kufuatia hali hii, niwaombe sana vijana wenzangu hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi ndani ya Chama Chetu cha Mapinduzi, tusimameni na kusimamia misingi na maadili ya nchi yetu kwani mimi na wewe ndiyo jicho kubwa tegezi kwa nchi na vizazi vyetu.

Tusimamieni na kuhakikisha tunawaaminisha viongozi wetu kuwa sisi vijana tukipewa mamlaka tunaweza, lakini tuwaaminishe kwa vitendo na mate ndiyo mema na siyo matendo yasiyoiridhisha jamii na taifa kwa ujumla.

Kazi tuliyonayo sisi vijana wa CCM ni kuhakikisha Rais na Mwenyekiti wetu cha CCM Taifa pamoja na viongozi wenzake waandamizi wa chama na serikali tunawasemea vizuri, tunawalinda na kuhakikisha wanafanya kazi zao bila kusumbuliwa na mtu yoyote. Hilo ndilo jukumu pekee tulilonalo sisi vijana wa Chama Cha Mapinduzi.

Viongozi hawa ni sawa na wazazi wetu ambao hatupo tayari kukuta mzazi wetu anatukanwa na kupewa kashfa ningali nipo hai.

Ndugu zangu na vijana wenzangu, tubadilikeni na tuchukue hatua za mabadiliko katika kujitunza na kuutunza muda wetu, kwa kuheshimu sheria na mamlaka zinazosimamia sheria huku tukitambua kuwa hakuna aliye juu ya sheria.

Pia tuyaishi matendo mema kwa kukihurumia kizazi chetu kinachotufuata nyuma yetu, leo viongozi wetu watatuongoza na kesho tutasimama mimi na wewe. Je, kwa hali hii tunakwenda wapi? Kwa hali hii tunalipeleka wapi taifa? Kumbe ni lazima tubadilike na tuishi kwa kufuata na kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za nchi.

Muhimu sana ifahamike simaanishi wala kuingilia kilichomkuta mdogo wangu CHIEFSON, lakini nimeona nitumie wasaa huu kwa kuwa ni muda wake, kuwashirikisha ninyi kipande hiki cha ushauri kwa maslahi mapana ya vijana wenzangu na taifa kwa ujumla.

Mwisho, nitumie fursa hii kuwapongeza sana viongozi wetu wote wa Chama Cha Mapinduzi kwa ngazi zote kuanzia na ngazi ya Taifa. Nimpongeze sana Mwenyekiti wetu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Ndg. Samia Suluhu Hassan Ndg. kwa Kazi kubwa na nzuri sana anayoendelea kuifanya ndani ya mipaka ya nchi yetu.

Kazi kubwa anafanya na hata Watanzania wanashuhudia kote shughuli na miradi ya maendeleo inatekelezeka, kwa hivyo nimpongeze sana kwa kusimamia vyema ilani yetu ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi CCM.

Pia nimpongze sana Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Ndg. Daniel Chongolo kwa kazi kubwa anayoendelea nayo ya kumsaidia Mwenyekiti majukumu yake na kukisaidia Chama chetu Cha Mapinduzi katika kila aina ya utendaji wake nchi nzima.

Tunaona matunda makubwa yanayotokana na usimamizi na utendaji mzuri sana kwa Chama chetu Cha Mapinduzi chini ya katibu mkuu Ndg. Daniel Chongolo.

Kipekee sana niwapongze sana sana viongozi wetu wote wa mikoa nchi nzima wakiongozwa na Wenyeviti wa CCM Tanzania kutoka katika kila mkoa, wakisaidiwa na Makatibu wa CCM Tanzania nzima pamoja na Viongozi Waandamizi wa Chama Cha Mapinduzi CCM kwa kazi nzuri mnayoendelea nayo katika maeneo yenu yote. Hakika watanzania wanawaelewa.

Kwa umuhimu sana naomba nitumie fursa hii kumpongeza sana Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Vijana Tanzania Ndg. Kenani L. Kihongosi kwa kazi nzuri na kubwa anayoendelea kuifanya kwa vijana wote wa nchi hii. Hakika kazi yako inaonekana na kama mimi na yule hatuioni basi Mungu wetu wa Mbinguni atakulipa wewe na familia yako.

Niwashukuru sana Wenyeviti na Makatibu wa Jumuiya ya Vijana kote nchi nzima wakiongozwa na viongozi wangu wa mkoa wa Simiyu Mwenyekiti na Katibu wake. Ninawaombea sana kwa Mungu atusimamie na kutupatia maisha marefu na yenye baraka tele.

Vijana wenzangu wote wa nchi hii niwatakie kila la kheri katika mabadiliko ya kijamii, kiuchumi na kiteknolojia kwa kulinda heshma ya chama chetu, viongzi wetu, na Taifa letu.

Mungu ibariki Afrika,
Mungu ibariki Tanzania,
Mungu ibariki CCM na
Mungu ibariki Jumuiya yetu ya UVCCM Taifa.


Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...


Imeandaliwa na kutolewa na:
CDE: John K. Joseph
Mwanacham wa Chama Cha Mapinduzi CCM na mwanamaendeleo katika mkoa wa Simiyu.

+255 715 333 330.
honjohnjoseph@outlook.com
honjohnjosephmlyambatte@gmail.com.
Screenshot_20221022-141853_Photos.jpg
 
Back
Top Bottom